Imeibuka tabia, wanafunzi waliosoma pamoja "alumni", watu walioishi mtaa mmoja, Ukoo moja na kabila, Parokia ama jumuia moja, kuanzisha vikundi vya Watsup na baadae kujisajili kuwa Rasmi.
Vikundi hivi huwa lazma kuwe na kisebengo ambaye ata-anzisha M-Koba na kutaka watu wachangieni iwapo mwenzao atapata msiba au ugonjwa wa kudumu.
Niwape siri: KUFA TUTAKUFA TU, NDUGU WASIPO KUZIKA , HALMASHAURI ITAKUZIKA MANA HAKUNA ATAKAYE KUBALI KUKAA NA MZOGA, wenzetu wenye asili ya ASIa wanaunda group za fursa za biashara, kuwekeza UTT , tuwekeze kwenye soko la hisa na Kufungua kampuni kugombea tenda, sisi tunawaza kuzikana tu.
Imekuwa ni ufahari kumzika mama yako, kumjazia maua rose, mabango ya Sijui tutakumis, kumpost marehemu status-insta, ticktok wakati akiwa hai hukuwahi kumuweka status bali ulimuweka Zuchu, Dai, na wamama wengine ambao hawakuhusu! ambayo kipindi cha uhai wake hukuwahi kumpa hata "ua mgomba" wacha mbali "rose" siku ya kinamama duniani!
Mnaweka na kuandaa Bufee, watu wale mpaka wasaze, mnaweka vinywaji vikali na bia lakini kipindi cha uhai wake alikuwa anakula mashona-nguo, mchunga na miguu ya kuku na ugalli wa jero au anashindia chai kavu !
Maziko ya mama yenu mnaleta vikundi vya ngonjera na sala na kupiga kila aina ya sifa ambayo kipindi akiwa hai hamkuwahi kufanya hivyo!
huu ni unafiki na ndio unaleta umaskini.
HITIMISHO:
Mtu yeyote, asiniunge magroup ya michango ya kuzikana, niunge kwenye group za kupeana biashara, viwanja, kazi na uwekezaji!