Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Al Watani, Wanazingati kuzikwa kwa hesha,ma kuliko kuish kwa heshma, Ndio maana hata hizi Speacil Hire ni safari za uchagani tu, bora hata wazaramo wanaenda ucheza ngoma !Kwenye kusanyiko lolote wakiwepo wachaga wawili lazima kianzishwe kikoba cha kuzikana.
Hawa watu hawajawahi kuwaza kingine beyond hela
Kipaumbele kiwe kuishi, kifo kipo tu, ni aibu kumzzika bibi au mama pale mndenyi kwa sherehe au bajeti ya milioni 20 wakati amekufa kwa njaa!Hizo hela wanizipata wapi za kuzikana kifahari?Tafsiri nyepesi ni kwamba wanafanya kazi wanawekeza pesa za nyakati za starehe na huzuni.Jambo ambalo mi naona wako Sawa.
Acha kabisa mkuu, nadhani watu hawajawahi kufiwa, hawajui kubeba mizigo ya misiba, hawajawahi kuuguza kwa miezi, hawajui relief inayopatikana ukiwa na kikundi cha watu wanaokupa support!!Siku akifa mkeo/mumeo au mtoto.
Huna hela ya kuutoa mwili Hospitalini, amefia mbali huna nauli ya kwenda kuuchukua mwili au kwenda kumzika.
Huna pesa za wachimba kaburi.
Hapo ndio utajua umuhimu wa hivyo vikundi.
Wazo lako la kusaidiana kiuchumi lilikuwa zuri pasipo kuponda wazo la michahgo ya misiba.
Au hujawahi kufiwa katika mazingira tata au hali ngumu?
Achana ni Kifo mzee.
Kama ingekuwa zamani ndugu wote mpo kijiji kimoja hapo sawa.
Lakini dunia ya leo.
Unasafiri kutoka Arusha unaelekea Dar. Unafika Segera unapata ajali unafariki.
Unafikiri mwili wako utasafirishwaje mpaka hospitalini bika gharama ya pesa? Utahifadhiwa bure hospitalini?
Unafikiri wapendwa wako watakubali uzikwe bila wao kuja kukuaga(kuaga mwili wako)
Hapo utakuwa umekufa kama kama waliopotezwa na wasiojulikana
niwape siri:KUFA TUTAKUFA TU, NDUGU WASIPO KUZIKA , HALMASHAURI ITAKUZIKA MANA HAKUNA ATAKAYE KUBALI KUKAA NA MZOGA,
Acha kabisa mkuu, nadhani watu hawajawahi kufiwa, hawajui kubeba mizigo ya misiba, hawajawahi kuuguza kwa miezi, hawajui relief inayopatikana ukiwa na kikundi cha watu wanaokupa support!!
Kipaumbele kiwe kuishi, kifo kipo tu, ni aibu kumzzika bibi au mama pale mndenyi kwa sherehe au bajeti ya milioni 20 wakati amekufa kwa njaa!
Ninakuunga mkono mleta mada. Upendo wa kweli kwenye familia lazima uwepo bila hata kuunda groups za watsapp. Kwani zamani watu walikuwa wanafanyaje bila watsapp? Sisi kwenye ukoo wetu hakuna group ila ukitokea msiba hadi aliyepo nje ya nchi atatuma mchango wake. Hivi vikundi ni show offs za kifala na kupotezeana muda. Mimi nimejitoa kwenye vikundi vyote vya watsapp ila likitokea jambo huwa nashiriki kikamilifu.
Kuna baadhi ya wanafunzi waliosoma pamoja shule za sekondari wamepiga hatua sana na wako mbali, kama wale wenzetu wa Mzumbe hawashikiki.Imeibuka tabia, wanafunzi waliosoma pamoja, watu walioishi mtaa mmoja, Koo moja na kabila kuanzisha vikundi vya Watsup na baadae kujisajili kuwa Rasmi.
Vikundi hivi huwa lazma kuwe na kisebengo ambaye atanzisha M-Koba na kutaka watu wachangieni iwapo mwenzao atapata msiba au ugonjwa wa kudumu.
niwape siri:KUFA TUTAKUFA TU, NDUGU WASIPO KUZIKA , HALMASHAURI ITAKUZIKA MANA HAKUNA ATAKAYE KUBALI KUKAA NA MZOGA, wenzetu wenye asili ya ASIa wanaunda group za fursa za biashara, kuwekeza UTT na Kufungua kampuni kugombea tenda, sisi tunawaza kuzikana tu.
Imekuwa ni ufahari kumzika mama yako, kumjazia maua rose ambayo kipindi cha uhai wake hukuwahi kumpa hata "ua mgomba" .
Mnweka Bufee, watu wale mpaka wasinzie, lakini uhai wake alikuwa anakula samaki na ugalli wa jero au anashindia chai!
Maziko ya mama yenu mnaleta vikundi vya ngonjera na sala na kupiga kila aina ya sifa ambayo kipindi akiwa hai hamkuwahi kufanya hivyo!
huu ni unafiki na ndio unaleta umaskini.
HITIMISHO:
Mtu yeyote, asiniunge magroup ya michango ya kuzikana, niunge kwenye group za kupeana biashara, viwanja, kazi na uwekezaji!
Waislamu kwenye suala la msiba wana taratibu nzuri kuliko dini zingine zote.Kuna baadhi ya wanafunzi waliosoma pamoja shule za sekondari wamepiga hatua sana na wako mbali, kama wale wenzetu wa Mzumbe hawashikiki.
Hayo ndiyo mambo yetu sisi Wakristo tu! Wenzetu waislamu wamestaraabika sana, haya mambo ya kuzikana wala sio shida zao! Sijui sanduku la gharama, gari jeusi la kukodi la kisasa kubeba mwili wa maraehemu, Tshirt, madela au sare nyeupe! Hizo zote ni gharama tu zisizo na maana yoyote.