Wachagga:Agenda za kikao cha ukoo 2026 hizi hapa!

Wachagga:Agenda za kikao cha ukoo 2026 hizi hapa!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Siku 80 tu zimebaki kabla ya wachagga kwenda kuhesabiwa huko kilimanjaro .

Tabia ya wachagga kurudi kwao kwa gharama yeyote imekuwa kivutio na inasemekana kuna makampuni ya Utali yameanza kupata booking toka nje ili "wazungu waje kuona wachagga wakirudi kwao" kama wanavyokwenda Koga Tende Serengeti kuangalia Nyumbu wakihama Kenya - Tanzania!

Katika kikao cha mwaka 2026, kuna mikakati ya kujadili.:-
  1. Kumshukuru Mungu na kutoa sadaka ya Shukrani kwa Mungu tu.
  2. Kuhesabiwa watoto wote na wajukuu.
  3. Kutambulisha watoto wa nje ya ndoa.
  4. Kutambulisha wachumba.
  5. Kutoa hesabu ya kazi uliyokuwa unafanya mjini.
  6. Kupeana fursa za kuhamia Geita, Chunya, Songwe na Morogoro kuchimba madini na vijana kuacha bodaboda , kuacha bajaji na kujihusisha na madini, ndiyo yanalipa kuliko vihela vya kizaramo.
  7. Kila mchaga aliyeko kwenye nafasi kumpa mchongo/koneksheni mtoto wa ndugu yake, kupeana fursa.
  8. Watoto wapelekwe private school hata kwa kuchangiea ili wawe wanasheria, madaktari na wanasayansi-kurudisha kilimanjaro ya miaka 1980"
Ongeza Agenda Nyingine:
 
Back
Top Bottom