Wachezaji 10 walioitendea haki jezi namba 9 dimbani

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
1,667
Reaction score
2,595
MABAO ndiyo yanayoleta ushindi kwenye mchezo wa soka. Ukizungumzia ufungaji wa mabao, wachezaji wakubwa wamefanya hivyo wakiwa na jezi namba tisa.

Kiutamaduni, jezi namba tisa ndiyo inayohusika na ufungaji wa mabao, ingawa soka la kisasa mambo yamebadilika kidogo katika mbinu – lakini kazi ya namba tisa inabaki ile ile ya kucheka na nyavu.

Kwa maana hiyo, makala haya yanawaangalia wachezaji 10 ambao wameitendea haki jezi namba tisa, twende sasa...

#10. Luis Suarez
Luis Suarez ni mmoja wa wachezaji wakubwa wanaovaa jezi namba tisa katika historia ya mchezo huo ambaye bado anacheza hadi sasa.
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Uruguay ni mmoja wa washambuliaji waliokamilika zaidi katika kizazi chake.

Katika umri wake wa miaka 34, amekuwa na mafanikio makubwa katika klabu alizozichezea; akianza kushinda taji la Ligi Kuu Uholanzi, Eredivisie, akiwa na Ajax, Kombe la Ligi na Liverpool, kabla ya kwenda kufurahia mafanikio makubwa zaidi kule Barcelona.

Suarez alishinda mara mbili tuzo ya Kiatu cha Dhahabu wakati akicheza pale Camp Nou, akifunga mabao 195 na kutoa pasi za mwisho 112. Pia alishinda mara nne taji la LaLiga, taji la Copa Del Rey (Kombe la Mfalme) mara nne na mataji matatu msimu wa 2014-15, likiwamo la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

#9. Robert Lewandowski
Nyota wa timu ya Taifa ya Poland, Robert Lewandowski, mmoja wa washambuliaji wamaliziaji bora zaidi kwenye historia ya mchezo huo. Amebarikiwa kwa kuwa na jicho la goli, amefunga mabao 454 katika klabu nne tofauti.

Lewandowski alianza maisha ya soka katika klabu ya nyumbani kwao Poland ya Znicz Pruszkow. Baada ya kucheza kwa muda Lech Poznan, alihamia kwa majirani zao Ujerumani ambako alijiunga na Borussia Dortmund.

Ilikuwa ni pale Dortmund ambako Lewandowski ndiko alijenga jina lake akifunga mabao 103 katika mechi 187 na kushinda mataji mawili ya Bundesliga na timu hiyo inayotumia jezi yenye rangi nyeusi na njano. Baada ya misimu minne, akaondoka hapo Dortmund na kwenda kwa wapinzani wao, Bayern Munich.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ameweka historia ya heshima yake hapo Munich – akishinda mataji nane mfululizo ya Bundesliga pamoja na Ligi ya Mabingwa na Klabu Bingwa Dunia pamoja na mchezaji bora wa msimu.

Lewandowski amefunga mabao 73 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kumfanya kushika nafasi ya tatu kwa wafungaji wa wakati wote wa mashindano hayo.

#8. Filippo Inzaghi
Huyu ni gwiji wa Juventus, AC Milan na Italia na bila shaka yoyote, Filippo Inzaghi alikuwa mchezaji bora zaidi kuvaa jezi namba tisa.
Inzaghi alifurahia mafanikio yake akiwa pale Rossoneri, ambako alishinda mara mbili Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji mawili ya Serie A, moja la Klabu Bingwa Dunia na Coppa Italia.

Anashika nafasi ya saba kwa wafungaji bora wa Italia na anashikilia rekodi ya kufunga ‘hat-tricks’ 10 kwenye Serie A.

katika moja ya mafanikio yake, Inzaghi alifunga mabao mawili dhidi ya Liverpool kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2007 kuwasaidia Rossoneri hao kupata ushindi wa mabao 2-1.

Inzaghi alifunga mabao 25 katika mechi 57 na timu ya taifa. Alishinda Kombe la Dunia mwaka 2006.

#7. Marco Van Basten
Marco Van Basten alikuwa mmoja wa mastraika bora zaidi miaka ya 80' na kuisaidia Uholanzi kushinda Kombe la Euro mwaka 1988.
Van Basten alikuwa mshambuliaji aliyekamilika zaidi na alifurahia mafanikio akiwa Ajax Amsterdam na AC Milan. Alishinda mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya msimu wa 1988-89 na 1989-90.
Akiwa AC Milan, alishinda tuzo ya Ballon D'Or mwaka 1988 na 1989 na kwa mara ya tatu mwaka 1992. Raia huyo wa Uholanzi wakati anastaafu soka pale Milan, alikuwa amefunga mabao 277 na kutoa pasi za mwisho 82 katika mechi 373.

#6. Gabriel Batistuta
Gwiji wa Fiorentina na Argentina, Gabriel Batistuta.

Batistuta alikuwa na misimu tisa ya kufurahia zaidi mafanikio pale Fiorentina akifunga zaidi ya mabao 200 katika mechi 331 na kuingia kwenye historia ya kipekee klabuni hapo.

Akiwa anajulikana kwa jina la 'Batigol', alimalizia soka lake pale AS Roma, akifunga mabao 184, anashika nafasi ya 11 kwa wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi kwenye historia ya Ligi Kuu Italia, Serie A.

Pia raia huyo wa Argentina, alishinda taji la Copa America 1991 na ndiye alikuwa anashikilia rekodi ya kuifungia mabao mengi timu ya taifa (56) iliyodumu kwa kipidi cha miaka 15, kabla ya kuvunjwa na Lionel Messi mwaka 2016.

#5. Alan Shearer
Alan Shearer alikuwa mshambuliaji wa hatari zaidi katika zama za soka la kisasa.

Akiwa shabiki wa Newcastle tangu utotoni, Shearer akaitosa klabu hiyo na kwenda kusajiliwa Southampton wakati akiwa kinda.

Akianza kuichezea akiwa na umri wa miaka 17, haraka Shearer akaingia kwenye vitabu vya historia wakati alipofunga mabao matatu ‘hat-trick’ dhidi ya Arsenal.

Akasajiliwa Blackburn Rovers ambako alifunga mabao 112 kwenye Ligi Kuu katika mechi 138 alizocheza na kuiongoza Blackburn kushinda taji la EPL.

Halafu akaenda kujiunga na klabu yake kipenzi tangu utotoni, Newcastle United kwa ada iliyoweka rekodi ya dunia ya pauni milioni 15.

Shearer huko ndiko alikoweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa wakati wote wa Ligi Kuu England akifikisha mabao 260.

#4. Johan Cruyff
Awali alikuwa akivaa jezi namba 14, lakini Johan Cruyff baadaye akatambulika zaidi kwa jezi namba tisa mgongoni.

Alikuwa na mafanikio makubwa kwenye jezi namba tisa akiwa mchezaji na baadaye pia kupata mafanikio akiwa kocha.

Mholanzi huyu ndiye aliyebuni na kuanzisha akademi maarufu ya Barcelona ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana 'La Masia', ambayo ndiyo iliyowatoa nyota wake wakali kama Lionel Messi, Andres Iniesta na Xavi.

Alishinda tuzo ya Ballon D'Or mara tatu na mwaka 1999, Cruyff alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Karne wa Ulaya.
Alifunga mabao 260 na pasi za mwisho 136 katika mechi 501 kwenye mashindano yote ngazi ya klabu.

#3. Gerd Muller
Mmoja wa wafungaji bora kwenye historia ya mchezo huo, Gerd Muller – ambaye alifunga jumla ya mabao 721 katika mechi 769.
Mara zote alikuwa akijulikana kwa jina la utani la 'Der Bomber' (mlipuaji), Muller anachukuliwa kama mmaliziaji wa wakati wote, akifunga mabao 68 katika mechi 62 alizoichezea iliyokuwa Ujerumani Magharibi.

Alishinda Euro mwaka 1972 na Kombe la Dunia 1974.

Mchango wa Muller pia unatambulika sana pale Bayern Munich akiwa ameshinda mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na manne ya Bundesliga.

Mshindi huyo wa Ballon D'Or alitumia miaka 15 kuichezea Bayern Munich, akifunga mabao 523 na kutoa pasi za mwisho 101 katika mechi 580.

#2. Alfredo Di Stefano
Alfredo Di Stefano alikuwa mmoja wa wachezaji bora walioubariki mchezo huo.

Raia huyo wa Argentina, ambaye baadaye akaamua kuchukua uraia wa Hispania, alikuwa nguzo muhimu kwa utawala wa Real Madrid na Hispania katika soka la dunia, karne iliyopita.

Di Stefano alishinda taji la Ulaya mara tano kuanzia miaka ya 50'. Alikuwa anavaa jenzi namba tisa na mshindi mara mbili wa Ballon D'Or.

Alfredo Di Stefano alikuwa mfungaji bora wa Real Madrid akitikisa nyavu mara 216 kabla ya kufunikwa na Raul mwaka 2009. Bado anashikilia rekodi pale Madrid ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye mchezo wa El Classicos (18).

Katika mechi 709 alizocheza ngazi ya klabu kwenye mashindano yote, alifuga mabao 519.

#1. Ronaldo Nazario
Huyu kwa waliomshuhudia hawana maneno mengi sana ya kumzungumzia zaidi ya kumtaja kama 'El Fenomeno', Ronaldo Nazario na bila shaka yoyote ndio mshambuliaji bora zaidi katika historia nzuri ya mchezo huo mzuri.

Wakati Cristiano Ronaldo amefuata nyayo zake kwenye kufunga mabao matamu, gwiji huyu wa Brazil anabaki kuwa ndiye Ronaldo kwa wale wote waliopata muda wa kutosha kumwangalia dimbani.

Alitumia muda wake wa kucheza katika nchi nne tofauti na mabara mawili, akipata mafanikio makubwa zaidi.

Mshindi mara mbili wa Ballon D'Or aliichezea PSV Eindhoven katika misimu miwili, akifunga mabao 54 katika mechi 57.

Kwa ujumla amecheza mechi 119 katika klabu mbili pinzani nchini Italia, Inter Milan na AC Milan, akifunga jumla ya mabao 68. Alitumia msimu mmoja pale Barcelona na misimu mitano Real Madrid, akifunga jumla ya mabao 151 katika mechi 226 kwa timu hizo mbiliza Hispania.

Alirudi kwenye Ligi ya Brazil akifunga mabao 79 katika mechi 116. Pia akafunga mabao 62 na mechi 98 kwa timu ya Taifa ya Brazil.

Ronaldo Nazario ni mmoja kati ya wachezaji wanne walioshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Dunia mara tatu mfululizo. Ronaldo Luis Nazario de Lima ni mmoja wa wachezaji bora zaidi ambaye anaishi.

©IppMedia
 
Ungesema wa kizazi hiki ingependeza zaidi, hao kina Van Basten na Gerd Muller nani amewahi kuwaona live huku jf nimpe zawadi?
 
Ahsante kwa muongozo mkuu, Kongole sana kwao
 
[emoji767]IppMedia
Orodha ya 10 bora bila Jurgen Klinsman? Hapana kaka.
 
Ungesema wa kizazi hiki ingependeza zaidi, hao kina Van Basten na Gerd Muller nani amewahi kuwaona live huku jf nimpe zawadi?
Van basten alikuwa most completed Stricker
ever niliye muona akicheza ,, bila majeruhi kupata Ac Milan wangekuwa na UCL kama 5 ivi
 
Waqt mmoja ruud guillit alipokuwa kocha wa Chelsea vanalipita kumtembelea basi kwa wingi waandishi wa khabari wakasogea pale mazoezini wakidhani mkongwe anataka kulamba saini akawaambia nimepita kumtembelea ndugu yangu. Ule utata wao pale rossoneri ulikuwa ukiogopwa sana ni kizazi cha dhahabu kwa umahiri wao naweza sema mafanikio makubwa kwao ni kuchukua euro 1988 nadhani walistahili zaidi ya hapo.
 
Hawa ndio striker wangu bora

1.Diego Milito
2.Alfredo
3.Alan shearer
3.Batistuta
3.Johan cruyff
3.De lima
4.Aguero
4.Suarez
4.Lewandowski

licensed-image.jpeg
images (4).jpeg

Diego Millito

images (6).jpeg
Alan shearer
 
Batistuta alikua hatari sana, mashabiki wa Man U tulimfaham mwaka 2000 alipofunga goli mbali pale OT ingawa walikufa 3-1.
images.jpg
 
Back
Top Bottom