Katika era ya CR7 na Messi usimuweke Zidane! Utakosea sana!
Zidane awekwe katika era za Ronaldo Lima, Henry, na wengineo bwana Gaucho.
Zidane na bwana Gaucho ni zama za watu wa udambwi udambwi!
Siku hizi ni nadra kuona maudambwi udambwi kama yale, ya kupiga kanzu watu wa 4!
Katika tik taka style ya barca utapiga kanzu watu wa 4 saa ngapi wakati wenzako wanataka pasi mpaka 500 half time tu.
Kwenye hii era ya andunje na Cr7 wawekwe watu ambao ni nguli wa kupiga mabao na watengeneza mabao,
Watu kama Sergio Busquet andaa headline ya kumuweka. Ipe Jina hili hapa Best Offensive Midfielders of all Time.
Hapa utamuweka Fabinho, Ng'olo Kante, Busquet, na wengineo wazee wa kukata umeme.
Mtoa mada umejaribu sana, lakini umefeli kutofautisha aina za hao watu.
Kuna mabenki bora wa kushoto duniani, mawinga bora duniani, na wengine wengi tu.