Hii mada nimeshaichangia vya kutosha, nitakuwa narudia tu majibu yangu maana majibu yenu na nyie ni yale yale tu.
Kukurahisishia tu, GSM kama siyo mmiliki ni nani? Maana ndiye anayeimbwa mkifunga magoli na siyo SportPesa ambaye ndiye mdhamini mkuu wa klabu.
Azam Media inadhamini ligi kwa kupitia mkataba wake na TFF. Azam FC ni timu. Haya ni makampuni mawili tofauti.
Mwisho, mnajichanganya na inaonyesha hamna jibu mnaloliamini pale mnapotumia Bakhresa kama mfano wa kuonyesha kuwa inaruhusiwa kumiliki timu na kudhamini timu zaidi ya moja wakati huo huo mnamkana GSM kuwa siyo mmiliki wa Yanga. Kama GSM siyo mmiliki wa Yanga, kwa nini mnatumia mfano wa Bakhresa mnayeamini ndiye mmiliki wa Azam FC na Azam Media?