Wachezaji wa kibongo nini kinawasibu, tunatamani tuone mafanikio yenu ya kisoka kama hawa wanaopita kwetu

Wachezaji wa kibongo nini kinawasibu, tunatamani tuone mafanikio yenu ya kisoka kama hawa wanaopita kwetu

Dr.adams faida

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
1,888
Reaction score
3,352
Wakuu nimekuwa najiuliza kwanini wachezaji wa kibongo bado wanafeli kutusua kucheza mpira nje ya nchi kama mataifa mengine.
Kila mwaka hatuuzi mchezaji wa ndani kwenda kucheza nje na ikitokea akaenda hamalizi msimu anarudi kupiga ndondo na tolori combine tunafeli wapi au mnafeli wapi?

Simba wameuza wachezaji wawili kwa thamani ya juu sana luis na chama inakaribia billion 5 wameweka kwenye kikapu chao na wote hawa ni wachezaji wa kigeni.

Yanga wamemuuza kisinda naye ni mchezaji wa kigeni lakini wabongo bado wanang'aa sharubu tu kwenye majaruba yetu kwanini hawasanuki?

Mbona tunawachezaji wazuri tu kucheza mataifa hayo wanayoenda wenzetu.

Mwisho wa siku wachezaji wa kigeni wamekuwa wakiitumia tz kama sehemu ya kutusulia tu vijana komaeni mnapokuwa uwanjani ,ktk msimu huu sikutegemea kama manula angeendela kusalia ligi kuu kwa kiwango alichokionesha tunafeli wapi?

Hawa wachezaji wetu wabadilike sasa kuweni na connection pia muwe na wasimamizi wenu maagent,wanasheria wanaosimamia kazi zenu muwe na malengo msicheze mpira wakimazoea soka limebadilika sana wenzetu wameshasanuka sana ndo maana wanapitia kwetu.

Leo msimu huu sijui kama tumeuza hata wachezaji wa kibongo hata watatu nje tupo tunang'aa macho tu....unakuta mchezaji anafurahia chama kuuzwa billion 1.8 alihali yeye ni mwendo wa kusugua benchi msimu mzima.

Nyinyi ndio mnadombaga mkipewa nafasi kwenye timu ya taifa kwa sababu hamna exposure ya kisoka.

Inaniuma mpaka leo miaka nenda rudi tunajivunia wachezaji wanne au watano wanaocheza nje kwenye angalau mataifa manne komaeni sana wazee kina mohamed hussein, dilunga,adam adam,waziri juniour,mwamnyeto,dickson job,dilunga, na wengine wote mnaofanya vizuri kwenye ligi kuweni na mikakati ya kusonga mbele zaidi ili nchi yetu ikue zaidi kisoka.
 
Akili za sera za ujamaa mkuu zimetulemaza Sana

Leo hii kuwa na passport ya bongo had uwe na uthibitisho wa safari

Nchi hii kwenda kutafuta maisha nje n kosa la jinai kabisa

Ukisimuliwa habar za akina etoo mane na wengneo walienda mbele na bila kupata timu na wakatusukia hukohuko kibish

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo ni kubwa.
Una mchezaji anatumia nguvu akili kidogo unatarajia atasajiliwa na nani?
 
Acha maskhara mkuu,Messi si yupo PSG[emoji23]
Ajib
Mkude
Messi
Ngassa

Hawa wote walikua wachezaji wazuri ila waliridhika na maisha ya Bongo
Lakini Singano si yupo nje huko alishafungua mipaka,mbona umemuweka kwenye urodha ya wachezaji walioridhika na soka la Bongo?
 
Akili za sera za ujamaa mkuu zimetulemaza Sana

Leo hii kuwa na passport ya bongo had uwe na uthibitisho wa safari

Nchi hii kwenda kutafuta maisha nje n kosa la jinai kabisa

Ukisimuliwa habar za akina etoo mane na wengneo walienda mbele na bila kupata timu na wakatusukia hukohuko kibish

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app

wakat naomba pasaport zile toleo la zamani wakaniambia nilete uthibitisho wa safari nikawaambia ni safari binafsi wakasema niandike barua kwa nini nipewe pasaport.. pale pale nikaandika barua fupi kuwa nipewe sababu ni haki yangu kama mtanzania..

yule afisa akaniambia mie ni jeuri.. nibadili barua yangu la sivyo atagomea ombi langu.. tulizinguana had akakubali kuhakiki form zangu.. ila kama masaa matatu hivi sibanduki dirishani ..

ila hili swala la kupewa pasaport mpaka uthibitisho wa Safar linakera sana.. mi naona passport ni kama Identity card ya taifa kila mtanzania anapaswa awe nayo atakayependa tena ina nguvu kuliko hiyo ID yenu ya NiDa sababu yenyewe inavuka mipaka ila Bongo passport kama vile unaomba visa

yaan bongo wanajifanya wao ndo mawakala au maafisa wa nchi za kigen kwenda hizo nchi mpaka eti wajiridhishe..

cha ajabu kwenye NiDA wala hawakomai yaan ID inatoka kiulaini .. ngoja wasikie unataka kuvuka mpaka.. dah
 
Wachezaji wetu hawajitumi,hawajiandai kiakili kuwa wachezaji wenye mbinu na maarifa ya kimpira.
Nahisi kukosa wasimamizi wa maendeleo ya mchezaji;naamini kuna chama cha wachezaji,kama kipo kiwape wachezaji wetu utaratibu utakaomjenga mchezaji mfano:
1.Mchezaji kuwa na meneja,mwanasheria na wakala.
2.Mchezaji kuwa tayari kujifunza lugha za kimataifa(English,french,spanish ),na wajiendeleze kielimu.
3.Wachezaji kujitengea fedha kwa ajili ya kutengeneza video za matukio yote ya uchezaji("anavyokaba,anavyotoa pasi,kukimbia,kuruka,n.k).
4.Kusimamia nidhamu binafsi(kiafya,tabia ndani ya uwanja na nje ya uwanja).

Ushauri kwa wachezaji waache kuridhika na kusajiliwa na vilabu maarafu Tanzania,wafikirie kujiendeleza, kuongeza muda wa mazoezi hata kuiga wale wachezaji waliofanikiwa zaidi.(wajifunze kwa wanamuziki wa " bongo flavour" ni kuiga na kushirikiana na wengine ili uweze kuwa na kiwango kinachokubalika sokoni.!!)
 
Wakuu nimekuwa najiuliza kwanini wachezaji wa kibongo bado wanafeli kutusua kucheza mpira nje ya nchi kama mataifa mengine.
Kila mwaka hatuuzi mchezaji wa ndani kwenda kucheza nje na ikitokea akaenda hamalizi msimu anarudi kupiga ndondo na tolori combine tunafeli wapi au mnafeli wapi?

Simba wameuza wachezaji wawili kwa thamani ya juu sana luis na chama inakaribia billion 5 wameweka kwenye kikapu chao na wote hawa ni wachezaji wa kigeni.

Yanga wamemuuza kisinda naye ni mchezaji wa kigeni lakini wabongo bado wanang'aa sharubu tu kwenye majaruba yetu kwanini hawasanuki?

Mbona tunawachezaji wazuri tu kucheza mataifa hayo wanayoenda wenzetu.

Mwisho wa siku wachezaji wa kigeni wamekuwa wakiitumia tz kama sehemu ya kutusulia tu vijana komaeni mnapokuwa uwanjani ,ktk msimu huu sikutegemea kama manula angeendela kusalia ligi kuu kwa kiwango alichokionesha tunafeli wapi?

Hawa wachezaji wetu wabadilike sasa kuweni na connection pia muwe na wasimamizi wenu maagent,wanasheria wanaosimamia kazi zenu muwe na malengo msicheze mpira wakimazoea soka limebadilika sana wenzetu wameshasanuka sana ndo maana wanapitia kwetu.

Leo msimu huu sijui kama tumeuza hata wachezaji wa kibongo hata watatu nje tupo tunang'aa macho tu....unakuta mchezaji anafurahia chama kuuzwa billion 1.8 alihali yeye ni mwendo wa kusugua benchi msimu mzima.

Nyinyi ndio mnadombaga mkipewa nafasi kwenye timu ya taifa kwa sababu hamna exposure ya kisoka.

Inaniuma mpaka leo miaka nenda rudi tunajivunia wachezaji wanne au watano wanaocheza nje kwenye angalau mataifa manne komaeni sana wazee kina mohamed hussein, dilunga,adam adam,waziri juniour,mwamnyeto,dickson job,dilunga, na wengine wote mnaofanya vizuri kwenye ligi kuweni na mikakati ya kusonga mbele zaidi ili nchi yetu ikue zaidi kisoka.
Wavivu,walevi,malaya,hawajitambui

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
mkuu umenifurahisha apo kwenye kuitàja timu ya nyumbani kwetu keko ambayo ni toroli combine ndani ya kata ya chang'ombe mtaa wa toroli.
 
Kuna kibwagizo kinasema, nchi zote alizopita Vasco zinaupiga mwingi isipokuwa TZ tu😀

Ligi ya Uingereza nayo ina tatizo kama letu isipokuwa tu, ligi hiyo tayari ni kubwa sana kuliko yetu.

Pamoja na wachezaji wetu kutokwenda nje ila ligi imeanza kukua/kusikika/kutambulika au kutazamika na mataifa mengine. Sio hatua mbaya ingawa tumechelewa sana.

Wachezaji wetu hawa hawana tofauti na kada nyinginezo hapa TZ, hatujiongezi, hatuna morali ya kujituma na wakati mwingine ikibidi, kujisusa kabisa.

Africa magharibi ni mfano wa watu wanaojituma na unaweza kuona mafanikio yao kimichezo, kimuziki n.k, Africa kaskazini ni vivo hivyo. Pembe ya Africa nayo juhudi zao za kushika mitutu zinaonekana. A. Mashariki, ni Kenya tu ndio inayoonesha jitihada hinafsi ingawa na yenyewe ni kutokana na mfumo wa nchi uliojengwa sio na wao, bali wakoloni.

Turuhusu kila mwenye nia na uwezo, achukue pasi ya kusafiria, kikwazo kiwe visa! Watu watoke wakachakarike, na si lazima aanzie TFF. Tutoke kihalali, tukakae kwa watu kihalali, tupate nafasi ya kufanya vitu kihalali, TUTAONEKANA tu.
 
Back
Top Bottom