Wachezaji wa Real Madrid wapigana mazoezini, mmoja apelekwa hospitali

Wachezaji wa Real Madrid wapigana mazoezini, mmoja apelekwa hospitali

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Nyota wa Real Madrid, Fede Valverde, ameripotiwa kulazwa hospitalini baada ya kuzuka tena kwa ugomvi mkubwa kati yake na mwenzake Aurelien Tchouameni, hali iliyoanza wakati wa mazoezi ya timu siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wachezaji hao wawili walihusika katika mabishano makali yaliyotokana na faulo iliyochezwa wakati wa mazoezi, kabla ya mvutano huo kuendelea hadi kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Inaelezwa kuwa baadhi ya wachezaji wenzao waliingilia kati kujaribu kutuliza hali kabla mambo hayajaharibika zaidi. Vyanzo vya karibu na klabu vimedai kuwa tukio la pili lilikuwa “baya zaidi” kuliko lile la awali lililotokea uwanjani mazoezini.

Ripoti hizo pia zinadai kuwa Valverde alikataa kumpa mkono Tchouameni aliporejea eneo la mazoezi, jambo lililoendelea kuongeza hali ya sintofahamu ndani ya kikosi.

Katika vurugu zilizodaiwa kutokea ndani ya chumba cha kubadilishia nguo baada ya mazoezi, Valverde alijeruhiwa kwa kipigo cha bahati mbaya wakati wa msuguano wa kimwili. Jeraha hilo lilimlazimu kwenda hospitalini kupata matibabu ya dharura.

Wakati huo huo, mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe, alionekana akiondoka katika uwanja wa mazoezi huku akicheka kwa sauti kubwa, jambo lililozua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki kwenye mitandao ya kijamii.


Chanzo: DailyMail
 
Screenshot_20260507-180314_Facebook.jpg
 
Daah timu imejaa ego sana wamlete Mourinho aje awapunguze Hawa maboya
 
Hii timu badala ya kupigania makombe wanadundana wao kwa wao.
Wachezaji wa sasa wa Real Madrid hawana spirit ya kupambania timu kutwaa makombe...wameshasahau REAL MADRID ni klabu kubwa iliyo na historia kubwa sana
 
Hawa jamaa wasipobadili hicho kikosi na mwakani hawapati kombe lolote!
Kuna watu kibao wanatakiwa kutoka hapo.
 
Timu kubwa inatakiwa kuajiri makocha wenye CV kubwa. Kinachotokea Real Madrid kwa sasa hakina tofauti na kile kinachotokea Chelsea!

Timu zote mbili ziliajiri makocha ambao hawana CV kubwa! Matokeo yake wamejikuta wanawatimua hao makocha na kubakiwa na care takers wasioheshimiwa na baadhi ya wachezaji wanaojiona ni mastaa ndani ya timu.
 
Back
Top Bottom