Soka Ndio Maisha Yangu
Member
- Nov 27, 2024
- 43
- 127
Mwaka 2024 unaisha leo, kesho majaliwa ni mwaka 2025, nimeona kikosi chote cha wachezaji wangu wa Simba Sports Club, kiukweli hadi kufikia leo binafsi ni wachezaji wawili tu ndani ya timu yangu ukimuondoa kiungo wa pembeni Elie Mpanzu ambaye ndio kwanza anajitafuta na ambaye nina matarajio naye makubwa sana kijana huyu.
Mchezaji wa kwanza ambaye amenivutia na ana mchango mkubwa mno kwa sasa ndani ya Simba ni Kibu Dennis.
Kibu kwa sasa ndio uti wa mgongo wa Simba, kwanza aliwafunga Yanga bao wakati wa mzunguko wa kwanza lakini lilikakataliwa kuwa ni offside, Kibu ametoa mchango mkubwa sana kwenye Ligi ya Mabingwa, aliwafunga Al Ahly Tripoli na kutuvusha hatua ya makundi, Kibu akawaua Cfxien ya Tunisia na kutupa sana furaha, Kibu juzi aliwapelekesha Singida Black Stars mnooo.Huyu ni assets sana kwa sasa, hakuna beki wa pembeni hapa Afrika anayetamani kukabiliana na shujaa huyu wa Simba kwa sasa.
Wa pili ni kipa Camara, aisee kuna mazingira ambayo bwana mdogo huyu ametuokoa sana wanasimba, amefanya saves katika mazingira ambayo wote tuliamini ni bao lakini kijana huyu alitusaidia sana wanasimba.
Wengine ongezeni bidii kuanzia kesho na hasa mechi kule Tunisia, tukifungwa kule Tunisia tutakuwa katika wakati mgumu sana.