Wachezaji wenye akili na hatari zaidi Mamelodi

Wachezaji wenye akili na hatari zaidi Mamelodi

Heshima pia Kwa COACH RULANI MOKWENA
Yupo vizuri Hata sub zake Zinaleta maana ya mchezo .
Alikuwa msaidizi wa Pitso wakati wanachukua ubingwa wa Afrika.
Alimtoa Mvala baada ya kuona amepata yellow kuogopa angepata red Kama mechi na Waangola.
Inasemekana familia yake wana umiliki wa Orlando pirates
 
Mzamiru anatumia AKILI?????
Mzamiru ni kiungo mwenye akili sana ila naona hatumika vizuri tu kutokana na timu aliyopo. Mzamiru ana utulivu mkubwa hasa kutokana na pressure ya eneo analocheza huwezi kutegemea mtu kuwa calm namna ile.
 
Yupo vizuri Hata sub zake Zinaleta maana ya mchezo .
Alikuwa msaidizi wa Pitso wakati wanachukua ubingwa wa Afrika.
Alimtoa Mvala baada ya kuona amepata yellow kuogopa angepata red Kama mechi na Waangola.
Inasemekana familia yake wana umiliki wa Orlando pirates
Sio inasemekana ni ukweli na ndiyo team ya mapenzi yake pale yupo kazini tu
 
Beki ya kulia ile siyo mchezo, pale kati(kiungo) mamelodi naona wana watu mno, Kuna beki moja ya kati ya mamelodi inacheza Kwa akili nyingi sana...hizi timu kuzifikia ni ngumu, naona timu nyingi za south afrika zikikutana na waarabu gemu huwaga ngumu, nadhani ubora wa ligi zao unawasukuma zaidi, we fikiri timu hata za mwisho tu za ligi ya afrika kusini zikikutana na mabingwa wa kwetu bado tunatoana jasho kweli...naona hata waarabu huzihofia timu za SA kuliko zozote barani afrika, level ya maendelea Kwa ujumla wako juu ya waarabu.
 
Najua wengi Jana tuliuangalia mpira wa Mamelody vs Al AHLY lakini ni wachache tulioangali Kwa jicho la tatu na kung'amua vipaji haswa katika kikosi kile.

1. Kuna beki mmoja wa kati kitasa haswa sura ya mama anaitwa GRANT KEKANA
Uyu bwana mdogo matumizi ya akili ni makubwa mno sawa na umchukue BACCA +INNONGA ndiyo unampata.

2. Kuna Jamaa niliezoea kumuona akicheza kama beki wa kati Jana alikuwa kiungo kutokana na kutokuwepo Kwa MOKOENA jamaa alifit na aliupiga mwingi Sana anaitwa AUBREIN MODIBA appreciation post yake hii ni anaajua kuamua mpira uchezwe Kwa speed gani Kwa sasa.

3. ALLIENDE kijana tutoka chille uyu Sina comment [emoji119]

HAO NDIYO NILIO WAONA NI ROHO YA TEAM KWA JANA.
Huyu MWAMBA hukumuangalia
Screenshot_20231102-092511.jpg
 
Ila mkumbuke waarabu na wasouth Africa hamna afadhali wote wabaguzi....
Angalizo tuu
 
Back
Top Bottom