Wachina ni noma aisee,nimeshuhudia live bila chenga!

Wachina ni noma aisee,nimeshuhudia live bila chenga!

Najiuliza tu swali moja hapa, hizo noti za shilingi 50 na 100 walikuwa nazo kwa madhumuni yapi ilihali fedha hizo hazitumiki tena...
 
Hadithi za kupikwa
Nilikuwa site pamoja na wafanyakazi wenzangu katika kampuni moja ya kichina inayojishughulisha na ujenzi wa barabara.

Siku hiyo kulikuwa na shughuli inayo involve cement kuchanganywa na material fulani kwa umbali wa kama mita 500, hii shughuli ilikuwa inahitaji mifuko 248 ya cement.

Mifuko ikaletwa na kupangwa barabarani,ikachanwa ili kuchanganya na G15 material,mara bonge la wingu likafunga lilkiambatana na ngurumo za radi za kutisha.
Ilikuwa obvious kwamba ile mvua lazima ingedondoka na kutibua shughuli yote na hatimaye hasara ya mifuko yote.

Wachina wakaitana wakachukua noti za sh.50 na sh.100 za zamani za Tanzania pamoja na magamba ya kakakuona, kisha wakajikusanya na kuongea maneno machache tu ya kichina.

Huwezi amini, lile wingu lilipotea ghafla, anga likawa jeupe na mzigo ukapigwa ile kisawasawa,

Hawa watu ni wachawi ila uchawi wao una manufaa kwao.
 
jamani haya makitu sijui ila kuna siku sie tulikuwa tumealikwa kwenye sherehe sehemu kupika.basi acha mvua ianze kunyeshaa bonge la mvua akina mama wakaaomba sh 50 na 100 kwa wenyeji wetu waliotualika. wakatupia jikoni na mvua ikakatika na mapishi yakaendelea basi nilibaki jisho limenitoka hata sikuamini.
 
hii kali ila watanzania wataacha lini huu upuuzi wa hizi imani?
 
Back
Top Bottom