Wachina wakamatwa wakizalisha vinywaji feki Dar?

Wachina wakamatwa wakizalisha vinywaji feki Dar?

1703713229175.png
 
Kweli aisee yaani jamaa wanatoka Asia wanakuja kupiga hela sisi tumelala. Jiulize kwao wanaweza kutengeneza kinywaji fake? Hapa kwetu wameweza tuwape kongole tuu maana hatuna akili hii.
Ata wa tz wanatengeneza nenda rombo utalijua hilo.
 
Kama ni mla K Vant na Moet, basi hii ni kwa ajili yako. Yasemekana hao mabwana kutoka Asia ya Mashariki wamekamatwa jijini Dar wakiwa kwenye ‘karakana’ yao la kufyatua kopi za vinywaji hivi murua.

Hivi huwa wanapataje vifungashio visivyotia shaka?

Kwa uchafu wa hayo madumu, huenda yanahifadhia molasses. Na kama ndivyo, ningependezwa kuona mtambo wao na mchakato wa kukopi ladha na harufu za hivi vinywaji. Bado nabaki na maswali kedekede.

Nimestushwa zaidi na hiyo paint roller na rangi kwenye beseni, sijui vina kazi gani Mungu wangu!

View attachment 1899801View attachment 1899802View attachment 1899805View attachment 1899809
"Hivi huwa wanapataje vifungashio visivyotia shaka?" Vifungashio vyote Tanzania vinatoka kwao China na vinapatikana Kariakoo na Gerezani, usishangae koo kuwa na kifaranga wakati koo ndio hutaga mayai.
 
Hao madogo 2 kwenye picha wasifungwe. Wanavipaji watafika mbali ni hadhina ya baadae kwa taifa.
 
Kwa serikari yetu inavyowakumbatia hawa jamaa Nafikiria kuacha kunywa Pombe kabisa.
 
Hawa jamaa ni wahuni sana. Sipati picha nchi walikojaa kama Angola na Zambia hali ikoje?
SHUGHULI ZAO ZIRASIMISHWE, WAPIGWE FAINI KWANZA, WAELEKEZWE NJIA SAHIHI ZA KUPITIA ILI WAZALISHE KWA TRADE MARK ZAO WENYEWE, NDIYO TUNAKWENDA SASA KWENYE INDUSTRALISATION.
 
Back
Top Bottom