Wachina wakamatwa wakizalisha vinywaji feki Dar?

Kweli aisee yaani jamaa wanatoka Asia wanakuja kupiga hela sisi tumelala. Jiulize kwao wanaweza kutengeneza kinywaji fake? Hapa kwetu wameweza tuwape kongole tuu maana hatuna akili hii.
Ata wa tz wanatengeneza nenda rombo utalijua hilo.
 
"Hivi huwa wanapataje vifungashio visivyotia shaka?" Vifungashio vyote Tanzania vinatoka kwao China na vinapatikana Kariakoo na Gerezani, usishangae koo kuwa na kifaranga wakati koo ndio hutaga mayai.
 
Hao madogo 2 kwenye picha wasifungwe. Wanavipaji watafika mbali ni hadhina ya baadae kwa taifa.
 
Kwa serikari yetu inavyowakumbatia hawa jamaa Nafikiria kuacha kunywa Pombe kabisa.
 
Hawa jamaa ni wahuni sana. Sipati picha nchi walikojaa kama Angola na Zambia hali ikoje?
SHUGHULI ZAO ZIRASIMISHWE, WAPIGWE FAINI KWANZA, WAELEKEZWE NJIA SAHIHI ZA KUPITIA ILI WAZALISHE KWA TRADE MARK ZAO WENYEWE, NDIYO TUNAKWENDA SASA KWENYE INDUSTRALISATION.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…