johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 104,319
- 183,639
Hivi bado kuna Wazamia meli kizazi hiki cha dot.com?!
Hivi bado kuna Wazamia meli kizazi hiki cha dot.com?!
Mkuu kweli kumtosa binadamu ni kosa la jinai.Nahodha na mabaharia wa Meli ya wachina wawatupa Watanzania baharini kwa hofu ya kuambukizwa Corona
Nahodha na mabaharia wa Meli ya Wachina wamekiri kosa la jaribio la mauaji kwa kuwatupa watanzania wawili baharini kutoka kwenye meli ya mizigo iliyokuwa inaelekea katika bandari ya Durban, Afrika Kusini kwa hofu ya Watanzania hao kuwaambukiza virusi vya Corona.
Wakipewa chupa mbili za maji kila mmoja na jaketi la kusaidia kutozama kwenye maji, Amiri Salamu (20), na Hassani Rajabu (30) waliambiwa kuwa wapige mbizi hadi wafike nchi kavu kwa kutumia mikono yao kama makafi.
Kwa siku tatu, hawakula na walibahatika kusafirishwa na mawimbi hadi katika ufukwe wa Zinkwazi, karibu na Durban, linasema gazeti la Daily Mail la nchini Uingereza.
Mara baada ya kupokea taarifa hizo, The African Maritime Safety Agency ilikamata meli hiyo ya MV Top Grace ilivyotia nanga katika bandari ya Richards Bay na nahodha alikamatwa mara moja.
Nahodha huyo Cui Rongli, pamoja na mabaharia wake Lin Xinyong, Zou Yongxian, Tan Yian, Xie Wenbin, Xu Kun na Mu Yong wote walikiri kosa la jaribio la mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Durban siku ya Ijumaa.
Nahodha Rongli alipigwa faini ya dola 5000 huku mabaharia wakipigwa faini ya dola 2500 kila mmoja ili kumaliza shauri.
Msemaji wa Jeshi la Polisi la Afrika Kusini, Natasha Cara aliliambia gazeti la Daily Mail kuwa ‘’watuhumiwa waliwapa wahanga majaketi ya uokozi na mabaharia wakawatishia na kuwarusha baharini. Meli ikaondoka na kuwaacha wakiwa baharini. Watuhumiwa wamekiri kuwa kitendo walichofanya kingeweza kusababisha majeraha makubwa na hata kifo’’, alisema
Wakili wa Utetezi, Willie Lombard akiwatetea wateja wake alisema ‘’hatua muhimu za kiusalama zilichukuliwa, na ikiwa mabaharia walikuwa na nia ya kuwa wakatili wangewatupa watu hao mbali kabisa na nchi kavu tena bila jaketi ya uokozi’’
Watanzania hao wamechukuliwa na kupatikwa matibabu na mamlaka za Afrika Kusini na hivi sasa wanaendelea vizuri. Wakati wanaokolewa, walikutwa na hali mbaya ya kiafya inayotokana na baridi na ukosefu wa chakula.
Hivi karibuni, kumeibuka wimbi la malalamiko kwa Waafrika kubaguliwa na raia wa China hasa wale waliopo nchini China. Katika taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya kimataifa, inaonesha waafrika wengi wakiwa wametengewa katika maeneo ya umma na hata kufukuzwa katika nyumba wanazoishi na kulazimika kulala nje mitaani kwa madai kuwa wana maambukizi ya Virusi vya Corona.
Hata hivyo, Serikali ya China kupitia msemaji wake ilisema kuwa si sera ya taifa hilo kuwabagua wageni na kwamba ubaguzi wa rangi hauvumiliki.
Chanzo Taarifa:
Daily Mail Newspaper
serengetipost.co.tz
MY TAKE:
Kinachonisitikisha na Kuniuma sana kama si mno GENTAMYCINE ni Kuona Sisi Watanzania ( hasa kupitia Viongozi au Watawala wetu ) wakiwa ' Wanajipendekeza ' kwa Wachina na Serikali yao huku Wachina hao hao pamoja na Kujifanya wanatupenda Watanzania na wanatusaidia kwa Misaada mbalimbali lakini ndiyo hao hao ambao wanatuumiza kama hivi walivyowafanyia Watanzania wenzetu.
Hao washukuru wamepewa maji na life jacket wazungu wangewashikisha ukuta na wangetoswa majini bila Life jacket
Mkuu kweli kumtosa binadamu ni kosa la jinai.
Lakini nikuulize swali hivi ukiwa umelala nyumbani kwako ghafla usiku unagundua mtu amejificha uvunguni mwa kitanda utamchukulia hatua gani?
Hao vijana ni wahalifu,kwa kuingia melini bila idhini ya mamlaka ya meli.
Pili hakuna ajira bila mkataba,kwa hiyo kupenda meli haikupi ajira.
Ili upewe ajira unapitia mambo mengi mbali mbali kama vyeti vya kazi,passport, vaccination card,medical fittiness certificate, drug free certificate, seaman book, Fingerprints ,mandatory certificates n.k,baada ya hapo wahakiki vyeti vyako kama una sifa ya kuajiriwa katika meli ya bendera ya nchi husika.
Vijana sampuli hii hawajui sifa wala kazi za baharia kwa miaka ya sasa,bado wanadhani ni hadithi za miaka ya 70 hadi 80.
Mkuu mimi Ubaharia ni fani yangu nimejifunza kazi hii kwa miaka 15 hadi kufikia ngazi ya mhandisi mkuu kwenye meli za kimataifa na kwasasa nina karibu miaka 40 kwenye kazi na kufanya na watu wa mataifa mbali mbali.
Niseme tu,Ubaharia kwa miaka 20 iliopita una vigezo vingi sana kufuzu kuwa BAHARIA.
Naunga mkono hoja.Wanaccm tuwachangie faini ndugu zetu wa damu na tulaani mahakama kutowatendea haki ndugu zetu wachina.
Mtetezi wa wachina, chama chenye undungu wa damu na ccm. Asante Mr. Chong Wan.Hao washukuru wamepewa maji na life jacket wazungu wangewashikisha ukuta na wangetoswa majini bila Life jacket
Kwani utani washukuru mungu uzamie meli za wazungu wakupe maji na life jacket? Wakufanyia kitu mbaya na wanakutosa kwenye maji ukaliwe na [emoji1655] sharksMtetezi wa wachina, chama chenye undungu wa damu na ccm. Asante Mr. Chong Wan.
Sent using Jamii Forums mobile app
Chadema pia kina undugu na wakoloni waliberali watetea mashogaMtetezi wa wachina, chama chenye undungu wa damu na ccm. Asante Mr. Chong Wan.
Sent using Jamii Forums mobile app