Wachina wanasubiri Rais Magufuli aondoke kwenye bandari

Wachina wanasubiri Rais Magufuli aondoke kwenye bandari

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Mradi wa bandari ya bagamoyo ambao ulikuwa mbaya sana haujafutwa kwa ujumla wake. Kuna watu wengi serikalini wamekaa mkao wa kula wakisubiri Magufuli aondoke ili warudishe mradi kwa manufaa yao binafsi. Kuna watu wengi sana walikuwa wameshawekwa mfukoni.

China watahakikisha wanatumia kila namna kujenga bandari na sio kwa manufaa ya Tanzania lakini ni kwa manufaa yao ya kumiliki bandari muhimu zote Duniani hasa kwenye bahari ya Hindi. Hivyo nia yao sio kutoa mkopo bali ni kumiliki bandari Tanzania. Kwa sasa wanatumia Chama cha Mapinduzi kwa kupitia huko kwa kisingizio cha uhusiano wa Chama lakini wanataka wawaweke sawa hawa viongozi wa ndani ya chama na watu wote wanaomzunguka Magufuli ili iwe rahisi kumchagua mtu wao urais ujao.

Kama Magufuli anataka kweli kuuwa huu mradi ni kugawa ile sehemu kwa wawekezaji wa viwanda, kusema kwa uwazi wote mradi umekufa. Hata kama wakibadilisha maneneo kwenye mkataba wanaweza kuja kuhonga baadae na kubandika maneneo mengine kwenye mkataba.

Kikubwa ni kwamba nia ya China ni kuhakikisha DRC na Zambia vitu vyao wana control kuanzia vinakotoka mpaka China bila kuhojiwa wala kuulizwa. Huu ni kama ukoloni na tusikubali huu mkataba hata kama wakisema mkataba unabadilishwa. Lakini kingine hii bandari haina umuhimu tayari tuna bandari za kutosha.


Is Sri Lanka Really a Victim of China’s ‘Debt Trap’?
 
Magufuli akitaka afanikiwe jambo hili, asilifanye kutafuta kiki ya kisiasa, kama hulka yake ilivyo. Nasema hivyo kwa sababu, rasilimali huwezi kuzilinda hivi hivi, kama hauna demokrasia ya kweli kweli katika jamii unayoiongoza.

Vinginevyo na yeye atataka aone maslahi yake; na akiua upinzani tu tumekwisha. Kuna miradi sugu ni sumu kwenye hivi vi nchi vyetu ndani ya bara la afrika.

Sijaona kiongozi wa kupambana na mabeberu, in Tanzania bado hatujapata brave and smart leader mpaka sasa, waliopo hawayatazami matatizo yetu serious.
 
Kwa hiyo aendelee kutawala ili alinde bandari??

Hapana yale maeneo yatolewe kwa wajenga viwanda, hoteli na biashara nyingine. Kuna wengi sana wanasubiri kula pale na wanajaribu sana kumsahaulisha.
 
Kila zama na zama zake wanaweza subiria akiondoka na wakajenga vilevile.
 
Hilo ndilo lengo la mleta mada anatumia kisingizio cha Bandari kuharalisha kuwa Rais wa milele
Milele ataishi zaidi ya 50 yrs ,ukomo wa mwanadamu ni 80,90.
Hata wengine walikimbiza nje pesa zao wasifirisiwe alipoonda sokoine na Nyerere wakarudisha mitaji yao.
 
Kuna haja gani kujenga bandari mbili katika umbali mfupi?

Akili za Chadema bwana, mtaishia hivyo hivyo
South Africa zipo Bandari kubwa nyingi East London, Port Elizabeth, captown na Darban zote ni kubwa na kila Bandari ina majukumu yake, Mfano Bandari ya Darban ni ya kimataifa inahudumia mataifa mengi na hizo Bandari zingine ni za kazi zingine ikiwemo meli kiasi za kimataifa pia.
 
Huu mradi naona kama vile umekufa kwa sura ya nje ila ndan bado unaendelea kama kawaida sababu bagamoyo sasaiv naona wamejenga ma godaun ya kufa mtu Sasa sijui hayo magodaun ni ya nn kama sio io Bandar
 
Milele ataishi zaidi ya 50 yrs ,ukomo wa mwanadamu ni 80,90.
Hata wengine walikimbiza nje pesa zao wasifirisiwe alipoonda sokoine na Nyerere wakarudisha mitaji yao.
Rais mpya wa Malawi kamuondolea kinga ya kutoshitakiwa Rais wa zamani na yule IGP wa malawi aliyekuwa akitoa Amri za kuwaonea wapinzani kama Tanzania na yeye kafukuzwa kazi, huenda wameona malawi sasa wanasaka mbinu za kutafuta visingizio vya kubakia madarakani mpaka kuzeekea ikulu kama Rais wa Cameroon.
 
Wewe mlugaluga ulisoma mashariti ya hiyo bandari ya wachina pale bagamoyo?

Au unabweka km mjinga
South Africa zipo Bandari kubwa nyingi East London, Port Elizabeth, captown na Darban zote ni kubwa na kila Bandari ina majukumu yake, Mfano Bandari ya Darban ni ya kimataifa inahudumia mataifa mengi na hizo Bandari zingine ni za kazi zingine ikiwemo meli kiasi za kimataifa pia.
 
Hatuhitaji tena hiyo Bandari,Magufuli ameshatuzindua akili mpaka sisi walala hoi tuliokuwa hatujui nini kilikuwa kinaendelea...
 
Back
Top Bottom