Wachina wanasubiri Rais Magufuli aondoke kwenye bandari

Huu mradi naona kama vile umekufa kwa sura ya nje ila ndan bado unaendelea kama kawaida sababu bagamoyo sasaiv naona wamejenga ma godaun ya kufa mtu Sasa sijui hayo magodaun ni ya nn kama sio io Bandar
ikumbukwe watu walilipwa mabilioni ya shillingi kama fidia ni pesa nyingi sana zimepotelea humo Bagamoyo kama hakuna Bandari ina maana waliolipwa pesa watazirejesha? au nyumba zao viwanja vyao ni mali ya Serikali?
 
Rais mpya wa Malawi kamuondolea kinga ya kutoshitakiwa Rais wa zamani na yule IGP wa malawi aliyekuwa akitoa Amri za kuwaonea wapinzani kama Tanzania na yeye kafukuzwa kazi, huenda wameona malawi sasa wanasaka mbinu za kutafuta visingizio vya kubakia madarakani mpaka kuzeekea ikulu kama Rais wa Cameroon.

Katiba si msahafu kwa muona mbali uona kesho yake.Katiba haimkingi mtu dhidi ya uovu aliowatendea mabaya wenzake.Afrika mfumo ukishakutupa huna chako waweza fanywa chochote na aliyepo.
 
Issue si Magufuli. Chama chochote kitakachothubutu kutuyawala kama awamu ya nne ni kukifutilia mbali ndo maana Rais Magufuli na team yake wanatakiwa kumpika mtu kumwandaa kulinda masilahi ya watanzania.

Tunajua viongozi wetu wengi wana vichwa kama vya mende .mfano ni yule DC ambaye ndugu zake huko china wanabaguliwa kuwa ni wachafu wananuka yeye yuko busy kuwagawia ardhi wachina hao na kuwanyang'anya wazawa.

Chama cha mapinduzi awamu ya tano kimenufaika na nyota ya magufuli ila kiukweli viongozi wengi humo ni walafi wanaokula bila kunawa. Ni jukumu la magufuli kumwandaa mzalendo wa kutetea raslimali zetu.
 
Hapana yale maeneo yatolewe kwa wajenga viwanda, hoteli na biashara nyingine. Kuna wengi sana wanasubiri kula pale na wanajaribu sana kumsahaulisha.
Hata ukiyatoa maeneo hayo kwa wafanyabiashara tambua kwamba tunahitaji bandari nyingine moja au mbili zenye viwango vya kimataifa. (Bandari ya Tanga na Mtwara)
 
Kwa mkataba ulivyokuwa hiyo bandari ya bagamoyo ingeua bandari ya Dar

Yaani mkataba ulikuwa unakataza bandari ya dar kupokea mizigo inayoenda nje ya Nchi
Na pia huo mkataba Tanzania haturuhusiwi kukusanya kodi kwa miaka 999
Bandari nyingi uchochea uchumi,ujui ya bagamoyo itahudumia kaskazini,na Kanda ya ziwa,plus nchi jirani
 
Lengo la Bandari ya Bagamoyo ilikuwa ni kuua soko la Dubai, Qatar, Oman Bidhaa zote za huko zinazokuja Africa ziletwe Bagamoyo waje kukunua hapo, ingekuwa ni Bandari kubwa Africa nzima na kampuni kubwa za magari na bidhaa zingine zingewekeza Bagamoyo, Reli kiwanja cha Ndege kingine kingejengwa Bagamoyo , pengine Bagamoyo ingekuja kugeuka kuwa Dubai ya Africa, wamekwamishwa kisa wamegoma kutoa 10% kwa Naibu Rais ndugu Bashite na wenzake, lakini wakiamua kutoa 10 hata mda huu nina hakika Bandari itajengwa kwani Bandari ya Dsm ina kina kifupi na ipo uchochoroni meli kubwa za kimataifa hushindwa kufika.
 
ikumbukwe watu walilipwa mabilioni ya shillingi kama fidia ni pesa nyingi sana zimepotelea humo Bagamoyo kama hakuna Bandari ina maana waliolipwa pesa watazirejesha? au nyumba zao viwanja vyao ni mali ya Serikali?

Ile sehemu ni mali ya serikali au Watanzania wote kwa ujumla. wagawe kwa uwekezaji maalumu lakini hakuna haja ya badari hasa kwa kukopa China au kuendeshwa na hawa jamaa. China wameshasema niya yao ya kuwa na bandari huru na wamesema watatumia kila njia
 
Dawa sio kumkimbia mchona na kukimbilia kwenye Janga lingine kubwa. Dawa ni kutafuta mwekezaji mwengine mkubwa ambaye interest yake itakuwa ni huo mradi pekee, na hana nia nyingine kama, mauzo ya vitokavyo viwandani mwake, au usombaji wa maligafi. Kwa mfano mwekezaji kama Dubai Port World ( DPW ), Abu Dhabi Investment nk..
 
Kwa mkataba ulivyokuwa hiyo bandari ya bagamoyo ingeua bandari ya Dar

Yaani mkataba ulikuwa unakataza bandari ya dar kupokea mizigo inayoenda nje ya Nchi
Na pia huo mkataba Tanzania haturuhusiwi kukusanya kodi kwa miaka 999
Hivyo visingizio ni propaganda za CCM ili kuharalisha Uongo wao, kila Bandari ingekuwa na majukumu yake, Mfano wangeamu Bandari ya Dsm iwe Bandari ya meli za mafuta, bidhaa za ndani ya Nchi na kusafirisha bidhaa, Bandari ya Tanga inafanya kazi sawa na ya Dsm na Hiyo Bandari ya Bagamoyo ingekuwa ni Bandari ya kimataifa tu hakuna kupitisha bidhaa za ndani.
 
Lengo la Bandari ya Bagamoyo ilikuwa ni kuua soko la Dubai, Qatar, Oman Bidhaa zote za huko zinazokuja Africa ziletwe Bagamoyo waje kukunua hapo, ingekuwa ni Bandari kubwa Africa nzima na kampuni kubwa za magari na bidhaa zingine zingewekeza Bagamoyo, Reli kiwanja cha Ndege kingine kingejengwa Bagamoyo , pengine Bagamoyo ingekuja kugeuka kuwa Dubai ya Africa, wamekwamishwa kisa wamegoma kutoa 10% kwa Naibu Rais ndugu Bashite na wenzake, lakini wakiamua kutoa 10 hata mda huu nina hakika Bandari itajengwa kwani Bandari ya Dsm ina kina kifupi na ipo uchochoroni meli kubwa za kimataifa hushindwa kufika.

Yaani unayosema yamesemwa na China na sio Tanzania na wenywe ndiyo walikuwa wanajaribu kudanganya manufaa yake. Nenda hizo nchi walizojenga bandari na mikataba hiyo wamejimilikisha kwa miaka 99 na hayo unayosema yanashindikana vipi sasa!!!! kwani hatuna bandari
 
Hata ukiyatoa maeneo hayo kwa wafanyabiashara tambua kwamba tunahitaji bandari nyingine moja au mbili zenye viwango vya kimataifa. (Bandari ya Tanga na Mtwara)
Naibu Rais Daud Bashite kasema Wachina wasipompa 10% yake hakuna cha Bandari wala kitu gani.
 
Wewe kumbe ni giza totoro kichwani! Nyie ndio Chadema mnajiita wasomi!

Unajua kitu hichi kilichobuniwa na china?
Lengo la Bandari ya Bagamoyo ilikuwa ni kuua soko la Dubai, Qatar, Oman Bidhaa zote za huko zinazokuja Africa ziletwe Bagamoyo waje kukunua hapo, ingekuwa ni Bandari kubwa Africa nzima na kampuni kubwa za magari na bidhaa zingine zingewekeza Bagamoyo, Reli kiwanja cha Ndege kingine kingejengwa Bagamoyo , pengine Bagamoyo ingekuja kugeuka kuwa Dubai ya Africa, wamekwamishwa kisa wamegoma kutoa 10% kwa Naibu Rais ndugu Bashite na wenzake, lakini wakiamua kutoa 10 hata mda huu nina hakika Bandari itajengwa kwani Bandari ya Dsm ina kina kifupi na ipo uchochoroni meli kubwa za kimataifa hushindwa kufika.
20200701_162656.jpg
 
We mlugaluga wacha nikuache na ujinga wako
Nchi ya Sirilanka ambayo ni developed country imepokonywa bandari na China kwa kushindwa kulipa mkopo wa ujenzi wa bandari!
Huo mkataba wa china ulikuwa wa kilaghai ni mpuuzi tu angeweza kukubali
Hivyo visingizio ni propaganda za CCM ili kuharalisha Uongo wao, kila Bandari ingekuwa na majukumu yake, Mfano wangeamu Bandari ya Dsm iwe Bandari ya meli za mafuta, bidhaa za ndani ya Nchi na kusafirisha bidhaa, Bandari ya Tanga inafanya kazi sawa na ya Dsm na Hiyo Bandari ya Bagamoyo ingekuwa ni Bandari ya kimataifa tu hakuna kupitisha bidhaa za ndani.
 
Kuna haja gani kujenga bandari mbili katika umbali mfupi?

Akili za Chadema bwana, mtaishia hivyo hivyo
Atakuja kiongozi mwingine hii miradi akikuta ataipiga chini naye atafanya yake

Ova
 
Wewe kumbe ni giza totoro kichwani! Nyie ndio Chadema mnajiita wasomi!

Unajua kitu hichi kilichobuniwa na china?View attachment 1494413
Kwanini unawalaumu Cdm katika hili sakata ?!. Waliokula rushwa kuingia mikataba mibovu ni hao hao wana Ccm . Na aliyezuia ni hao hao Ccm, sasa Cdm insinhiaJe humu ?! Au usipowataja siku haihesabiki ?! UNAKERA
 
Magufuli akitaka afanikiwe jambo hili, asilifanye kutafuta kiki ya kisiasa, kama hulka yake ilivyo. Nasema hivyo kwa sababu, rasilimali huwezi kuzilinda hivi hivi, kama hauna demokrasia ya kweli kweli katika jamii unayoiongoza.

Vinginevyo na yeye atataka aone maslahi yake; na akiua upinzani tu tumekwisha. Kuna miradi sugu ni sumu kwenye hivi vi nchi vyetu ndani ya bara la afrika.

Sijaona kiongozi wa kupambana na mabeberu, in Tanzania bado hatujapata brave and smart leader mpaka sasa, waliopo hawayatazami matatizo yetu serious.
Ni kweli kabisa hatuna kiongozi anayeweza kupambana na mabeberu manake aliyepo ndio kabisa kilaza wa diplomasia na hata hajui lugha na wala jinsi ya kukaa kwenye kiti na watu wastaarabu na kuzungumza kwa hoja. Yeye atataka atoe maagizo ya kienyeji kwa wachina au wazungu haiwezekani. Hayo yanawezekana kwa wateule wake wanaomwabudu na sio kwenye round table discussion. Kwa sasa tusubiri rais ajaye baada ya huyu tyrant.
 
Kwanini unawalaumu Cdm katika hili sakata ?!. Waliokula rushwa kuingia mikataba mibovu ni hao hao wana Ccm . Na aliyezuia ni hao hao Ccm, sasa Cdm insinhiaJe humu ?! Au usipowataja siku haihesabiki ?! UNAKERA
Huyo ni zuzu wa ccm achana naye.
 
Kwa mkataba ulivyokuwa hiyo bandari ya bagamoyo ingeua bandari ya Dar

Yaani mkataba ulikuwa unakataza bandari ya dar kupokea mizigo inayoenda nje ya Nchi
Na pia huo mkataba Tanzania haturuhusiwi kukusanya kodi kwa miaka 999
Mungu wangu. Sasa unambie hao ni watanzania ama majambazi yaloingia mkataba kama huo maana yake bandari ilikuwa inaua uchumi wetu. Zitto na Ndugai kuna kitu gani mpaka wanautetea huo mkataba.
 
Back
Top Bottom