Wachina wanasubiri Rais Magufuli aondoke kwenye bandari

Wachina wanasubiri Rais Magufuli aondoke kwenye bandari

Magufuli akitaka afanikiwe jambo hili, asilifanye kutafuta kiki ya kisiasa, kama hulka yake ilivyo. Nasema hivyo kwa sababu, rasilimali huwezi kuzilinda hivi hivi, kama hauna demokrasia ya kweli kweli katika jamii unayoiongoza.

Vinginevyo na yeye atataka aone maslahi yake; na akiua upinzani tu tumekwisha. Kuna miradi sugu ni sumu kwenye hivi vi nchi vyetu ndani ya bara la afrika.

Sijaona kiongozi wa kupambana na mabeberu, in Tanzania bado hatujapata brave and smart leader mpaka sasa, waliopo hawayatazami matatizo yetu serious.
Hakuna nchi yenye demokrasia ya kweli kweli duniani! Mpaka sasa sisi Tanzania tunazidi nchi nyingi kidemokrasia.
 
Kwakuwa eneo lililotengwa kwa mradi wa bandari ya Bagamoyo ni 'ideal' kwa bandari kubwa ya kisasa, si Jambo la busara kuacha kabisa kuijenga bandari hiyo bali ni kutafuta njia mbadala ya kuanzisha na kuuendeleza ujenzi huo!
NB: Bandari ya Dar imechoka, na msongamano wa magari jijini unapunguza 'efficiency' yake!
 
NB: Bandari ya Dar imechoka na msongamano wa magari jijini unapunguza 'efficiency' yake!
ili Bandari ijengwe lazima Naibu Rais na wajanja wachache wapewe 10% kwanza bila hilo hakuna Bandari mpaka siku wakizeeka na kufa ndipo mchakato utaendelea tena
 
Sio China tu anarondoe mtu wa msimamo kama JPM atoke, ila manyang'au wote wakiwemo "watasha".

The New Confessions of an Economic Hit Man by John Perkins - PDF Drive

Ukisoma shuhuda za John Perkins ametoa models kadhaa namna mikopo inakuja na econometrics ili kuwashawishi watawala wa nchi za ulimwengu wa 3 kusaini miradi kama uliotakiwa ufanyike Bagamoyo wakijua una nafasi kubwa ya kushindwa kulipa katika muda wa makubaliano; hivyo wanachukua walichojenga kwa hela zao na kukiendesha kwa muda ambao "wataona" unarejesha hela zao,
Tanzania ina rasilimali nyingi ipo vizuri usifananishe Tanzania na sehemu zingine Duniani, hakuna kinachofanya Tanzania ikashindwa kulipia chochote
 
Hata hiyo SGR lilikuwa suala la muda tu,huo mkopo wao hali ingekuwa kama Kenya vile.

Wanataka waendeshe wao hadi 2027!!
 
Bandari ya Dsm ipo kichochoroni imejibana sana kina cha maji ni kifupi sana, meli kubwa hazifiki hapo na hata zile meli kubwa za wasitani zikija hupanga foleni majini kusubiria kushusha mizigo kuna usumbufu mapungufu mengi kwenye Bandari ya Dsm ndiyo maana mataifa mengi yameikimbia Bandari hiyo na kuhamia mombasa kenya, Beira msumbiji, Namibia, Angola South Africa, kikwete aliona hilo ndipo akaja na wazo la Bandari kubwa ya Bagamoyo lakini wajanja wachache huko CCM wameikwamisha kwa kudai 10%
Haina 10% so wapiga dili wameitelekeza
 
Huu ni Ujinga, hata kama China wakimiliki hiyo Bandari Tatizo liko wapi? Duniani Kote bandari nyingi tu zinamilikiwa na Private Operators, Serikali kazi yake ni kukusanya Kodi Ushuru mbalimbali

Umekurupuka kasoma sera za china za kumiliki bandari halafu uje na hoja
 
Bandari ya Dsm ipo kichochoroni imejibana sana kina cha maji ni kifupi sana, meli kubwa hazifiki hapo na hata zile meli kubwa za wasitani zikija hupanga foleni majini kusubiria kushusha mizigo kuna usumbufu mapungufu mengi kwenye Bandari ya Dsm ndiyo maana mataifa mengi yameikimbia Bandari hiyo na kuhamia mombasa kenya, Beira msumbiji, Namibia, Angola South Africa, kikwete aliona hilo ndipo akaja na wazo la Bandari kubwa ya Bagamoyo lakini wajanja wachache huko CCM wameikwamisha kwa kudai 10%

Tatizo la TZ so bandari bali ni barabara na treni. Haya ni maneno ya kulishwa
 
Hata ukiyatoa maeneo hayo kwa wafanyabiashara tambua kwamba tunahitaji bandari nyingine moja au mbili zenye viwango vya kimataifa. (Bandari ya Tanga na Mtwara)

Sijui kama umeelewa hili bandari haitakuwa ya kwetu😂😂 hiyo ndiyo point yenyewe yaani ni kama china hata blendera yao wanaweka, bei yao. Wanaosema magodauni ni ya kuuza vitu kutoka kwao. Magu kaeleza bado watu wazito kuelewa
 
Mkuu naomba kuuliza! Huo mktaba ulishasainiwa? Pili kama ulishasainiwa kwa nini usivunjwe au tuanzishe majadiliano mapya na China ili kuurekrbisha?

Tatizo la Tanzania ni kusaini mikataba ambayo haina tija mfano ni kwenye madini. Mikataba mingi ya madini ni wizi mtupu na watanzania wenzetu walisaini kwa niaba yetu na haijavunjwa licha ya mapungufu yaliyopo.
 
South Africa zipo Bandari kubwa nyingi East London, Port Elizabeth, captown na Darban zote ni kubwa na kila Bandari ina majukumu yake, Mfano Bandari ya Darban ni ya kimataifa inahudumia mataifa mengi na hizo Bandari zingine ni za kazi zingine ikiwemo meli kiasi za kimataifa pia.
lakini hazimilikiwi na wachina
 
Rais ajaye ni mimi, na mimi ni kauzu zaidi ya Magu,wachina hapa wamenoa,Tanzania kwanza,mengine baadae
 
Mradi wa bandari ya bagamoyo ambao ulikuwa mbaya sana haujafutwa kwa ujumla wake. Kuna watu wengi serikalini wamekaa mkao wa kula wakisubiri Magufuli aondoke ili warudishe mradi kwa manufaa yao binafsi. Kuna watu wengi sana walikuwa wameshawekwa mfukoni.

China watahakikisha wanatumia kila namna kujenga bandari na sio kwa manufaa ya Tanzania lakini ni kwa manufaa yao ya kumiliki bandari muhimu zote Duniani hasa kwenye bahari ya Hindi. Hivyo nia yao sio kutoa mkopo bali ni kumiliki bandari Tanzania. Kwa sasa wanatumia Chama cha Mapinduzi kwa kupitia huko kwa kisingizio cha uhusiano wa Chama lakini wanataka wawaweke sawa hawa viongozi wa ndani ya chama na watu wote wanaomzunguka Magufuli ili iwe rahisi kumchagua mtu wao urais ujao.

Kama Magufuli anataka kweli kuuwa huu mradi ni kugawa ile sehemu kwa wawekezaji wa viwanda, kusema kwa uwazi wote mradi umekufa. Hata kama wakibadilisha maneneo kwenye mkataba wanaweza kuja kuhonga baadae na kubandika maneneo mengine kwenye mkataba.

Kikubwa ni kwamba nia ya China ni kuhakikisha DRC na Zambia vitu vyao wana control kuanzia vinakotoka mpaka China bila kuhojiwa wala kuulizwa. Huu ni kama ukoloni na tusikubali huu mkataba hata kama wakisema mkataba unabadilishwa. Lakini kingine hii bandari haina umuhimu tayari tuna bandari za kutosha.

Is Sri Lanka Really a Victim of China’s ‘Debt Trap’?

Eboo! Wanasubiri mpaka Magufuli aondoke madarakani? awali ya wote Magu yupo mpaka 2035 na mpaka hapo atapatikana Edward Moringe Sokoine II na Mwl Nyerere III(for your information Magu ni NyerereII)!!! - Shirika la Ndege (ATCL) limeshafufuliwa with 11 planes, Reli - Usafiri wa garimoshi Dsm - Arusha umefufukiwa , na mengine mengi!!
 
Magufuli akitaka afanikiwe jambo hili, asilifanye kutafuta kiki ya kisiasa, kama hulka yake ilivyo. Nasema hivyo kwa sababu, rasilimali huwezi kuzilinda hivi hivi, kama hauna demokrasia ya kweli kweli katika jamii unayoiongoza.

Vinginevyo na yeye atataka aone maslahi yake; na akiua upinzani tu tumekwisha. Kuna miradi sugu ni sumu kwenye hivi vi nchi vyetu ndani ya bara la afrika.

Sijaona kiongozi wa kupambana na mabeberu, in Tanzania bado hatujapata brave and smart leader mpaka sasa, waliopo hawayatazami matatizo yetu serious.
Endelea kuota mchana, JPM kakuambia yeye huwa haoti mchana, ni USIKU TUUUUU.Endelea kusubiri
 
Eboo! Wanasubiri mpaka Magufuli aondoke madarakani? awali ya wote Magu yupo mpaka 2035 na mpaka hapo atapatikana Edward Moringe Sokoine II na Mwl Nyerere III(for your information Magu ni NyerereII)!!! - Shirika la Ndege (ATCL) limeshafufuliwa with 11 planes, Reli - Usafiri wa garimoshi Dsm - Arusha umefufukiwa , na mengine mengi!!

Ufalme uwekwe Tanzania. Nafikiri ushabiki wenu mnajisahaulisha kwamba Watanzania ni hatari kuliko mnavyofikiri. Nyerere alishidwa hii nchi, vijiji vya ujamaa vilishidwa, kuiga China ilishindikana jiulize ni kwanini. Sababu moja ni kwamba watanzania ni mkusanyiko wa wakabila mengi sana, dini zote , mila tofauti hutaweza kuwapelekesha kama punda iko siku watagoma. Tanzania sio China wala Rwanda
 
Kwakuwa eneo lililotengwa kwa mradi wa bandari ya Bagamoyo ni 'ideal' kwa bandari kubwa ya kisasa, si Jambo la busara kuacha kabisa kuijenga bandari hiyo bali ni kutafuta njia mbadala ya kuanzisha na kuuendeleza ujenzi huo!
NB: Bandari ya Dar imechoka, na msongamano wa magari jijini unapunguza 'efficiency' yake!

Hakuna sababu ya msingi ya kuwa na bandari mbili Dar wakuze badari ya Tanga
 
Kuna haja gani kujenga bandari mbili katika umbali mfupi?

Akili za Chadema bwana, mtaishia hivyo hivyo

We dada una mambo? Hapa Chadema inaingiaje?? Chadema inaishi kichwani mwako bila kulipa hata kodi!

Unasahau mradi huu ni wa Kikwete?? Unasahau hata Spika aliutetea na kamati ya Bunge kufanya ziara UChina??

Chuki yako dhidi ya Chadema inakubalika lakini una wajibu wa kujitendea haki kwa kuwa mkweli kwa nafsi yako!!
 
Back
Top Bottom