Wachina wasio na vibali vya kufanya kazi nchini,wazidi wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya.

Wachina wasio na vibali vya kufanya kazi nchini,wazidi wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya.

Katika yote niliyo andika hapo, umeona mahali popote nikitaja CHADEMA; na kwa nini unanihusisha na CHADEMA. Hilo ndilo litakalo kuwa jibu la kuwa punguzia shida ya ajira waTanzania wa Itumbi?

Naona haupo makini.
Wewe ni chadema??
 
Uhamiaji wapo busy kuwauliza vijana wanaotaka Passport maswali ya ajabu ajabu au wanaotaka kusafiri kupitia mpaka wa Tunduma kama vile sio raia huku wakiacha majukumu yao ya msingi Wageni wapo wengi sana Tanzania wakifanya kazi bila kibali chochote na wengine wanakuja na mitaji mikubwa kitu ambacho hauwezi kufanya Nchi za watu..
 
DSO,OCD, uhamiaji na mbunge ndio walinzi wa wachina
 
Wachina hao ,hawana faida eneo Hilo Bali ni kuvuna madini na kuondoka nayo.
1. Walio ajiriwa na wachina 200,000 kwa mwezi
2. Kodi wachina hawalipi hata sent Tano.
3. Barabara ni mbovu, hawawezi hata kuchangia ujenzi wake
4. Eneo halina maji safi na salama,hawana uwezo hata wa kuchangia uwepi wa maji safi
5. Hakuna shule ya sekondari, mbunge amelala usingizi, na wachina hawawezi kuchangia hata mfuko mmoja wa cement ili shule ijengwe.
6. Hakuna stand ya mabasi, na mabasi ni mengi.
7. Hakuna kituo cha polisi,usalama ni zero.
8. Hakuna vyoo vya umma Wala vya watu binafsi, kipindu pindu Kila Kona
9. Umeme wa REA,upon ila maeneo mengi wananchi wanawasha vibatari
10. Meneja wa Taneso chunya ni mzigo,kazi yake ni kufungia wachina umeme wa migodini raia wanawasha vibatari.
11. Maelfu ya nyumba za raia hazina umeme!
12. Migodi karibia yote Haina vyoo,watu wanajisaidia porini.
13. Maksmpuni makubwa ya uchimbaji,hayachangii mirafi ya kijamii ya Kijiji,.
14. TRA chunya,imelala usingizi, haitembelei wateha Wala kutafuta wateja wapya, wanasubiri Rais akakope WB
 
Wachina wameshahonga wahusika. Hakuna wanachoweza kufanywa kwa Sasa mpaka atakapotokea Tena mzalendo.
 
Jaman ni mm au macho yangu kuna mtanzania anachukia wachina ??? Mm sijapata ona watu poa kama wachina yaan huku kwetu tumewapa hadi wake
 
Back
Top Bottom