Wachokonozi waachiwa huru, wakamatwa tena na kushtakiwa upya

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Leo Julai 21, 2025 wamiliki wa jukwaa la mtandaoni la #wachokonozi Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko, leo wamefikishwa kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa ajili ya kusomewa hoja za awali katika kesi ya jinai inayowakabili, kabla ya kuachiwa huru na kukamatwa tena mara baada ya kutoka mahakamani.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa mawili. Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo kwa njia ya mtandao, kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015. Kosa la pili ni kutoa maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni, kinyume na Kifungu cha 116(3)(b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 marejeo ya mwaka 2020.

Washitakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Juni 27, 2025 ambapo walikana mashtaka yote mawili na kupatiwa dhamana, kwa kuwa makosa hayo yanadhaminika kisheria. Kesi hiyo ilipangwa kuendelea Julai 21 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.

Hata hivyo, katika kikao cha leo, upande wa Jamhuri uliiambia Mahakama kuwa haujajiandaa kuwasilisha hoja hizo hivyo hawapo tayari kuendelea na shauri hilo kwa sababu ambazo hawakuziweka wazi, jambo lililoilazimu Mahakama kutoa amri ya kuwaachia huru washitakiwa kwa mujibu wa sheria.

Hata ivyo mara baada ya washitakiwa kutoka nje ya viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, walikamatwa tena na askari wa Jeshi la Polisi na kupelekwa katika Mahakama ya Wilaya ya Meru, ambako walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe. Sodeyeka, kwa ajili ya kusomewa upya mashtaka hayo hayo.

Baada ya hakimu kusikiliza hoja za pande zote mbili ameitaka upande wa jamuhuri kuhakikisha wanakamilisha upelelezi kabla ya Agosti 13, 2025 ambapo shauri hilo limepangwa kuanza kusikilizwa

Katika shauri hilo, washitakiwa wote wawili wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa. Kila mtuhumiwa amedhaminiwa na wadhamini wawili kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya Shilingi milioni tatu kwa kila mmoja.

Watuhumiwa wote wanawakilishwa na mawakili Ally Mhyellah na Simon Mbwambo kutoka mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC)

Video: Millard Ayo
 
View attachment 3413357
Video: Millard Ayo
CCM buana ina akili kama za kuku wa kisasa
 
Mambo mengine yanawezekana Tanzania tu.

Uwezi mshitaki mtu kwa makosa yale yale baada ya kuachiwa au kupatikana na hatia katika mahakama nyingine.

Hiyo ni kanuni ya ‘Double Jeopardy’ lazima itakuwa kwenye sheria moja wapo ‘penal code’ au ‘Criminal Justice/procedure Act’.

Sasa kesi ile ile kwa mashtaka yale inapoenda mahakama nyingine na ikafunguliwa uoni kuna uwalakani wa watu mbali judge, prosecutor na defence; wote itakuwa uelewa wao wa sheria una shida.
 
DAH inasikitisha Kuna WATU hawataki kabisa watanzania wawajadili hata wakikosea inaumiza SANA one day yes

Kwishaaaaaa

Bro Alex on da beats yoow
 
Back
Top Bottom