Wachokonozi waachiwa huru, wakamatwa tena na kushtakiwa upya

Wewe nani kakwambia kua Wayahudi ni wakristo? wayahudi hawaamini unachokiamini wewe wala sio wakristo,sasa vipi uingize kukashifu imani za wengine? imetajwa Israel haikutajwa dini yeyote ile,kwa mujibu wa dini yako,hao wayahudi ndio waliomtesa Mungu wako na kumsulubu,

Moderator Cookie Boqin Fang Paw Payge Maxence Melo

Kwanini hawa watu wanapokashifu Uislamu hua mnawaacha?
Kwani huwaoni wenzako wanaokashifu ukristo,au wewe kipofu?
 
Leo Julai 21, 2025 wamiliki wa jukwaa la mtandaoni la #wachokonozi Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko, leo wamefikishwa kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa ajili ya kusomewa hoja za awali katika kesi ya jinai inayowakabili, kabla ya kuachiwa huru na kukamatwa tena mara baada ya kutoka mahakamani.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa mawili. Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo kwa njia ya mtandao, kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015. Kosa la pili ni kutoa maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni, kinyume na Kifungu cha 116(3)(b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 marejeo ya mwaka 2020.

Washitakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Juni 27, 2025 ambapo walikana mashtaka yote mawili na kupatiwa dhamana, kwa kuwa makosa hayo yanadhaminika kisheria. Kesi hiyo ilipangwa kuendelea Julai 21 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.

Hata hivyo, katika kikao cha leo, upande wa Jamhuri uliiambia Mahakama kuwa haujajiandaa kuwasilisha hoja hizo hivyo hawapo tayari kuendelea na shauri hilo kwa sababu ambazo hawakuziweka wazi, jambo lililoilazimu Mahakama kutoa amri ya kuwaachia huru washitakiwa kwa mujibu wa sheria.

Hata ivyo mara baada ya washitakiwa kutoka nje ya viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, walikamatwa tena na askari wa Jeshi la Polisi na kupelekwa katika Mahakama ya Wilaya ya Meru, ambako walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe. Sodeyeka, kwa ajili ya kusomewa upya mashtaka hayo hayo.

Baada ya hakimu kusikiliza hoja za pande zote mbili ameitaka upande wa jamuhuri kuhakikisha wanakamilisha upelelezi kabla ya Agosti 13, 2025 ambapo shauri hilo limepangwa kuanza kusikilizwa

Katika shauri hilo, washitakiwa wote wawili wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa. Kila mtuhumiwa amedhaminiwa na wadhamini wawili kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya Shilingi milioni tatu kwa kila mmoja.

Watuhumiwa wote wanawakilishwa na mawakili Ally Mhyellah na Simon Mbwambo kutoka mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC)

View attachment 3413357
Video: Millard Ayo
Harafu Kuna mtu atasema wanaonewa wakati kumbe ni kweli hawana leseni.

Mimi ni shabiki wao ila sio Kwa Kila wanachoongea.Wafuate sheria za
Nchi .
 
Wewe nani kakwambia kua Wayahudi ni wakristo? wayahudi hawaamini unachokiamini wewe wala sio wakristo,sasa vipi uingize kukashifu imani za wengine? imetajwa Israel haikutajwa dini yeyote ile,kwa mujibu wa dini yako,hao wayahudi ndio waliomtesa Mungu wako na kumsulubu,

Moderator Cookie Boqin Fang Paw Payge Maxence Melo

Kwanini hawa watu wanapokashifu Uislamu hua mnawaacha?
Mkuu mbona umekurupuka? Hii reply yako imeendana na nilichopost?
 
Tunaojibu huu uzi tunahitaji leseni kwa haya maudhui tunayosambaza?
 
Ardhi yenye amani, rutuba na bila kusahau maji uliyoyataja na sio jangwani ambapo mvua wanaishia kuiona YouTube
tokea enzi hizo wanakombolewa huko utumwani,wamekuwa ni watu wa kuishi kwa miujiza,watu wauome utukufu wa Mungu kupitia wao.
 
Leo Julai 21, 2025 wamiliki wa jukwaa la mtandaoni la #wachokonozi Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko, leo wamefikishwa kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa ajili ya kusomewa hoja za awali katika kesi ya jinai inayowakabili, kabla ya kuachiwa huru na kukamatwa tena mara baada ya kutoka mahakamani.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa mawili. Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo kwa njia ya mtandao, kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015. Kosa la pili ni kutoa maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni, kinyume na Kifungu cha 116(3)(b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 marejeo ya mwaka 2020.

Washitakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Juni 27, 2025 ambapo walikana mashtaka yote mawili na kupatiwa dhamana, kwa kuwa makosa hayo yanadhaminika kisheria. Kesi hiyo ilipangwa kuendelea Julai 21 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.

Hata hivyo, katika kikao cha leo, upande wa Jamhuri uliiambia Mahakama kuwa haujajiandaa kuwasilisha hoja hizo hivyo hawapo tayari kuendelea na shauri hilo kwa sababu ambazo hawakuziweka wazi, jambo lililoilazimu Mahakama kutoa amri ya kuwaachia huru washitakiwa kwa mujibu wa sheria.

Hata ivyo mara baada ya washitakiwa kutoka nje ya viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, walikamatwa tena na askari wa Jeshi la Polisi na kupelekwa katika Mahakama ya Wilaya ya Meru, ambako walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe. Sodeyeka, kwa ajili ya kusomewa upya mashtaka hayo hayo.

Baada ya hakimu kusikiliza hoja za pande zote mbili ameitaka upande wa jamuhuri kuhakikisha wanakamilisha upelelezi kabla ya Agosti 13, 2025 ambapo shauri hilo limepangwa kuanza kusikilizwa

Katika shauri hilo, washitakiwa wote wawili wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa. Kila mtuhumiwa amedhaminiwa na wadhamini wawili kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya Shilingi milioni tatu kwa kila mmoja.

Watuhumiwa wote wanawakilishwa na mawakili Ally Mhyellah na Simon Mbwambo kutoka mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC)

View attachment 3413357
Video: Millard Ayo
"Leo Julai 21, 2025 wamiliki wa jukwaa la mtandaoni la #wachokonoziJackson Kabalo na Joseph Mrindoko, leo wamefikishwa kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa ajili ya kusomewa hoja"! Kwani Arusha saa zenu ni tofauti na za Tanzania!
 
Tanzania tunaishu kwenye maziwa na asali ila hatuwafikii hao jamaa hata punje
bro tambua kwamba kuna Duniani na Guniani watanzania tunawaza october tunatick na kushabikia Hamas vs Israel, US vs China
 
tokea enzi hizo wanakombolewa huko utumwani,wamekuwa ni watu wa kuishi kwa miujiza,watu wauome utukufu wa Mungu kupitia wao.
Kama haya mambo ya netanyahu ni miujiza -- basi ni hatari sana aise
 
Tanzania kama nchintumefika sehem ambayo viongozi wako very comfortable mpaka hawataki kuongelewa au kukosolewa na wananchi haswa mtandaoni. Yaan watafanya kila namna ilimradi mkosoaji awekwe matatani nakunyamazishwa, ikiwezekana hata apoteze uhai. Hichi kitu tunazidi kukuona kila kukicha nachakusikitiaha zaidi nikwamba kuna baadhi ya watanzania wenzetu wanaona ni sawa kabsa. Watanzania wenzangu hapa tulipofika sio sehemu yakupuuzia makovu na uonevu unaoendelea kwenye nchi yetu pendwa, WATANZANIA TUAMKE KUTOKA KWENYE USINGIZI NAKUNYAMAZI WOVU
Kiufupi ni kwamba tukifumbia macho huu uovu tutakutana na majibu yake mbeleni

#TanzaniaAmka
#SiasaZaKukandamiza
#SiasaZaTumboLanguKwanza
#UpuuziUnaendelea
#BackeBenchers
 
bro tambua kwamba kuna Duniani na Guniani watanzania tunawaza october tunatick na kushabikia Hamas vs Israel, US vs China
Uko sahihi.
My point is,MUNGU anaweza kukuweka au kufanya lolote lile.
 
Kweli watu hubadilika,Jack alikua msabato mzuri tu!!
 
Back
Top Bottom