‘Wachokonozi’ wapandishwa kizimbani Arusha kwa ‘Makosa ya Kimtandao’

‘Wachokonozi’ wapandishwa kizimbani Arusha kwa ‘Makosa ya Kimtandao’

Kabisa, ngoja wapigwe pini za kutosha kisha wakafungwe wachokonolewe vizuri gerezani
Watu hawajatazama video zao kujua upuuzi wanaoongelea hawa wachokonozi. Ni vijana waliojaa dharau na ujuaji. Kuna clip wanakebehi watu kumwita Rais mama... nikauliza wanataka aitwe baba? Wamepost ujinga mwingi sana kwenye social media.
 
Wangekuwa wanaimba na kusifu mama mamaa mamaaa wala wasingekamatwa!
Mahaba ya kiukweli kbs ya Sa100 kwa watz walio wengi (ukiacha uchawa na kupalilia teuzi) ni ya kufosi!!!.
Huyu mama hatoshi kwenye urais!
 
Hilo kosa la pili ni wazi kabisa wanalichomoa. Hilo la kwanza ngoja tuone facts za Jamhuri zimekaaje. Ila ilo la pili wala hazihitajiki facts sababu kwanza kwa content zao hawahitaji leseni.

Hao sio chombo cha habari. Hichi kitu wamekoshindwa kweli Jamhuri kukiona na kuachana na ilo kosa?.

Anyway.
 
Refer to Mrisho Mpoto, ile nyimbo yake ya mjomba wakati wa JK ilimuweka kando na watawala, sasa hivi baada ya kuusoma mchezo kageuka vuvuzela na mwendo wa ngiri kila anapofanya ziara za ndani nchi Mama basi Mrisho Mpoto ni kama mkia humkosi anavuta per diem zake na bahasha daily.

Na vile amejuwa kukaririshwa miradi na figure basi Mama humwambii kitu kwa Mpoto.

Hiyo ndio Tanzania yetu ilipofikia.
Ile nyimbo ilimuweka kwenye wakati mgumu....ndomana kaishia kusifiasifia

Ova
 
Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko wanaojulikana kama “Wachokonozi” jana Juni 27, 2025 walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kushtakiwa kwa makosa mawili ya kuchapisha taarifa za uongo kinyume na kifungu namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrimes Act) na kosa la pili ni kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na leseni kinyume na kifungu namba 116(3)(b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Kanuni za Maudhui Mtandaoni).

Baada ya kusomewa mashitaka, Kabalo na Mrindoko walipatiwa dhamana kutokana na makosa wanayotuhumiwa nayo kuwa na sifa ya kupata dhamana na hivyo kesi hiyo itatajwa tena kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za awali Juni 21 Julai 2025.

Watuhumiwa wote wanawakilishwa na mawakili Ally Mhyellah na Simon Mbwambo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Vijana hao walikamatwa Juni 20, 2025 katika Kijiji cha Maji ya Chai wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha na Kamanda wa Polisi mkoa huo, Justin Masejo alithibitisha kukamatwa kwao
Muungano ufe Tanganyika iwe huru
 
Tatizo kumbe liko kwaMahakama. Badala ya kuwaadhibu kwa ukalu.liwe fundishonkwa wengine wanawakumbatia na kuwapa ushujaa. Kama mathalani mtu kama Askofu Bagonza akikamatwa na kuhukiwa haraka kwa matamshi yake ya kicjocjezi, hatorudia tena na wale walikuwa wanataka wawe kama yeye mathalani Padri Kitima hawatathubutu kufanya uchochezi kwani yataeapata yaliyompata mwenzao. Kenya hivo hivo, Mahakama zinawatetea. Na Mawakili kama Kibatala au Madeleka nao hivo hivo wanatukuzwa kwa kuhojonmaseali ya kijinga na kuwadhalilisha Polisi wakimtetea Gaidi kama Mbowe au Haini kama Lissu. Jamii inatakies kuwabana Mahakama, hawatudaidii.
 
Watu hawajatazama video zao kujua upuuzi wanaoongelea hawa wachokonozi. Ni vijana waliojaa dharau na ujuaji. Kuna clip wanakebehi watu kumwita Rais mama... nikauliza wanataka aitwe baba? Wamepost ujinga mwingi sana kwenye social media.
Wapo sahihi yule ni rais wa nchi sio mama nchi, vijana na watoto wa 2000 rais Samia ni kama bibi yao na wazee wengine Samia ni kama mdogo wao au dada yao

Mbona Magufuli alikuwa haitwi baba Magufuli
 
Mlindoko anajifanya mjuaji sana wacha asulubishwe tu tuone hizo energy anazozizungumziaga kama zitamsaidia
 
Wapo sahihi yule ni rais wa nchi sio mama nchi, vijana na watoto wa 2000 rais Samia ni kama bibi yao na wazee wengine Samia ni kama mdogo wao au dada yao

Mbona Magufuli alikuwa haitwi baba Magufuli
Keyboard warrior mnawaponza sana vijana wapuuzi kama wachokonozi... dola ina njia nyingi za kuwaadabisha watu kama wewe
 
Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko wanaojulikana kama “Wachokonozi” jana Juni 27, 2025 walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kushtakiwa kwa makosa mawili ya kuchapisha taarifa za uongo kinyume na kifungu namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrimes Act) na kosa la pili ni kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na leseni kinyume na kifungu namba 116(3)(b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Kanuni za Maudhui Mtandaoni).

Baada ya kusomewa mashitaka, Kabalo na Mrindoko walipatiwa dhamana kutokana na makosa wanayotuhumiwa nayo kuwa na sifa ya kupata dhamana na hivyo kesi hiyo itatajwa tena kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za awali Juni 21 Julai 2025.

Watuhumiwa wote wanawakilishwa na mawakili Ally Mhyellah na Simon Mbwambo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Vijana hao walikamatwa Juni 20, 2025 katika Kijiji cha Maji ya Chai wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha na Kamanda wa Polisi mkoa huo, Justin Masejo alithibitisha kukamatwa kwao
Wana bahati sana wamerudi next tym hawaturudi na wala kujua wamechukuliwa na nani.
 
Back
Top Bottom