Wachumi Na wafanyabiashara tushauriane, naanzisha biashara ya kukopesha

Mawazo yako yamenifanya ni subscribe topic..
 
Mawazo yako yamenifanya ni subscribe topic..
Kabisa kabisa ndo njia ambayo nimeona ni sahihi nimekuja Na mpango kazi UO, naajiri kijana mmoja kwa ajili ya kuwapitia Na kukusanya , nimeshampata Ila ntaanza Na wamama 25 TU kutest
 
Kwa Madiba, watu kama wewe tunawaita mashonisa! Majambazi yanayojifanya yanakopesha hela. Hiyo riba yako inatafsiri moja tu, nayo ni wizi.
 
Ukitaka kuifaidi biashara hii jitahidi ujisajiri, ukifanya ki undugundugu inaweza kukugharimu kwani mtu anaweza kuchelewesha marejesho then ukaenda kunadi dhamana zake na yeye akapiga hatua mbele ukajikuta hatiyani.Pia rekebisha riba maana ni kubwa kiasi na muda ni mfupi, mfn, niliwahi kufanya biashara hii na nikafanikiwa. Pia kabla ya kuangalia riba unayotaka kutoza angalia pia mazingira ya wateja wako km yanawafaa kufanya mzunguko wa fedha hadi wakarejesha kwa wakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii biashara ilikua nzuri enzi za jk japo hata kwa sasa inafanyika ila changamoto zake zmekua nyingi so umakini unahitajika mkubwa sana,mbinu mojawapo ni kupunguza riba ikizd sana iwe 30% kwa mwez na pia ubahatike kukutana na mtu anaeheshimu mkopo na inabd ujue chanzo cha hela cha mteja wako ni kipi na akitoa rejesho kwenye revenue yake anabaki na hela ya kuyamudu maisha yake kama ni hapana atashawishika kukusumbua na kama ni mzoefu wa madeni imekula kwako.ninaifanya hii biashara ila am about to quit ntakufa vchomi nkiwa bado mdogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sorry mkuu

Kufanya hii biashara ni lazima uisajir!??
Mie niko kilosa.. Na plab kuwa na kopesha wakulima vip !??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Powa ajira ngumu nimeamua niuze kiplot changu nipate 5,000,000 yaan hapo nimeshapiga mahesabu ma feasibility study ya kutosha
Hakikisha umejisajili kisheria na una leseni za biashara kama mtoa mikopo vinginevyo tegemea kesi za kufa mtu ambazo zitakufilisi.
 
Kwa kipind hik utakopo weng na utadhulumiwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli,na nimeliona. Ila nashauri,kuepuka hilo,anza kukopesha kwa hatua. Anayetaka laki,achukue nusu,akirudisha,apewe lets say,robo tatu na kuendelea. Pia kopesha wamama na anza na wanaotaka hela ndogondogo huku unacheki mwitikio.
 
Hiyo riba ni kubwa sana kwa week,fanya 30% kwa mwezi,kwasasa nchi hii mzunguko wa pesa uko chini sana hakuna mtu atakayeweza kurudisha pesa ndani ya week.

Fanya riba ambayo ni affordable,20-30%,

Then hakikisha fomu ya mkopo inachukuliwa kwa 10,000.ili kusaidia kuziba gapes
 
kwa week afu mariba makubwa hivyo?utakopesha wehu tuu
 
Ni biashara nzuri lakini yenye laana! Mwanzoni utaenda vizuri sana halafu itafika kipindi utaanza kuporomoka, utajikuta una dhamana nyingi zisizouzika.. Hasa viitu vya umeme havikawii kuisha fasheni
Kitu kingine kibaya kwenye hii biashara ni hiki hapa, kuna mali zilipatikana kwa kutumia ushirikina au zilitumika kwenye mambo ya kishirikina, huko ziliko zikaleta kasheshe na mabalaa na haziuziki, unaletewa kwa njia ya bond unatoa hela.... Baada ya hapo sasa utaanza kupambana na hali yako yakhe

Jr[emoji769]
 
toka nje ya Dar es salaam nenda mikoani tena wilayani hiyo Biashara itakulipa kwa mjini pasua kichwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…