FURSA SI NDO HII SASA!
Ushauri wenu wakubwa ni muhimu sana,
September mosi nina mpango wa kuanzisha kabiashara haka,
Niko dar es salaam ,
Mkopo rahis wenye mashart nafuu,
Nitaanzisha ukopeshaji kwa wahitaji wa hela kiasi Kidogo kidogo,
Kiasi cha kukopesha riba Na muda wa kurejesha
1. 50,000 ndani ya wiki moja 75,000 inarejeshwa,
2. 75,000 ndani ya wiki moja inarejeshwa 110,000
2. 100,000 ndani ya wiki moja inarejeshwa 140,000
3. 200,000 ndani ya wiki moja 280,000
Mpango ni kuwa watakaozidi 200,000
Kwa wanaotaka zaid ya laki 200,000-400,000
Marejesho ni miezi miwili kila week amarejesha ifuatavyo
200,000 kila week anarejesha 40,000
300,000 kila week 60,000
400,000 kila week anarejesha 80,000
Dhamana nayokubali
1. Telephone
2. Radio sub woofer
3. Laptops
4. Desktops
5. Pikipiki
6. Projector
7. Photocopiers
8. Printers
9. Kipande Cha eneo
Hatua husika nahakikisha kisheria kuwa Mali iliyowekwa dhamana ni ya muhusika kweli siyo kuiba alafu ukaleta ,
1.Utatakiwa uwe Na kitambulisho chako 2.Receipt ya kifaa unachoweka dhamana,
3. Picha yako ya karibuni
4. Barua ya kukutambulisha unapokaa,
MUHIMU: ukipitisha siku moja bila kuleta hela Mali inauzwa HAPA KAZI TU,
Ushauri wenu katika haya
1. Je kuna haja ya kufungua ofisi maana mi mtaji si Mkubwa ofis itamaliza hela yangu, Bora tukopeshane kiundugu ndugu,
2. Je soko kwa wakopaji limekaaje?
3. Vipi kuuza Mali aloweka dhamana si inaweza leta msuko suko?
Asante yakhee
ILA HELA NGUMU NIKIFIRIA KUWEKEZA ALAFU MTU ASINILIPE SIJUI NTAFANYAJE,
Updates nimefika hatua hii kitu kinaanza
Nimemaliza taratibu zote September project hii