Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
TOA USHAURI HAPA, MBONA YEYE AMEKUJA KUOMBA USHAURI HADHARANI?Kwa maelezo yako inaonekana upo mwanza. Nicheck inbox nikupe ushauri
Acha kulalamika hapa ndugu makanisa ya T A G ni mengi rafiki ama kabisa tafuta kanisa lingine la TAG.Sifa kubwa ya mchungaji ni kuwa na huruma.Wakuu habarini
Mimi ni muumini wa kanisa la mahali pamoja ambalo ni T.A.G(X)
Jana nimepokea ujumbe wa kunikwaza kunifedhehesha na kunifanya nione kama natwaga maji kwenye kitu
Jana mchungaji kanitumia msg akiniuliza mbona sijahudhuria jana kanisani? Au na mpango wa kuhama kanisa !!
Nami 'nikamjibu kwa kumpigia simu nikamwambia mbona nilikuandikia msg kuwa nadharula sitahudhuria ibadani hukuupata ujumbe na nilimtumia pia na mzee nikakata simu nikascreen short msg nikamtumia whatsap
Akanijibu kuwa dharula zipo ila kama ni siku ya ibaada utume sadaka na michango , ni muhimu sana nikaa kimya
Leo Asubuhi nimeamka asubuhi nikiwa na ratiba ya kutoka kumpeleka mama yangu mzazi cliniki ya dialysis Bugado wakati natoa kausafiri kwenye chasis number alikuwa anapita tukasalimiana na kumwambia tunaelekea Hospital akasema sawa na hongera nyingi za kunua kausafiri kapya.
Imefika saa nne nipo hospitali naona Msg tena
akiniandikia ujumbe unasomeka hivi"
Leo ni mwisho wa mwezi na jana haukuwepo ibadani Tuma sasa hivi FUNGU LAKO LA KUMI UTUME NA HELA YA KUTOLEA KANISA LINA MADENI MENGI ""
Nikausoma nikatulia nakuvuta pumzi nikamtumia msg KUWA KWA SASA SINA PESA, FEDHA NINAYOBAKIA NAYO NI KWA AJILI YA MATUMIZI MUHIMU YA FAMILIA NAJUA PIA ZAKA UMUHIMU WAKE, nikikaa sawa nitatoa wala haina shida na hapo ndio nilikuwa najiandaa kulipia matibu ya mama kila mwezi natakiwa kulipia Milion 3 .8 kwa ajili ya dialsis ,mwez huu mambo yameyumba kabisa .
Akajibu tena wewe unabadili tu magari kwa habari ya zaka hutaki kutoa nikamwambia kwani zaka ni lazima lini sijatoa zaka zaidi ya mwezi huu nimepata msiba, na unanihusu kwa sehemu kubwa sina fedha na ninauguliwa wewe mwenyewe shahidi hali ya mzazi wangu Muda wote gari inapaswa kuwa na mafuta, muda wowote hali inabadilika tukawa tumeachana hivyo
Sasa hebu mnisaidie huu utaratibu unatoka wapi kwanini sadaka na zaka ni lazima au ni vile mtu anavyoguswa kulingana na Vile anavyopata! Maana Mungu anasema nijaribu sasa huku Naona mchungaji anatumia command utadhani kanipa yeye kisa anamadeni.
Hebu nipeni njia itakayoniondoa kanisa mikwaruzo na Mchungaji
Mungu yupo kwa sababu nature inatunoesha hivyoAchana na mambo ya dini ni mambo ya kitapeli. Mungu hayupo.
Eeh mkuu nimejaribu sana kumuelewesha ili afahamu hali ninayopitia kwa sasa
Hakuna mtu anatoa zaka hapa kama mwanaume hata tukienda bar zaka tunatoa mara ninunulie moja tunanunua nayo ni zaka piaWanaume mnaojielezea Sana mnakera
Endelea kutoa zaka acha kujilalamisha
Umeamua mwenyewe.
Huyo ni mdada sio mwanaume. Mchungaji hawezi kumpiga mkwara mshirika mwanaumeWanaume mnaojielezea Sana mnakera
Endelea kutoa zaka acha kujilalamisha
Umeamua mwenyewe.
Acha uzwazwa, kuna nyumba ya ibada isiyokuwa na matoleo ? Mbona mnatoa kwa waganga wa kienyeji wakati mnapunga majini ? MPE Bwana Yesu maisha yako.Mwanaume mzima unaenda kwenye makanisa ya kitapeli....hayo wanaenda wanawake tu, ndio wenye akili za kutapeliwa
Huyo Yesu uliwahi kumwona? Ama ni zile picha za Hollywood na sinema zao za kutumpubaza akili eti Yesu mweupe alitoa maisha yake kufa kwa wewe mweusi. Wewe unajuaje kuwa huyo Yesu unayemwabudu hakuwa mganga wa kiyenyeji.Acha uzwazwa, kuna nyumba ya ibada isiyokuwa na matoleo ? Mbona mnatoa kwa waganga wa kienyeji wakati mnapunga majini ? MPE Bwana Yesu maisha yako.
Basi kama ulijua ni hivyo ungepiga kimya kimya tu .Kuliko kuja kuandika humu.Mengine yanakuja kama dhoruba kupima imani yako ni wakati mzuri wa kuonesha misimamo
Mchicha haaahaaahaaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]itapendeza kama makanisa yakawa yanalipa kodi maana skuhzi zaka zinafosiwa
mfano mm nina kadi ya jengo kwenye kanisa letu na kila nikienda kanisani nachuma mchicha napeleka kama sadaka ukipigwa mnada wanaandika pale ila muinjilisti akaniita skumoja akaniambia utoaji wangu ni hafifu nkamuuliza mungunkanibariki mchicha kwahiyo nisimshukuru kwa bidhaa alio nibariki nayo akaniambia sawa mchicha mungu kakubariki nao ila unatakiwa utoe hela nyingi zaidi ya hyo ya mchicha nkamwambia nakuheshimu kwakua upo kwenye vazi la kanisa ila usije ukaniongelesha haya mambo ukiwa upo nje ya kanisa nkasepa .
hvi wanataka tutoe roho zetu ama maana wanaona tunachotoa kidogo sana wakat hawana kodi wala malipo wnaayofanya kutokana na wanachoingiza
Mchungaji ndio kambariki au Mungu ndio katoa baraka!!??KAma kakubariki umenunua kagari why usitoe 10%
Ni project tu za watu kuwajaza hofu watu wazembe na wajinga kujipatia kipato.Nielimisheni kifungu cha zaka la kanisa kinasemaje.
Nyie watu mmevurugwa sana na hili fundisho la Zaka... Eti Zaka inaweza kumlinda mama na ugonjwa... Kwa hiyo ni unanunua uponyaji kutoka kwa Mungu?Fungu la kumi ni ya kwanza kabisa, kabla hujapanga bajeti yako
Unaweza kuona ni shida ya mchungaji anataka hela lakini zaka ni ya Mungu na agizo
Lakini utoe kwa hiyari na si kwa kulazimishwa
Na usipotoa ni kosa kubwa.
Unaweza endelea uguza mpaka senti yako ya mwisho
Zaka inaweza kukulinda na ugonjwa wa mama na matatizo mengine.
Lakini pia kama unajua vizuri kuhusu sadaka, unatoa tu hata kama huendi kanisani
Kwani sh ngapi jamani inakuuma? Unatoaga sadaka kubwa sana?
Si unatuma tu hata elfu 2, buku, tano, kumi.
Kwa hiyo Mungu anahitaji hela yako(Zaka) ili akuponye!!!!Toa fungu la kumi litakulinda na magonjwa hata bi mkubwa anaweza kupona huo ugonjwa unaokula Hela , maana tunajua MUNGU akuleta magonjwa duniani magonjwa ni ya shetani , msikilize Mchungaji wako utanishukuru.