Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

Hao wachungaji wengi ni wapigaji, ebu chukulia watu kama Kina Gwajima wanacheza hadi porno, angalia mwingira anazaa hadi na wake za watu, angalia Lusekelo anapiga hadi NYAGI na kutukana majirani, Mwamposa anawauzia watu maji kwa bei ya juu yaani ulanguzi na wizi, sasa wachungaji matapeli kama hao ndio wataongea mambo ya maana?
Imeandikwa:

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa

Hos 4:6 SUV​

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
 
Bro inakera umepata kipesa chako kwa kuangaika unamrushia huko mkoani ili nae aone zile ada alizomlipia mjukuu wake zinarudi, yan hapo ndo unampigia ili umuulize kama umepata pesa ulomtumia anakunjibu asante yesu nimepata sadaka kesho niende safina. Ukisikia hvo unatamani kumwambia em nirejeshee pesa yangu sema ndo hivo ukishampa na umeeka nia kua ni sadaqa yako kwa mzazi uanabaki tu kimya uanjimind. Na hii asikuambie mtu imnifanya nipunguze kiasi cha kumtumia
Maumivu uliyonayo ndiko kukomboka kwako kifikra....

Pole sana ndugu yangu....

"U can't fool people all the times but for sometime"

Be blessed amen 🙏
 
Hii ni sawa na serikali ya Tanzania, umebarikiwa kila kitu gesi, dhahabu, madini, wanyama pori, mito na maziwa, lakini bado inakazania kukusanya pesa za wasio barikiwa - wananchi ambao hata elfu moja kwa siku kwao kuipata ni shida
Kwasababu hawataki kuwekeza katika uchumi na maisha ya watu. Kama maji yangewefanyiwa kipaumbele kila nyumba ingekua na maji na inalipa Bill ya mwezi, wangeweza kuongeza shilingi 4,000 kwa kila bill ya maji.
 
Hapa kwenye dini napo ni pa kuangalia Sana maana unaweza pigwa mchana kweupe kabisa hawana tofauti na wanasiasa hawa siku hizi.Siku hizi kusali ni gharama lazima ulipie.Mimi nikiwa sina sadaka siwezi kwenda kanisani maana huu utaratibu wa kuinuana bench kwa bench upite mbele ukatoe sadaka ni aibu kubakia kwenye bench kama mtu mzima aisee.Badala ya vikapu wameweka masanduku Ili ukiweka sarafu isikike uone aibu,yaani hii ni kulazimisha noti badala ya sarafu aisee.
 
Hawa viongozi wa dini kuliko kununua ma v8 na helicopter huku waumini wao wakikosa hata nauli ya kurejea makwao baada ya ibada kwann hizo pesa wasijenge vyuo vya ujuzi Ili waumini wao wapate ujuzi na elimu bure au kulipia kidogo ada kuliko wao kuwekeza kwenye vitu vya anasa.
 
Hujamuelewa, ni yeye awe tajiri na kwenda kwenye maduka makubwa ya kisasa, na kwenda Ulaya kama wewe unavyoenda Kariakoo. Ushauri wa bure! Mungu atakubariki unapompa masikini unaemfahamu tena jirani yako. Mpe kwa mkono wako mwenyewe, usimpe mchungaji ili akastarehe.
 
Back
Top Bottom