Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

Imeandikwa:

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa

Hos 4:6 SUV​

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
 
Maumivu uliyonayo ndiko kukomboka kwako kifikra....

Pole sana ndugu yangu....

"U can't fool people all the times but for sometime"

Be blessed amen 🙏
 
Hii ni sawa na serikali ya Tanzania, umebarikiwa kila kitu gesi, dhahabu, madini, wanyama pori, mito na maziwa, lakini bado inakazania kukusanya pesa za wasio barikiwa - wananchi ambao hata elfu moja kwa siku kwao kuipata ni shida
Kwasababu hawataki kuwekeza katika uchumi na maisha ya watu. Kama maji yangewefanyiwa kipaumbele kila nyumba ingekua na maji na inalipa Bill ya mwezi, wangeweza kuongeza shilingi 4,000 kwa kila bill ya maji.
 
Hapa kwenye dini napo ni pa kuangalia Sana maana unaweza pigwa mchana kweupe kabisa hawana tofauti na wanasiasa hawa siku hizi.Siku hizi kusali ni gharama lazima ulipie.Mimi nikiwa sina sadaka siwezi kwenda kanisani maana huu utaratibu wa kuinuana bench kwa bench upite mbele ukatoe sadaka ni aibu kubakia kwenye bench kama mtu mzima aisee.Badala ya vikapu wameweka masanduku Ili ukiweka sarafu isikike uone aibu,yaani hii ni kulazimisha noti badala ya sarafu aisee.
 
Hawa viongozi wa dini kuliko kununua ma v8 na helicopter huku waumini wao wakikosa hata nauli ya kurejea makwao baada ya ibada kwann hizo pesa wasijenge vyuo vya ujuzi Ili waumini wao wapate ujuzi na elimu bure au kulipia kidogo ada kuliko wao kuwekeza kwenye vitu vya anasa.
 
Hujamuelewa, ni yeye awe tajiri na kwenda kwenye maduka makubwa ya kisasa, na kwenda Ulaya kama wewe unavyoenda Kariakoo. Ushauri wa bure! Mungu atakubariki unapompa masikini unaemfahamu tena jirani yako. Mpe kwa mkono wako mwenyewe, usimpe mchungaji ili akastarehe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…