Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

Yuko sahihi kabisa kuchekelea sadaka kwa noti ya elfu 10 kwani hata Mungu amekua akiwatakabali wanaotoa sadaka nzuri madhabahuni pake , mfano wa kaini na Abel.

Katika kitabu cha Nehemia 8:10 tunaambiwa tule vilivyo vinono na kunywa vilivyo vitamu.

Mungu wetu hajawahi kuwa Mungu wa vinyonge hata siku moja na tena anasema katika neno lake tukapeleke zaka zilizo kamili ghalani mwake.

Mtumishi nakuusia ukapeleke vilivyo kamili kamili mbele ya Bwana.

Mungu alitoa sadaka, Yesu.

Abraham akatoa Isack.

Wewe ni nani usitoe.

Enyi uzao wa Nyoka acheni Ukaidi.
Mungu alitoa sadaka kwa nani?
 
Ila sadaka ni lazima jamani hata Bible inasema usiende au asionekane nyumbani mwa BWANA mikono mitupu, kuombea watu nao kazi wapendwa, Mchungaji anasimama saa 1-9 anaongea tu kweli? Sasa Mchungaji afungue genge sasa Mimi ulweso nikitaka kumuona niende pale gengeni?

Unajua maana ya sadaka? Yaani nitoe sadaka nimpe gwajima akanunue Hummer na helicopter? Nitoe sadaka nimpe lusekelo akanunua VX V8?
 
Hao wachungaji wengi ni wapigaji, ebu chukulia watu kama Kina Gwajima wanacheza hadi porno, angalia mwingira anazaa hadi na wake za watu, angalia Lusekelo anapiga hadi NYAGI na kutukana majirani, Mwamposa anawauzia watu maji kwa bei ya juu yaani ulanguzi na wizi, sasa wachungaji matapeli kama hao ndio wataongea mambo ya maana?
Mkuu umenena; hawa wanaosali ktk vioski vya hawa jamaa ndio wanaotakiwa 'kukutanishwa' na Ma-Dr bingwa wa mirembe au pale Muhimbili kwani inaonekana vichwa vyao havipo sawa!
 
Kama wao kweli ni watumishi wa Mungu...Mungu awape hizo hela siyo sisi...huu ni wizi kama wizi mwingine tu.

Mtu baada aombe Mungu ampe pesa ili afanye kazi yake,anachukua pesa yako halafu anakuombea kwa Mungu akupatie pesa maradufu,nonsense.
Usisahau mimi na wewe ndio part ya kanisa; kanisa siyo mali ya watumishi
 
jamani wazee wastaafu..ndio dili wanapewa mpaka uzee wa kainisa hapo....si unajua shetani akizeeka anakuwa malaika..wamewafilisi baba na mama yangu...dhuuuuu...kwa kuwa ni masuala ya imani unawaacha wapambane nayo wenyewe na hela ni zao..toa ubarikiwe..weeee...ubarikiwe nini zaidi mstaafu uongezewe pension au mifugo yenyewe unafuga passion usikae bure ila sio ki biashara...yaani akipata ibada mara tatu kwa wiki ni vichekesho tukienda kumtembelea maza siku tatu anashinda huko kanisani na cheo wamempa...full kumchuna
 
Yaani kuwasiliana na muumba ingekuwa ni ishu ya kumpigia simu au kuchat naye, maisha yangekuwa mazuri sana...

Ila hii ishu ya kupitia kwa mtu/watu (mitume n.k) ndio imekuwa kasheshe...

Enzi na enzi haijawahi tokea wanadamu wote wakawaelewa mitume/manabii you name them, iwe ni kwa habari ya sadaka au nyinginezo tu...

Hivyo Sky, toa sadaka ukijua wawajibika kama shukrani tu kwa Mungu, ukishaanza kuwaza habari ya upigaji, hakuna kanisa lisilotumia sadaka za waumini kinachotofautiana ni aina ya matumizi tu
 
jamani wazee wastaafu..ndio dili wanapewa mpaka uzee wa kainisa hapo....si unajua shetani akizeeka anakuwa malaika..wamewafilisi baba na mama yangu...dhuuuuu...kwa kuwa ni masuala ya imani unawaacha wapambane nayo wenyewe na hela ni zao..toa ubarikiwe..weeee...ubarikiwe nini zaidi mstaafu uongezewe pension au mifugo yenyewe unafuga passion usikae bure ila sio ki biashara...yaani akipata ibada mara tatu kwa wiki ni vichekesho tukienda kumtembelea maza siku tatu anashinda huko kanisani na cheo wamempa...full kumchuna
Inawezekana hujui,mafanikio uliyonayo wewe yanatokana na wazazi wako kutoa na kushinda nyumbani mwa Bwana kukuombea.

Nadhani utakuja kulijua hili baadae.
 
Back
Top Bottom