MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nawasalimu katika jina la Chama Cha Mapinduzi.
Naandika huu uzi nikiwa na hasira kali sana dhidi ya baadhi ya wachungaji, manabii, Motivational speakers na wengine wote wanaotoa mahubiri au semina mbalimbali. Hii ni kwa sababu ya wengi kuanza kudhalilisha watu kwa kisingizio cha ushauri. Mara nyingi Motivational speakers ndo huwa wanaleta kauli tata.
Jana nimetazama video ya mchungaji Rose Shaboka nikapatwa na hasira kali sana juu yake. Alikuwa akitoa ushauri kwa wanawake wadogo jinsi ya kuvaa na kujipamba. Kwa jinsi alivyokuwa akielezea utaona jinsi gani huyu mchungaji alivyokuwa akijikweza kwa kiburi kisichoelezeka. Alivuka mipaka yote ya ustaarabu kwa kuwatukana waalimu wa shule za msingi kwamba nywele zao huwa ziko rafu rafu. Huyu mchungaji alinirudisha hadi mwanzoni mwa miaka ya 90 nikamkumbuka mwalimu wangu wa darasa la kwanza na kujikuta nikipatwa na huzuni endapo angeangalia hiyo clip.
Ninamtaka huyu Rose Shaboka aombe msamaha waalimu wote. Kwa ushahidi tazama hiyo video.