Wachungaji na Maaskofu waiache CHADEMA ijipambanue kama chama cha siasa

Wachungaji na Maaskofu waiache CHADEMA ijipambanue kama chama cha siasa

Ujumbe muhimu/ Hitimisho: Upinzani ni muhimu sana kwa maendeleo ya Tanzania. CCM haiwezi jikosoa, bali inategemea upinzani uwakosoe ili wajitazame na kujisahihisha.

Upinzani unaotakiwa ni ule upinzani wa Tija, Upinzani ambao unatoa majibu ya changamoto za wananchi. Upinzani unaojitambua, si ule wa siasa za maji taka. CHADEMA ikiwa chama kikuu cha upinzani lazima kionyeshe njia. Chama husikiliza wananchi (makundi) wote, kero zao, shauku zao, manunguniko yao n.k.

Nasikitika kusema kuwa CHADEMA bado haijafika hapo. Ina safari ndefu! Na ndio maana wasipoungwa mkono katika hoja/wito/maandamano utasikia wakitoa matamko mbali mbali kama: watanzania waoga, hawajitambui, wamelogwa na chama tawala, si kama Gen-Z-Kenya n.k. Hapana watanzania wanajitambua sana, ila nyie kama chama mmeshindwa kuwafikia wananchi, na mmekuwa na haraka ya kushika madaraka kuliko kuwaelewesha watanzania mtafanya nini tofauti na hawa watawala wa sasa.

CHADEMA amkeni! Bado mna nafasi, jifungueni minyororo wafikieni wale mliowadharau/wasahau. Wachungaji na maaskofu tu hawatoshi kuwavusha. Nendeni na ule upande wa pili mkawasikilize hivi mmesigana wapi? Nendeni kwa machifu, nendeni vijijini, waelezeni wakulima hivi nyie mtafanya tofauti gani na haya wanayofanyiwa sasa hivi. Safari yenu imefanikiwa 30% tu, lianzisheni tena kumalizia 70% kwa maeneo hayo niliyoyataja. Nia ni kuwasaidia ili msimame imara. Alamsik!
 
Hangaika na chuo wenzako ni matajiri wanaenda Ulaya kuliko wewe unavyoenda kwa bibi ako, baba ako amewahi kukutana na balozi wa nchi gani?
Mangi utajiri na kwenda ULAYA ndio nini wewe msukule ? Muulize Lema aliekimbilia CANADA na tuko nae hapa tunatafuta ajira ,si angebakia huko majuu?🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Mangi utajiri na kwenda ULAYA ndio nini wewe msukule ? Muulize Lema aliekimbilia CANADA na tuko nae hapa tunatafuta ajira ,si angebakia huko majuu?🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
Lema juzi kamchangia Lisu ununuzi wa gari milioni 5, wewe ungeweza hata kutoa mia?
 
Lema juzi kamchangia Lisu ununuzi wa gari milioni 5, wewe ungeweza hata kutoa mia?
Unaijua historia ya Lema wewe ?leo ukimuuliza analipa kodi kiasi gani utashangaa mzee ,hakuna taarifa zake za ulipaji kodi ,maana yake jiulize hizo hela kazipata wapi ?
 
Kwa mwaka huu 2024 imekuwa vigumu kujua kama CHADEMA ni chama cha siasa chenye nia ya kuhudumia Watanzania wote au ni Taasisi ndani ya taasisi ya dini katika madhehebu tofauti.

Miaka ya nyuma kulikuwa na minong'ono tu kuwa hiki ni chama kinadhaminiwa na Mlengo wa Kikristo.

Maneno hayo nilikuwa nayapinga mara kwa mara lakini leo hii, nashawishika kabisa kuwa maneno hayo yalikuwa na ukweli. Kwasababu kila tamko la CHADEMA linabaraka 100% ya maaskaofu na wachungaji na kila tamko au barua za kichungaji zote zina baraka ya CHADEMA kwa asilimia 100, Kulikoni?

ChADEMA ijikague, vinginevyo itapata kundi moja tu na kamwe huwezi kushika nchi kwa kundi moja tu. Bado mna nafasi.

Pia soma: Siasa na dini
Mashehe waache CCM ijipambanie yenyewe.
 
Unaijua historia ya Lema wewe ?leo ukimuuliza analipa kodi kiasi gani utashangaa mzee ,hakuna taarifa zake za ulipaji kodi ,maana yake jiulize hizo hela kazipata wapi ?
Amewahi kuja kuomba kwa mumeo hela ya kula familia ake?
 
Back
Top Bottom