Wachungaji na Maaskofu waiache CHADEMA ijipambanue kama chama cha siasa

Wachungaji na Maaskofu waiache CHADEMA ijipambanue kama chama cha siasa

Umesahau waganga ,wachawi na machifu .

Walishasema Mungu hana maamuzi ya ushindi wa CCM kwa sababu hata akitaka au asipotaka CCM ushindi ni lazima .

CCM kimeonyesha dharau kubwa sana kwa Mungu na waumini wote wa dini ya Kiislamu na Kikristo wanaoamini kuwa mamlaka zote zinatoka kwa Mungu.

Nitashangaa Mkristo au Muislam anayeamini kuwa Kuna Mungu aliyeumba vitu vyote na mwenye uwezo wote wa kuamua jambo la
CCM ni zaidi ya shetani
 
Akina askofu Bagonza, Shayo, Mwamakula, etc. Tusishangae hawa makamanda wakichukua fomu kuwania ubunge kwa ticket ya chadema kwenye majimbo fulani.
Hapa pastor alikuwa anawania ubunge jimboni Ludewa.
images (49).jpeg
 
Kwa mwaka huu 2024 imekuwa vigumu kujua kama CHADEMA ni chama cha siasa chenye nia ya kuhudumia Watanzania wote au ni Taasisi ndani ya taasisi ya dini katika madhehebu tofauti.

Miaka ya nyuma kulikuwa na minong'ono tu kuwa hiki ni chama kinadhaminiwa na Mlengo wa Kikristo.

Maneno hayo nilikuwa nayapinga mara kwa mara lakini leo hii, nashawishika kabisa kuwa maneno hayo yalikuwa na ukweli. Kwasababu kila tamko la CHADEMA linabaraka 100% ya maaskaofu na wachungaji na kila tamko au barua za kichungaji zote zina baraka ya CHADEMA kwa asilimia 100, Kulikoni?

ChADEMA ijikague, vinginevyo itapata kundi moja tu na kamwe huwezi kushika nchi kwa kundi moja tu. Bado mna nafasi.

Pia soma: Siasa na dini
Siku ile mwamposa alivyowaambia waumini wake wakajiandikishe wampigie kura samia ulikaa kimya
 
Ni janga kubwa sana ,imagine hawakuwahi kuwa na mgombea uraisi muislam aisee🙆‍♂️🙆‍♂️


CCM wakristo wote wametoka na waislam wote wametoka wamebaki mafisadi .

Unapozungumzia Ukristo unazungumzia kiwango cha juu kabisa cha Uadilifu wa mwanadamu unaojenga ufalme wa Mungu Duniani na mbinguni .

Unapozungumzia Ukrsisto Unazungumzia umasihi ?

Kutaja ukristo katikati ya Taifa liliojaa wauaji na watekaji unakua umewasha Mwanga katikakati ya giza lililojaa matendo ya uovu na wao.Hivyo unakua unamulika wezi katika giza la uhalifu wao . Ukristo Hauwezi kupendwa kamwe ukisimama katika misingi yake ndio maana hata Yesu akarudi leo kimya kimya na kufungua kanisa atakosa waumini maana watataka aje akiwa na gari uzuri , suti kali akipendekeza kwa matajiri na watawala ,awe chawa wa Herode na Pilato na Makuhani,asifiwe watu wanaotoa sadaka nyingi, Ajenge mahoteli na majumba ya kifahari na yazinduliwe na wakubwa n.k. Hapo zitakubalika na kukimbilia na waumini wengi hasa wanawake na wanachama wahuni wa CCM .
Ukristo wa kweli unakemea wizi wa kura ,wizi wa fedha za umma ,wizi wa Mali za umma ,ufisadi,uonevu, rushwa , mauaji,utekaji wa watu wema , uongo,hukumu za dhulma kwa jaji kupigiwa simu na kutishwa , bunge kutunga sheria ambazo wao wenyewe hawawezi kuzifuata , kodi kubwa kwenye magari wakati ya kwao yanasamehewa kodi.
Ukristo unasimama katika Kanuni ya Dhahabu .
ukristo ni dhana ya uadilifu kwa kiwango cha juu kama Wana wa Mungu . Na waliopokea dini hiyo na kamwe hawaruhusiwi kutoka nje ya mafundisho hayo ya kujenga ufalme wa Mungu duniani.
Mohamad pia aliendeleza kuujenga ufalme wa Mungu kwa kusimamisha dini ya Haki na kukataa dhulma kwa kuwapinga na hata kuwakata mabichwa wale mabeduli waliokua wanadhulumu watu na kuikataa dini ya Mwenyezi Mungu kama CCM imivyomkataa Mungu kuwa hawezi kuwapangia anachopenda yeye bali apende asipende watashinda uchaguzi.

Pia CCM ilishakimbiwa na Waislam siku nyingi sana Tangu walipomuua Profesa Kushona Alipo Nalima aliyewahi kuwa waziri wa chapaa na waziri wa Elimu pia baada ya kuanzisha Chama cha NTRA na Waislam wote wakatoka CCM . Wakabaki waislam wauza unga na magaidi,watekaji na mafisadi tuu ndani ya CCM .
Walimuua Mzaramo wa watu wakiamini kuwa waislam wataogopa na kurudi CCM . Hata hivyo hawakurudi.

Baada ya Profesa Kushona Alipo Nalima kuuawa na CCM Chama chake cha NTRA Kilijifungua mtoto anayeitwa CECUF chini ya Propesa Efrahim Lumumba . Waislam wote wakahamia huko CECUF. CCM ikatumia mabilioni ya fedha kumghilibu Propesa Efrahim Lumumba na kufanya hujuma ya kuua CeCUF ili kuwarudisha waislam CCM lakini wapi . CECUF ikafa na kuacha mtoto mchanga anayeitwa ACTion Wazilindo. Mtoto huyo anakua kwa kasi sana japo anapata upinzani mkubwa sana kutokana na pesa chafu zinazomwagwa na waarabu wa Dudubaya kuhujumu upinzani Tanzania na kuua kabisa uzalendo wa Watanzania.
Kwa sasa CCM hakuna muislam hata mmoja aliyepo kwa nia kabisa ya kukiamini hicho chama kilichoanzishwa na Nyerere na baadae Azimio la Arusha.

Hata mama mwenye nyumba alikua mkosoaji mkubwa sana wakati ule wa CeCUF yenye nguvu ya mapanga Shaa . Wanaumeeeee, eeeeee😂😂😂😂
Wanawakeeeeee,eeeee
Mheshimiwa Lissu ingawaje nae mdomo hauna break hivyo hana sifa pia ya kiongozi


Tundu Lisu ni zaidi ya viongozi wote wa CCM waliopo.

Ukiwakusanya Viongozi wote wa CCM kwa pamoja ukawaweka kwenye mdahalo na Tundu unaohusiana na jambo lolote la kitaifa na kimataifa atawatoa jasho mpaka kwenye Meno.

Tundu Lisu ni Mwanasiasa wa kiwango kingene kabisa . Huwezi kumfananisha na machawa na wachumia tumbo waliopo popote . Hata Mbowe anamuogopa Tundu Lisu .

Kila Mtu anamuogopa Tundu Lisu . Lisu hana chembe ya ufisadi na dhulma yoyote na hapendi kuona mtu anadhumumiwa. Ukiona jambo amelikamia kimya ujue limemuudhi na amekuheshimu kukupa makavu.

Mtu mwingine aliyeonyesha uwezo mkubwa wa kuitetea na kuwasema wazi wazi waovu waliokalia ofisi za umma ni Mwabukusi.
Hawa wetu wawili ni chaguo la Mungu kwa ajili ya wanyonge wanaoonewa kwa muda mrefu na watawala wasiotaka kubadilika na kuwa watumishi wa umma kwa kusimamia haki za watu wote bila kubaguana kwa vyama na itikadi .
 
Siku ile mwamposa alivyowaambia waumini wake wakajiandikishe wampigie kura samia ulikaa kimya
Narudia, mimi si muumini wa "usichanganye dini na siasa". Maelezo haya huwa siyaelewi kabisa. Kulikuwa na mgombea ubunge "Padre" kule kipalapala- Tabora. Akipita makanisani na kuwaomba kura waumini wake. Kwangu hili ni sawa tu.

Ninachosema ni kuwa, CHADEMA isijifungie milango upande mmoja tu. Icheze na wote, taasisi zote. Ukweli nyie wote mnaujua kuwa kamwe CHADEMA au chama kingine chochote kile hakiwezi kushika hatamu kama kimeupata mgongo upande mwingine. Huu ndio ujumbe wangu utaowaokoa CHADEMA.
 
Umemaikia Mwamposa akiwa Bukoba????????
Nimemsikia na yupo sahihi, sioni tabu yeyote katika hilo. Hata hao wachungaji na maaskofu wanaohudhuria katika mikutano ya CHADEMA wasema hivyo.

Ninachosema CHADEMA isitie miguu yote katika chungu kimoja, ikutane na makundi yote.
 
Narudia, mimi si muumini wa "usichanganye dini na siasa". Maelezo haya huwa siyaelewi kabisa. Kulikuwa na mgombea ubunge "Padre" kule kipalapala- Tabora. Akipita makanisani na kuwaomba kura waumini wake. Kwangu hili ni sawa tu.

Ninachosema ni kuwa, CHADEMA isijifungie milango upande mmoja tu. Icheze na wote, taasisi zote. Ukweli nyie wote mnaujua kuwa kamwe CHADEMA au chama kingine chochote kile hakiwezi kushika hatamu kama kimeupata mgongo upande mwingine. Huu ndio ujumbe wangu utaowaokoa CHADEMA.
Chadema hawakuwahi kuwa na mgombea urais ambae sio mkristo aisee,hili waliangalie wa jicho la pili
 
Back
Top Bottom