Wachungaji na Maaskofu waiache CHADEMA ijipambanue kama chama cha siasa

Wachungaji na Maaskofu waiache CHADEMA ijipambanue kama chama cha siasa

Ni makosa makubwa kukiunganisha chama cha siasa na ukristo kwa hiyo unataka kutuambia CCm inaungwa mkono na waislam? Kitu ambacho si kweli hebu toeni sera zinazokubalika na wananchi na watu wakilizika na sera zenu mtachaguliwa tu, maana ndani ya chadema kuna wakristo na waislam na wasio na dini hivyo hivyo ndani CCm kuna wakristo na waislam na wasio na dini hivyo si vyema kuanza kuunganisha ukristo na chadema

Ma
 
Aliyekutuma kwenye hili ni nani?

Huyaoni ya chama tawala mmeona
chadema tu? Kuwa na kiasi kha!

Huwa mnalipwa kiasi gani mpaka mjitoe ufahamu?

Punguzeni kujipendekeza ni full udwazi
Nimeandika uzi huu kwa nia ya kuisaidia CHADEMA kwa vipi kitaendelea kuwa chama kikuu cha upinzani na hata kushika hatamu.
Nimeshangazwa na wengi kutokwa na povu na pengine kutouelewa ujumbe mkuu katika huu uzi.
 
Mashekhe , Maimamu, Baraza la Ulamaa, BAKWATA na SHURA YA MAIMAMU wafanye vivo hivyo kwa CCM na SAA 💯
Nianze kwa kusema kuwa mimi si muumini wa "usichanganye dini na siasa". Mantiki ya uzi huu ndio ilikuwa hilo uliloliandika ndugu Nandagala one. Mstari wa mwisho nimeandika- nukuu "ChADEMA ijikague, vinginevyo itapata kundi moja tu na kamwe huwezi kushika nchi kwa kundi moja tu"

Tegemeo langu lilkuwa kuwaona CHADEMA wananyoosha mikono kwa dini nyingine ili kutafuta kuungwa mkono kama maaskofu na wachungaji wanavyokiunga mkono. Ukinielewa kwenye hili tunaweza kwenda vizuri pamoja. Nia ni kuisaidia CHADEMA, fahamu bila upinzani CCM inalala.
 
Mkuu, mtu sahihi wa kukujibu hoja yako ni Mh. Msajili wa Vyama.
Hapana si msajili bali ni wananchi. Ndugu zangu, Msajili anaweza akafumba macho lakini si wananchi. Waogopeni sana wananchi kama wenyewe msemavyo- Peoples........Power.
 
Hapana si msajili bali ni wananchi. Ndugu zangu, Msajili anaweza akafumba macho lakini si wananchi. Waogopeni sana wananchi kama wenyewe msemavyo- Peoples........Power.
Peoples Power mbona wameshindwa kumpata mwenyekiti mmbada wa huyu mzee? Hivi kweli CDM ni chama cha kuongozwa na wazee mithili ya TLP au UDP?
 
..unakumbuka lile BOMU lililorushwa ktk mkutano wa Chadema Arusha ktk utawala wa Kikwete?

..juzi ktk kongamano la utekaji Afande Jumanne Muliro alisema lilikuwa ni shambulizi la MAGAIDI walioamini Chadema ni chama cha Wakristo.

..Hizi kampeni za UDINI dhidi ya vyama vya upinzani zina madhara mabaya kwa jamii yetu.

..CCM inaweza kushinda uchaguzi bila kufanya kampeni chafu na za kibaguzi kama hiki unachofanya.
Siungi mkono ugaidi wa aina yeyote ile, bali wananchi wana haki 100% kukinyooshea mkono chama chochote kile kinachobagua makundi fulani ya jamii.
 
Ukiona watu wa Dini wanakikubali chama cha siasa jua hicho ni chama cha Haki
Kama ni watu wa dini moja tu ndio wanakikubali, hapo kuna walakini. Tafakari mwenyewe, utapata jibu tu kwani ninakuamini sana katika chambuzi zako. Zingatia kuwa kwenye box unahitaji kura za wote ili ushinde Urais.
 
Nianze kwa kusema kuwa mimi si muumini wa "usichanganye dini na siasa". Mantiki ya uzi huu ndio ilikuwa hilo uliloliandika ndugu Nandagala one. Mstari wa mwisho nimeandika- nukuu "ChADEMA ijikague, vinginevyo itapata kundi moja tu na kamwe huwezi kushika nchi kwa kundi moja tu"

Tegemeo langu lilkuwa kuwaona CHADEMA wananyoosha mikono kwa dini nyingine ili kutafuta kuungwa mkono kama maaskofu na wachungaji wanavyokiunga mkono. Ukinielewa kwenye hili tunaweza kwenda vizuri pamoja. Nia ni kuisaidia CHADEMA, fahamu bila upinzani CCM inalala.
Nimekusoma kiongozi
 
Noa

Naona reactions za wanajukwaa zinaelezea ambayo hukutarajia. Ulitarajia wadau waiponde Chadema, sasa imekuwa tofauti. Pole sana.
Hapana, nilitarajia reactions kama hizi ila sikutaka kumalizia uzi kwa maneno kama hayo au nasubiri wenye Povu.....

Kimsingi ukikisahihisha chama hiki, subiri upigwe mawe. Kama huwezi kusubiri hayo, basi kila kukicha kisifu chama hiki. Mkifanya mazuri nitawasifia, lakini kwa hili hapana! Nia yangu ni kuwasaidia, Nendeni mkazungumze na ule upande wa pili. Mwanasiasa ni muhumi kuwa msikivu.
 
Hiwezi kutenganisha siasa na dini kk, vyote vinatemeana
Swadakta! Nakubaliana nawe, ila kama mwanasiasa usielemee upande mmoja. Jifunzeni kwa Gwajima alipokuwa anagombea ubunge, alirefusha mkono wake pande zote.
 
Back
Top Bottom