Mkuu, kwa hali kilivyo kwa sasa Chadema ni chama kinacho kubalika haswa. Kama uchaguzi ukiwa huru na haki kinashinda kabla ya saa 6.00 mchana.
Ni kweli ila kwa Hali ya Jamii ya Tanzania Chadema ikiungana na ACT Wazalendo ndio upinzani itaingia Ikulu zote za Tanganyika na Zanzibar vinginevyo hakuna chama kitakachoitoa CCM madarakani kwa karne hii. Japo patakuwa na mabadiliko sana ya kiutawala lakini ndani ya CCM. tutatawaliwa mpaka na madereva achilia mbali Makonda .
Mpaka Sasa ACT inatajwa kuwa ni chama chenye harufu ya kidini kama ilivyo chadema .
Sasa kama ACT ina mtaji mkubwa Zanziba, Kundi,Kigoma, Baadhi ya kata kwenye mikoa ya pwani basi hakuna namna ya kuacha kushirikiana nao ili CCM isipate mwanya wa kushinda hasa kwenye ubunge na udiwani na serikali za mitaa .
Cha msingi tu ni kuwapata wagombea wanaomuogopa na kujua kuwa kuna siku Mungu atahukumu wetu wote bila kujali cheo .
Kwa sababu tukiweza tu ikulu na kusahau nature ya watanzania kiimani basi ni wazi kabisa kuwa shetani kupitia CCM atakua ameshinda na Mungu atadhalilishwa sana Tanzania . Na ule usemi wao wa ushindi wa CCM sio Mungu anayeweza kuuzuia wala kuupanga bali ni lazima utatumia .
Kwa hiyo kwa sasa kazi iliyopo mbele yetu ni kuhakikisha kuwa SHETANI HASHINDI NA KUITAWALA TANZANIA KUPITIA Mgongo wa CCM . Kwa sababu ushindi wa CCM ni ushindi wa shetani na anavyopata ni damu za watu kuongezeka kumwagwa kama shukrani na malipo yake.
Sasa wapinzani wakuu ACT kule Zanzibar na Chadema Bara wasipoungana ni wazi kuwa Tutakuwa tumemkabidhi shetani nchi rasmi .Hivyo tujiandae tu kuona uovu wa kila aina ukifanywa ikiwemo ulawiti,ushoga ,bidhaa feki na zenye sumu, usagaji, magendo ,madawa , uonevu , mauaji ,migogoro mikubwa ya ardhi,kutorosha kwa wanyama na madini n.k .
kushirikiana na ACT ni jambo la Busara sana na litaleta baraka kwenye nchi na litabalance siasa na kuleta amani kati ya dini zote za Haki na wapenda haki dunia nzima .