Kijakazi Chizi
Member
- Dec 9, 2025
- 89
- 213
Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste mkoani Arusha, jana Desemba 13, 2025 ulifanya kikao cha dharura katika Kanisa la ARCC Sakina, kujadili madai ya Vitendo vya Unyanyasaji vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya Vijana wa jamii ya Kimaasai, dhidi ya Wachungaji wa Makanisa ya Kipentekoste, Wake zao na Watoto wao wa Kiume.
Katika kikao hicho, Wachungaji walidai kuwa wanakumbwa na mashambulizi, dhihaka na fedheha kwa kile walichosema ni kukataa kushiriki baadhi ya mila na tamaduni za Kimaasai, hususan tohara. Wamesema mila hizo zinakinzana na imani na mafundisho ya Kikristo wanayoyaamini.
Aidha, wachungaji hao wameeleza kuwa nyimbo zinazoimbwa wakati wa sherehe za tohara zinadaiwa kuwa na matusi pamoja na maudhui yasiyo ya kimaadili, hali wanayodai inaongeza chuki na uhasama dhidi yao.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwezeshaji Mkuu, Askofu Dkt. Shadrack King’ori, amesema changamoto hiyo imekuwa tishio kwa usalama, heshima na uhuru wa kuabudu wa watumishi wa Mungu katika maeneo yanayotekeleza mila hizo.
Ameeleza kuwa Wachungaji wengi wamekuwa wakipitia vitisho, udhalilishaji na hata vipigo kutokana na shinikizo la kutaka wao na Watoto wao kushiriki mila wanazoziona kuwa zinahusisha ibada ya mizimu.
Kwa upande wake, Kiongozi wa jamii ya Kimaasai nchini, Laigwanan Isack Ole Kisongo, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema kuwa maandalizi yanaendelea ya kuitisha kikao maalum kitakachofanyika tarehe 23 Januari 2026.
Ameeleza kuwa kikao hicho kinatarajiwa kuwakutanisha viongozi wa makanisa pamoja na viongozi wa jamii ya Kimaasai kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu na kuimarisha mshikamano wa kijamii.