Wadada, niulizeni kitu chochote kuhusiana na huduma za salon, hair & nails

Wadada, niulizeni kitu chochote kuhusiana na huduma za salon, hair & nails

Nywele yangu ni laini na ndefu (6 yrs)
Ilivyofikisha miaka 3 nikuweka beautiful beginning ya box ile ya watoto (kwa ushawishi).... Lakini haikunipa matokeo mazuri, labda kwasababu ilikua ni mwanzo. Nilitumia ikaisha

Kwa ushaur wa salon nikabadili dawa nikawa naweka miadi pamoja na steaming ya movit.... Ikakubali balaa.... naretach kila baada ya miezi 3

Sasa nikapewa zawadi ya mega growth kuanzia dawa,steaming mafuta etc (ya box) hiyo steaming ni leave-in, nimeweka mara 2 na mpaka sasa natumia steaming yake na ile ya movit (zinapokezana)

Naomba ushauri, nitumie steaming gani ili nywele ijae zaidi?

NB:
Nasuka rasta , nabana , naziachia na kusukwa za mkono sometimes

Sijawah kuwa na tatizo la mba wala kuungua na dawa tangu nianze kuweka

Hii ndiyo hiyo treatment
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    591.6 KB · Views: 939
Niliwahi kutumia beautiful beggining lakini nywele zikaanza kupukutika ndo nikaingia kwenye profective. Ilikua nzuri lakini nahisi kwa sasa naona imeanza kuchoka

Kwa kawaida unatumia stemming gani na unapaka mafuta gani?

ushauri wangu kwako...endelea kutumia hiyo dawa ya Profectiv ila tumia steaming ya motion na utumie mafuta ya T444Z kujipaka kwenye nywele zako kutoka chini ya ngozi hadi juu ya unywele.

image.jpg
 
Sorry for my late reply...kwanza hongera kwa kuwa na nywele zenye afya na zisizo na matatizo. Ila ningekushauri utulie au utumie hair treatment ya aina moja...kuchanganya changanya ni kuzitafutia matatizo nywele zako.

Tumia steaming hiyo hapo chini kwa mwezi mara mbili ( ni yakuingia kwenye steamer)...ni mzuri sana.


Asante kwa ushaur

Ndo ipi hiyo?
 
Hii ndiyo hiyo treatment


Ok nimekupata, ila sioni vizuri nipo through mobile

Unaweza nipatia jina kwa maandishi na bei tafadhali

Nipo mkoani na sio Dar

Swali: Ile ya movit na mega niachane navyo kabisa?
 
Nywele zangu no laini sana nahisi kuliko za binadamu wrote kila aliye ziona na kuzishika anashangaa na hazina DAWA ila ukizigusa ziko ka zinadawa nimechoka kusuka au kuwa na natural hair nataka niweke DAWA he ni DAWA gani nzuri naeza weka na steaming kwa nywele hizo
 
View attachment 123948 View attachment 123950View attachment 123951

Wapendwa ndugu zanguni wa MMU hasa wadada...kama kunakitu au vitu vilikuwa ninakutatiza kuhusiana na swala zima
la urembo wa salon' basi chukua nafasi hii kuniuliza swali lolote lile linalohusiana na huduma za salon.

Hair Reluxer
Hair treatment
Hair special treatment
Misuko
Hair designing &
Beauty clinic (full package)

Je,unatatizo lolote la nywele zako za asili? Au unatatizo lolote la kucha zako za asili?

Yaliyo ndani ya uwezo wangu nitayajibu na yale ambayo yatakuwa nje ya uwezo wangu basi nitayaacha.


"UZURI UNAZALIWANAO ILA UREMBO NA USAFI WA MWILI UNAJIPA MWENYEWE"
unyao wangu ni mgumu sana mpaka una dead skin je ni pedicure gani inanifaa
 
Mimi nina dreads ila nywele zangu ni chache nifanyaje zijae. Hali hii inafanya dreads zangu ziwe nyembamba.
 
Sitofautiani sana na MimiP..

Nina dread, ila nywele zangu ni chache sana na kavu.

Nipake nini zijae na nitumie mfuta gani mazuri? asante
 
Last edited by a moderator:
Kama kunamtu anahitaji wallpaper kwa ukuta wa saloon nyumba yake tafadhari tiwasiliane au nifollow insta wallpaper home decore
 
Mimi mda wote naeka ultra sheen, ilinikubali sana, lakin nilivyopata mimba na kunyonyesha nywele zimekua mbaaaaayaaaaa, sizipendi hata kidogo, nataka nibadili dawa, mega growth nadhan. nywele zangu ni nzito,nyingi, c laini wala c ngumu.
 
kwa saloon au binafsi anaye hitaji bidhaa za Nice & Lovely hata kwa piece moja ani julishe au Ana saloon na anataka mtaalamu wa nywere wa bidhaa za nice and lovely aje saloon kwako kufundisha namna ya kuzitumia anijulishe pia.

Alfred Kohi
0764800989
 
Nywele zangu no laini sana nahisi kuliko za binadamu wrote kila aliye ziona na kuzishika anashangaa na hazina DAWA ila ukizigusa ziko ka zinadawa nimechoka kusuka au kuwa na natural hair nataka niweke DAWA he ni DAWA gani nzuri naeza weka na steaming kwa nywele hizo

Ningeziona na kuzigusa hapo ningetoa ushauri sahii. Tafuta professional salon yeyote uende ukaonane na wataalamu.
 
Mimi nashida na dawa ya kuondoa makovu usoni ngozi yangu ni ya mafuta

Kama unahisi kuwa hilo tatizo lako ni kubwa sana basi nenda kwanza hospital...ila kama unaliona ni dogo basi tafuta any professional beauty clinic salon na ukafanyiwe skin care treatment ya facial
 
kwa saloon au binafsi anaye hitaji bidhaa za Nice & Lovely hata kwa piece moja ani julishe au Ana saloon na anataka mtaalamu wa nywere wa bidhaa za nice and lovely aje saloon kwako kufundisha namna ya kuzitumia anijulishe pia.

Alfred Kohi
0764800989
Noted mkuu
 
Back
Top Bottom