Samahani nakuuliza maswali mengi kwani nimechoka kuweka relaxer . Umegusia kuzitreat nywele kidogo je nazitreat na nini tafadhali nijibu kileiman nataka kuelewa ili nifanye mwenyewe. Nakumbuka ilikua june nilienda salun flani hapa napoishi nikataka curl lkn mtaalamu akaniambia haiwezekani kwani nywele hata kama zimeota haimaanishi kama hazina dawa nikachanganyikiwa manake nilikua nimekaa 6 months na nywele zilikua kipili pili kabisaa, majibu sikuridhika nayo ikabidi niwekeke tena relaxer kitu ambacho ssikukipenda kabisaa. Leo nimeshukuru kukuta hapa kuna mtaalamu so please nsaidie mwenzio kwani ujuzi unatofautianakwani huyo mdada sikuridhishwa hata na utendaji wake wa kazi. Swali jengine je apart from kuweka curl kuna option nyingine ya kufanya . Yaani nywele natural naweza weka dawa gani isiyo na madhara makubwa na ambayo naweza kuweka mwenyewe bila kwenda salun.