Wadada, niulizeni kitu chochote kuhusiana na huduma za salon, hair & nails

Wadada, niulizeni kitu chochote kuhusiana na huduma za salon, hair & nails

nikisuka kichwa kinauma sana upande wa kulia ni tatizo gani hilo? au ni msusi?
 
Hapana hutaitaji kusubiri tena...natural hair ikishajitokeza basi unazitream kidogo tu kisha unaanza kuweka permanent curl yako

Mimi pia nataka kuweka curl nimenyoa lengo langu nikuzie nywere zangu je nikiweka curl badae naweza rudi kwenye relax

Asili ya nywere yangu ni ngumu, nyingi na nzito
 
mimi nina nywele fupi kidogo ila ukishika zinasukika, naweka sana wave. nilikuwa natumia sofnfree sasa natumia MOvit, lakini hazichelewi kuota. nataka pia zijiviringishe zikiwa kubwa hivyo hivyo km ile picha uliyoattach katika comment yako ya saa 22:42 usiku. napaka mafuta ya sofnfree gel activator.
 
pole sana mpenzi wangu...wewe yakupasa uanze hair clinic ya Special treatment kwa miezi mitatu(3) I mean ndani ya kila mwezi mmoja utaifanya mara mbili. So jumla utaifanya mara 6 ndani ya miezi 3

mnayo hii huduma pale?? ni how much?
 
Haya jamani…hatimaye nimerudi ndani ya nyumba.

Niko busy sana ofisini lakini musijari pale ambapo nitapata chansi basi tutaenda sawa
 
nifanye steaming ya nini?
nitumie spray ipi nzuri?
NAKUAMINIA UJUE!
Tumia steaming ya aina yoyote ile ilimradi iwe ya kuingia kwenye steamer na wakuache kama dk 20 hivi ndipo wakuoshe.
Ila ningependekeza utumie steaming ya Tea Trea Naturals…inapatikana kwa SH Amon pale mtaa wa samora
 
nikisuka kichwa kinauma sana upande wa kulia ni tatizo gani hilo? au ni msusi?
Oooh pole sana mpenzi…mara nyingi unapendelea kusuka nini na unatumia matirial gani? na je umewahi kuwa na matatizo ya kuumwa na kichwa tangia enzi za utoto wako?
 
Mimi pia nataka kuweka curl nimenyoa lengo langu nikuzie nywere zangu je nikiweka curl badae naweza rudi kwenye relax

Asili ya nywere yangu ni ngumu, nyingi na nzito
Kwanza kwanini ulikata nywele? Zilikuwa zinatatizo lolote au uliamua kuzikata tu?
 
Nifanye nini ili kucha zangu za asili sizikatike ziwe ngumu?maana sipendi kucha bandia
 
mimi nina nywele fupi kidogo ila ukishika zinasukika, naweka sana wave. nilikuwa natumia sofnfree sasa natumia MOvit, lakini hazichelewi kuota. nataka pia zijiviringishe zikiwa kubwa hivyo hivyo km ile picha uliyoattach katika comment yako ya saa 22:42 usiku. napaka mafuta ya sofnfree gel activator.
Sawa mpenzi…ile picha uliyoiona inaitwa straws hair style…wanatumia hii mirija ya kawaida tu na wanachanganya na mafuta fulani ndiyo inatokea vila, lakini inapendeza zaidi nywele yako ikiwa na dawa (ume retouch)
 
Oooh pole sana mpenzi…mara nyingi unapendelea kusuka nini na unatumia matirial gani? na je umewahi kuwa na matatizo ya kuumwa na kichwa tangia enzi za utoto wako?

Mara nyingi natumia rasta za kawaida tu na pia kusuka nywelw zangu ..... sijawahi kuwa na tatizo la kichwa ... ila nikisuka tu iyo wiki ni mateso kwangu . Na ninapendwza wewe acha tu
 
View attachment 123948 View attachment 123950View attachment 123951

Wapendwa ndugu zanguni wa MMU hasa wadada...kama kunakitu au vitu vilikuwa ninakutatiza kuhusiana na swala zima
la urembo wa salon' basi chukua nafasi hii kuniuliza swali lolote lile linalohusiana na huduma za salon.

Hair Reluxer
Hair treatment
Hair special treatment
Misuko
Hair designing &
Beauty clinic (full package)

Je,unatatizo lolote la nywele zako za asili? Au unatatizo lolote la kucha zako za asili?

Yaliyo ndani ya uwezo wangu nitayajibu na yale ambayo yatakuwa nje ya uwezo wangu basi nitayaacha.

"UZURI UNAZALIWANAO ILA UREMBO NA USAFI WA MWILI UNAJIPA MWENYEWE"

mi naomba unisaidie..nitumie nin ili nywele zijae kwasababu napenda nywele nyingi na sina kiivo....pili kwanin nywele zinaweza kukua kwa kasi afu ikafika mda zinasimama..nini solution ya kupungua kukua au kuna vitu nakosea...tatu nywele zangu zinadawa lakini ni nyeusii lakin siku zinavoenda weusi unapungua...nifanye nin kuprotect hair colour..
 
Nifanye nini ili kucha zangu za asili sizikatike ziwe ngumu?maana sipendi kucha bandia
Kwanza umewahi kubandika kucha before? hilo tatizo la kukatika katika limeanzia udogoni au ukubwani?

Hebu funguka kwanza then tutaendelea
 
Unapatikana wapi? I mean hiyo beauty clinic yako iko wapi?
Do you take students?
Mimi napatikana hapa JF kama hivi unavyoona,ila kama utahitaji beauty clinic mzuri basi nitakuelekeza kwani ziko nyingi sana ndani ya Dar kuanzia Mikocheni,Mbezi,Masaki, Msasani na Posta area.

Huyo mwanafunzi wako anataka kujifunza nini?
 
Mie natumia beautiful begining box,au Argan oil products mafuta ya nywele napaka olive oil na parnevu oil laki nywele zangu nikavu nikipaka mafuta siku 2 tu nywele ishapauka ka sijapaka mafuta nina ngozi kavu kwa kifupi nitumie mafuta gani nywele yangu ishine
 
Back
Top Bottom