Wadada wa Dar na Visigino vyao

Joannah

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2020
Posts
20,921
Reaction score
49,014
Mambo zenu jamani.

Nimeona tukumbushane tu madiva wa Dslam kuhusu Visigino vyetu jamani. Sio Siri Dar panaongoza wadada kuwa na miguu michafu yaani hadi unashangaa huyu katoka kwenye vanga wapi? hii yote ni sababu ya kusingizia joto na kuendekeza hivi visendo vya kichina .Yaani mtu muda wote hana usafi, unakutana na dada mzuri kavaa nguo yake nzuri ukimuangalia chini anakukata stimu kabisa.

Jamani hebu tusugueni hivyo visigino, yaani mtu kisigino hakieleweki, cheusi utasema alikuwa anasigina masizi๐Ÿ™„. Huyu mchina asitudanganye na slipper zake, na vile sasa katoa hizo kopi za Tommy Hilfiger basi yamefika wa wadada wa Dar es salaam, hebu tuwe tunavaa na viatu siku moja moja tutunze miguu hiyo. Hivi mbona Mbeya na Arusha wasafi tu wenzetu.

Unaajita Diva na kisigino kichafu wapi na wapi! Tubadilike.
 
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ imebidi nijiangalie kabla sijacomment,

Mimi binafsi viatu navaa nikiwa naenda interview ๐Ÿ˜€, kanisani au shereheni kidogo na date huko kwingine woooi ni visendo tu ๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜ƒ ila miguu yangu misafi naitreat inavyopaswa
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Yaani Bora wewe unaitunza, majority tunavaa hivyo visendo wengi wavivu kusugua miguu. Yaani kungekuwa na yale mazoea ya kusugua tu miguu wenyewe Kabla ya kwenda saloon miguu ungekuwa poa.
 
Japo kapicha au kavideo ka sugua gaga basi
 
Kwa kweli umezungumza. Unakuta mtu anajichubua kisigino cheusi yani mguu mchafu. .

Kuna uzi juzi nilisema huwa naangalia miguu kumpa mwanamke marks watu wakabeza. .

Bora mmelijua mapema big turn off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ