Wadada wa Dar na Visigino vyao

Wadada wa Dar na Visigino vyao

Mambo zenu jamani.

Nimeona tukumbushane tu madiva wa Dslam kuhusu Visigino vyetu jamani.Sio Siri Dar panaongoza wadada kuwa na miguu michafu yaani Hadi unashangaa huyu katoka kwenye vanga wapi?hii yote Ni Sababu ya kusingizia joto na kuendekeza hivi visendo vya kichina .Yaani mtu muda wote hana usafi,unakutana na dada mzuri kavaa nguo yake nzuri ukimuangalia chini anakukata stimu kabisa
Jamani hebu tusugueni hivyo Visigino yaani mtu kisigino hakieleweki,cheusi utasema alikuwa anasigina masizi🙄!Huyu mchina asitudanganye na slipper zake,na vile Sasa katoa hizo kopi za Tommy Hilfiger Basi yamefika wa wadada wa Dar es salaam,hebu tuwe tunavaa na viatu siku moja moja tutunze miguu hiyo.Hivi mbona Mbeya na Arusha wasafi tu wenzetu.

Unaajita Diva na kisigino kichafu wapi na wapi!Tubadilike
Picha za viazi choma zikwapi
 
images (1).jpeg
 
Eeeeh hao Tena wapya sijakutana nao
Kuna sehemu nilienda kuangalia mgonjwa. Kulikuwa na sitting room za kiarabu (za kukaa chini, kuegemea mito). Aliingia binti mmoja mrembo hasa. Ila alipokuja kukaa na kunyoosha miguu ule uvundo uliotoka hapo ni Mungu tu ndio anajua. Haikujalisha kulikuwa na a/c na harufu ya oud.

Huyo ni mfano tu mmoja lakini wape kina dada wengi hasa wanaoshinda na viatu vya kufunika siku nzima huwa wananuka miguu mno.
 
Back
Top Bottom