Wadada wa Dar na Visigino vyao

Wadada wa Dar na Visigino vyao

Sio Siri Dar panaongoza wadada kuwa na miguu michafu yaani hadi unashangaa huyu katoka kwenye vanga wapi? hii yote ni sababu ya kusingizia joto na kuendekeza hivi visendo vya kichina .Yaani mtu muda wote hana usafi, unakutana na dada mzuri kavaa nguo yake nzuri ukimuangalia chini anakukata stimu kabisa.
Hujasikia matangazo na malalamiko kwenye vyombo vya habari Dawasa wanatoa maji mara 2 kwa wiki?
 
Wadada jitahidini zamani wenzenu wamama walikuwa na jiwe la kusugulia visigino siku hizi wanaotoa huduma za pedicure wamejaa tele. Mwanamke akiwa na miguu misafi isiyo na gaga wala sugu anavutia sana
 
Hili liwekewe msisitizo kwa wadada wanaojichubua, hawa raia huwa wana miguu inatisha sana kwenye visigino na ankle zao. Unamuangalia mpaka unapata kinyaa.

Wengine wanaenda mbali zaidi wanakuwa na magaga ( visigino vimepasuka), size ambayo hata shillingi inajificha.

Unawaza kama usafi katika sehemu inayoonekana na watu mara kwa mara umeshindikana, vipi huko ndani ambako hapaonekani?

Kero nyinyine ni mawigi, aiseeeeh mengi huwa yananuka vibaya sana. Wale wanaojua kutunza nywele zao zinakuaa na kaungevu fulani na zinanukia, mbarikiwe huko.


Mleta mada asante anaa, naamini watabadilika.
Asante kwa kuchangia kero yako naamini wengi watapata madini hapa
 
Back
Top Bottom