Wadada wa Dar na Visigino vyao

Wadada wa Dar na Visigino vyao

Hili liwekewe msisitizo kwa wadada wanaojichubua, hawa raia huwa wana miguu inatisha sana kwenye visigino na ankle zao. Unamuangalia mpaka unapata kinyaa.

Wengine wanaenda mbali zaidi wanakuwa na magaga ( visigino vimepasuka), size ambayo hata shillingi inajificha.

Unawaza kama usafi katika sehemu inayoonekana na watu mara kwa mara umeshindikana, vipi huko ndani ambako hapaonekani?

Kero nyinyine ni mawigi, aiseeeeh mengi huwa yananuka vibaya sana. Wale wanaojua kutunza nywele zao zinakuaa na kaungevu fulani na zinanukia, mbarikiwe huko.


Mleta mada asante anaa, naamini watabadilika.
Dada angu
Tajiri wangu
Naomba tuendelee kunyoa Carleen
 
Sitaki nionekane namsifia sana dada'ko Carleen , ila katika hayo niliyotaja hapo juu namkubali sana.

Wewe pia nakukubali hivyohivyo, as long as umesema unanyoa😄.
Yan huyo dada etu yuko 👌👌

Me nanyoa 😂😂
Labda waje waweke sheria ya kutufukuza masaluni ya kiume ndio tutaanza waza vingine.
 
Mdogo wangu tajiri...
Nina viporo hapa napambana navyo kama vyoote, naja soon kukulipa madeni yako yooote wewe na my wako..!!🤩
Em pambana chap chap kwanza ndio dec tusije kosa hela za kwenda kulisha Twiga Same 😂😂❤️
 
Mambo zenu jamani.

Nimeona tukumbushane tu madiva wa Dslam kuhusu Visigino vyetu jamani. Sio Siri Dar panaongoza wadada kuwa na miguu michafu yaani hadi unashangaa huyu katoka kwenye vanga wapi? hii yote ni sababu ya kusingizia joto na kuendekeza hivi visendo vya kichina .Yaani mtu muda wote hana usafi, unakutana na dada mzuri kavaa nguo yake nzuri ukimuangalia chini anakukata stimu kabisa.

Jamani hebu tusugueni hivyo visigino, yaani mtu kisigino hakieleweki, cheusi utasema alikuwa anasigina masizi[emoji849]. Huyu mchina asitudanganye na slipper zake, na vile sasa katoa hizo kopi za Tommy Hilfiger basi yamefika wa wadada wa Dar es salaam, hebu tuwe tunavaa na viatu siku moja moja tutunze miguu hiyo. Hivi mbona Mbeya na Arusha wasafi tu wenzetu.

Unaajita Diva na kisigino kichafu wapi na wapi! Tubadilike.
Hauna hata ka picha kakusindikizia huu uzi mkuu?
 
Si

Sisi tulifundishwa kunawa miguu nje kwa kuisugua sawasawa na kuosha ndala zetu za umoja enzi hizo kama sio bata ndo uende kuoga, naona itaratibu huu ni mzuri huezi kuta miguu iko hovyo,
Kwa kweli miguu ikisuguliwa kila unapoingia kuoga miguu itakuwa na Hali nzuri sana
 
Back
Top Bottom