Wadada wa saluni za kiume hawana kinyaa kabisa

Wadada wa saluni za kiume hawana kinyaa kabisa

Ukienda salon yoyote kabla ya kunyoa sali kwanza jikabidhi kwa Yesu Kristo, pia kabidhi nywele zako kwa Yesu. Jifunike kwa Damu ya Yesu, alafu nenda kanyoe.

Nywele zako na mwili wako vitakuwa salama dhidi ya ufedhuli unaofanywa kwenye salon na vinyozi ambao wengi ni maajenti wa kuiba nyota za watu na kuzipeleka kuzimu.
Hii ni point sana niliwahi ona kwenye sherehe maji ya walionawia mikono watu yanahifadhiwa
 
Barbershop ni madanguro ya kisasa, yaani wale wanawake siyo wa kugusa hata kidogo kwa mwanaume anayejitambua, siyo kubinya tu vichunusi, bali wanalala na wanaume chungu mzima aisee
Kwa hiyo sasa mkuu tufanyeje ?i.
 
Wakuu habari za jioni?

Mimi napenda sana kunyoa kwenye Saluni ambazo zinahudumiwa na wakaka Pamoja na wadada. Huwa najisikia Vizuri sana ninapomaliza kunyoa halafu naambiwa nenda chumbani ukaoshwe ambako unaenda na kumkuta mdada Mzuri atakayekuosha, kufanyia scrub, rolls, nk.Lkn mimi huwa naishia tu Kwenye scrub na rolls.

Kilichofanya nije hapa na kisha kuandika huu uzi ni jinsi hawa wadada wasivyo na kinyaa katika kutuhudumia sisi Wakulungwa, Unakuta anakubinya vipele vya kwenye kidevu ambavyo vitatoa usaha, anakuja tena anaibinya pua vinatoka viuchafu fulani hivi wao wanasema ni vimafuta, sasa Unakuta Wakati Mwingine umebanwa na mafua na makamasi yanajitokea tu hovyo, lakini unakuta hawa wadada wala hawajali.

Kama leo hii mdada wa watu ameniminya viupele vya kidevuni na shingoni vikawa vinatoa usaha.

Kamdada kakasema kaka vipele vinatoa usaha!!, Kidume nikajibu ahaaa!!, sawa![emoji23][emoji23][emoji23], Kamdada kakachukua tissue kakanifuta taratibu na vidole vyake vilaini bila kinyaa.

Hakika nawashukuru sana dada zetu Wapendwa wa Saluni za kiume kwa Huduma yenu,pasipo kinyaa.
Ungempa hela ya soda!
 
Back
Top Bottom