Vijana pamoja na kuhonga, msisahau kujiwekeza. Wanawake wapo tu na huwa ni viumbe hawaridhiki. Ukisema umridhishe kwa kumtoa out, kumspoil kwa 100k+ or so kila weekend, itafikia kipindi akiona umeyumba kiuchumi atahama kwa mwingine. Siku hizi wapo na msemo, "tafuta pesa", yes tafuta pesa ila sio kwa ajili yao...kwa ajili yako na future yako.
Jiwekeze, fungua miradi yako, hata ya kuku, chips, genge, fanya mishentown zako ili uingize hela na sio kutoa tu. Tafuta mwanamke mtulivu, anayeelewa kuishi ni nini, sio mdada kila siku anabadilisha viwanja(hawazi kesho), utaishia kulipa kodi ya nyumba hadi ufike 55yrs, utapanda boda na daladala hadi ukome.
Sisemi watu wasifurahie maisha, ila say NO to stupid mizinga, waza kujiwekeza, hizo buku mbili wanazokudharau nazo, ukiziweka kwa mwezi ni 60k, kwa mwaka ni 720k. Na ukiona mtu anadharau kiwango fulani cha pesa, ujue ana unyafuzi katika understanding yake.
Tuishi, tufurahie maisha, ila tuwaze uzee wetu tusije kusumbua watoto wetu tukizeeka.