Wadau hebu njooni tushauriane

Simu used halafu unalalamika Zemanda kweli? Hiyo wanaijua changamoto zake zote, wewe cha kufanya waambie wakubadilishie hiyo waiuze wao..!!

Na ujanja wote wa kupigia kelele wanawake kumbe boya unaingizwa mjini na kina Mr matelephone..!!!
 
Nahisi kioo ndio tatizo
Sijajua kwakweli. Ila ingekuwa kioo ni tatizo basi si ingewaka au ukiipiga iite mbona inasema "namba unayopiga inatumika" na muda huo simu haijawaka.

Sasa me nikaona hii shida itakuwa kubwa niwarejeshee simu yao wanipe nyingine maana wameniuzia changamoto.
 
Waambie wakubadilishie nyingine, na ishu kama hizo mwenye duka atakuwa anaijua sema tu wanakusikilizia.

Ukienda tu huko police ni sawa ununue simu nyingine tatu.
Namsikilizia huyo mwenye duka nimetoka kuongea nae jioni hii. Alinambia atafika shop kisha ajue shida ni ipi then anirejee.

Sasa kama hawatafanya jambo hadi ijumaa mimi nakwenda kwa sura ya ushari sicheki nao tena.
 
Simu used halafu unalalamika Zemanda kweli? Hiyo wanaijua changamoto zake zote, wewe cha kufanya waambie wakubadilishie hiyo waiuze wao..!!

Na ujanja wote wa kupigia kelele wanawake kumbe boya unaingizwa mjini na kina Mr matelephone..!!!
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sahihi umesema kweli.
 
Simu used Zina matatizo sana, na inavyoonekana hawana nia ya kutatua hiyo changamoto Bali wanataka wakuzungushe mpaka ukate tamaa uache kufuatilia
 
KAma hawataki kukupa mawasiliano ya bosi wao waambie kesho nikija sijapata msaada naenda msimbazi police
 
Simu used halafu unalalamika Zemanda kweli? Hiyo wanaijua changamoto zake zote, wewe cha kufanya waambie wakubadilishie hiyo waiuze wao..!!

Na ujanja wote wa kupigia kelele wanawake kumbe boya unaingizwa mjini na kina Mr matelephone..!!!
Ndio maana umegoma kutuma picha ya katress zako sio πŸ˜‚ mdomo
 
WAIT WAJANJA WAKALI WA TOWN WAPIGE FILE CHINI UWEKEWE MPYA NA UTOAMINI UTAIKUTA MPYA NA HAINA CHOCHOTE NDANI πŸ˜‚ USIACHE KUTOA FEEDBACK HAPA DA MTU
 
Kwani huna utaalamu kidogo wa kutengeneza vilipuzi kama vile TNT, gelignite au hata petrol bomb? Muda mwingine unamalizana nao kibabe. Ubaya ubwela!

Hapa natania tu. Usichukulie serious.

Kaanzie polisi. Hii chukulia seriously.
 
Nenda polisi, me kuna fundi alivunja kioo changu wakati anaondoa protector sikuwa na warranty ila nilipoenda polisi msimbazi hapo, haikuchukua muda jamaa akanipa kioo kipya , maana kilikuwa na bei sana zaidi ya 400k, such a loss, in short hao jamaa wanaogopa sana polisi, usiwachekee
 
Simu used Zina matatizo sana, na inavyoonekana hawana nia ya kutatua hiyo changamoto Bali wanataka wakuzungushe mpaka ukate tamaa uache kufuatilia
Lazima warudishe simu mpya ama pesa. Ama sivyo wanakwenda kujibu polisi kwamba pesa yangu wamepeleka wapi.
 
KAma hawataki kukupa mawasiliano ya bosi wao waambie kesho nikija sijapata msaada naenda msimbazi police
Hadi saa hii nimewaendea kistaarabu sijapiga biti,kuwatukana,kuwasha moto au kuwaonyesha any form ya harshness. Nawapa nafasi wanionyeshe customer service yao. Ili nikianza kuwa mkorofi wajue kuwa walinikorifisha.
 
WAIT WAJANJA WAKALI WA TOWN WAPIGE FILE CHINI UWEKEWE MPYA NA UTOAMINI UTAIKUTA MPYA NA HAINA CHOCHOTE NDANI πŸ˜‚ USIACHE KUTOA FEEDBACK HAPA DA MTU
Nataka nione watakachofanya.
 
Nawapa hadi ijumaa maana mwenye duka nimeongea nae leo na anaonekana muungwana so amenambia anashughulikia atanipa jibu kesho. Yeye huwa hakai dukani hata kidogo. Anapita kukagua tu vijana wake ndio kawaacha. Aliyeniuzia simu ndio ananionyesha kiburi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…