Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijajua kwakweli. Ila ingekuwa kioo ni tatizo basi si ingewaka au ukiipiga iite mbona inasema "namba unayopiga inatumika" na muda huo simu haijawaka.Nahisi kioo ndio tatizo
Namsikilizia huyo mwenye duka nimetoka kuongea nae jioni hii. Alinambia atafika shop kisha ajue shida ni ipi then anirejee.Waambie wakubadilishie nyingine, na ishu kama hizo mwenye duka atakuwa anaijua sema tu wanakusikilizia.
Ukienda tu huko police ni sawa ununue simu nyingine tatu.
😂😂😂😂Simu used halafu unalalamika Zemanda kweli? Hiyo wanaijua changamoto zake zote, wewe cha kufanya waambie wakubadilishie hiyo waiuze wao..!!
Na ujanja wote wa kupigia kelele wanawake kumbe boya unaingizwa mjini na kina Mr matelephone..!!!
Sahihi umesema kweli.Ujumbe wa malipo pekee hauchukuliwi kama risiti rasmi kisheria. Ujumbe huo ni uthibitisho wa malipo tu (payment confirmation) unaoonyesha kiasi kilicholipwa, tarehe, muda, na namba ya muamala. Risiti halali inapaswa kutolewa na muuzaji na iwe na maelezo muhimu kama:
1. Jina la kampuni au muuzaji
2. Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN)ikiwa biashara imesajiliwa na TRA
3. Maelezo ya bidhaa au huduma iliyouzwa
4. Kiasi kilicholipwa pamoja na kodi zinazohusika (kama VAT)
5. Tarehe ya muamala
6. Sahihi au muhuri wa kampuni kwa biashara zinazohitaji.
Hilo ndolamuhimuKabisa mzee. Nikiwarejea naenda asubuhi kabisa nitashinda nao pale hadi wanipe muafaka.
Nimenunua simu hivi karibuni kutoka duka moja hapo kariakoo. Sim nimeitumia tokea mwezi wa kumi na moja tarehe 15 mwaka jana (2024). Mwaka huu mwezi wa kwanza kwenye tarehe kama 20 hivi simu ghafla ikazima nikiwa naitumia.
Na ilizima katika hali ya kawaida tu kama imejirestart ila hii haikujirestart ukiwasha inapiga vibration tu kama inastuka ikitaka kuwaka ila haiwaki.
Sijaifungua wala kuipeleka kwa fundi nimeirejesha dukani na walinipa kikadi cha warrant cha miezi 6.
Lakini naona wanajizungusha kunipa majibu kwamba tunafanyaje baada ya hapa. Simu wapo nayo na kijana ambaye yupo dukani anaonyesha ukaidi na kushindwa kunipa ushirikiano ninaotaka baada ya changamoto hii.
Alichosema nisubirie amfikishie boss wake yaani mwenye biashara hiyo issue then atanipa jibu. Tokea ijumaa ya wiki iliyoisha hadi leo jumatano tunazungushana nikiwapigia simu wanasema subiri washughulikie.
Nipeni ushauri nisije nikafanya maamuzi kwa kukurupuka nikaonekana sina hekima au nikakosea nikaonekana mzembe.
Nipeni ushauri.
Ndio maana umegoma kutuma picha ya katress zako sio 😂 mdomoSimu used halafu unalalamika Zemanda kweli? Hiyo wanaijua changamoto zake zote, wewe cha kufanya waambie wakubadilishie hiyo waiuze wao..!!
Na ujanja wote wa kupigia kelele wanawake kumbe boya unaingizwa mjini na kina Mr matelephone..!!!
Kwani huna utaalamu kidogo wa kutengeneza vilipuzi kama vile TNT, gelignite au hata petrol bomb? Muda mwingine unamalizana nao kibabe. Ubaya ubwela!Nimenunua simu hivi karibuni kutoka duka moja hapo kariakoo. Sim nimeitumia tokea mwezi wa kumi na moja tarehe 15 mwaka jana (2024). Mwaka huu mwezi wa kwanza kwenye tarehe kama 20 hivi simu ghafla ikazima nikiwa naitumia.
Na ilizima katika hali ya kawaida tu kama imejirestart ila hii haikujirestart ukiwasha inapiga vibration tu kama inastuka ikitaka kuwaka ila haiwaki.
Sijaifungua wala kuipeleka kwa fundi nimeirejesha dukani na walinipa kikadi cha warrant cha miezi 6.
Lakini naona wanajizungusha kunipa majibu kwamba tunafanyaje baada ya hapa. Simu wapo nayo na kijana ambaye yupo dukani anaonyesha ukaidi na kushindwa kunipa ushirikiano ninaotaka baada ya changamoto hii.
Alichosema nisubirie amfikishie boss wake yaani mwenye biashara hiyo issue then atanipa jibu. Tokea ijumaa ya wiki iliyoisha hadi leo jumatano tunazungushana nikiwapigia simu wanasema subiri washughulikie.
Nipeni ushauri nisije nikafanya maamuzi kwa kukurupuka nikaonekana sina hekima au nikakosea nikaonekana mzembe.
Nipeni ushauri.
Lazima warudishe simu mpya ama pesa. Ama sivyo wanakwenda kujibu polisi kwamba pesa yangu wamepeleka wapi.Simu used Zina matatizo sana, na inavyoonekana hawana nia ya kutatua hiyo changamoto Bali wanataka wakuzungushe mpaka ukate tamaa uache kufuatilia
Hadi saa hii nimewaendea kistaarabu sijapiga biti,kuwatukana,kuwasha moto au kuwaonyesha any form ya harshness. Nawapa nafasi wanionyeshe customer service yao. Ili nikianza kuwa mkorofi wajue kuwa walinikorifisha.KAma hawataki kukupa mawasiliano ya bosi wao waambie kesho nikija sijapata msaada naenda msimbazi police
Nawapa hadi ijumaa maana mwenye duka nimeongea nae leo na anaonekana muungwana so amenambia anashughulikia atanipa jibu kesho. Yeye huwa hakai dukani hata kidogo. Anapita kukagua tu vijana wake ndio kawaacha. Aliyeniuzia simu ndio ananionyesha kiburi.Nenda polisi, me kuna fundi alivunja kioo changu wakati anaondoa protector sikuwa na warranty ila nilipoenda polisi msimbazi hapo, haikuchukua muda jamaa akanipa kioo kipya , maana kilikuwa na bei sana zaidi ya 400k, such a loss, in short hao jamaa wanaogopa sana polisi, usiwachekee
Kweli ni Bora uchukue hatua stahiki mkuuLazima warudishe simu mpya ama pesa. Ama sivyo wanakwenda kujibu polisi kwamba pesa yangu wamepeleka wapi.