Wadau kwa Milioni 17 naweza kujenga apartment 4?

Wadau kwa Milioni 17 naweza kujenga apartment 4?

wewe ni mpumbavu. bila shaka ulikimbia hesabu shule hata hivyo Watu ambao hamjawahi kujenga au kusimamia ujenzi mna mawazo finyu sana

pata elimu hii ya uhalisia.
hiyo apartment unayosema hata iwe na chumba kimoja na sebule jiko na cho utahitaji tofali angalau 1600 kwa uchache ambapo kwa apartment nne ni tofali 6400. ukinunua kila tofali kwa sh 1000 gharama ya tofali zote ni 6,400,000. Katika 17Mil umebakiza 10.6mil

Ukisema ujibane sana kila aprtment mpaka finishing utumie nondo 12 tu kila nondo 18,000 mara aprtment nne ni sh 864000 umebakiwa na tsh9,73,600

cement ukitumia 1.5 ton yaani mifuko 30 mpaka finishing kwa kila apartment utatumia mifuko 120 ambayo kwa mfano ununue kwa 13,000 kila mfuko utatumia 1560000 inabaki 8176000. Gharama za ufundi kwa kila apartment hata ukiwapata mafundi wa bei ya chee kuanzia kuchimba msingi mpaka finishing haipungui 1500000 kwa kila apartment yaani 6mil....umebakiza 2,176,000

vifuatavyo bado hujakamili
Plumbing
electrification-vifaa na fundi
ceptic tank
mbao zote za kushikilia zege na za kuezekea
mabati
misumali
mchanga na kokoto
gharama ya usafirishaji wa matofali na vifaa vingine vya ujenzi kama neno,cement, mabati na mbao

.....NB: Hapo una kiwanja tayari
***************************************************
Acha ujinga, apartment niliyoitaja ni ya chumba kimoja jiko na bafu bila sebule, nikaongeza kuwa zikiwa na sebule zitatoka 3. Hiyo sebule umeweka wewe. Moja ya nyumba zangu ina nyumba 3. Viwili ni self na sebule yenye 3.5m kwa 5.5m na dinning. Nilitumia 2200 blocks na kuingia ndani unapanda ngazi 4. Tena kuna upande una kozi 11 kwa 10 kabla ya kufunga dirisha. Acha uboya. Blocks 1600 unajenga nyumba kamili yenye vyumba 2 vya kulala, sebule, store, choo na bafu. Kwa nondo hizo unazungumzia nyumba yenye mzingo wa mita 48 au 29 kutegemea kama msingi hautaweka au utaweka nondo respectively. Hiyo nyumba yako ni ya 14m by 10m au 8m by 6.5m. Hizo ni nyumba kubwa.
 
4.5m kwa 3m. Upande wenye 4.5m unapunguza 1.5m. Itatoa jiko na choo size 1.5 kwa 1.5 na kubakiwa na chumba chenye 3m kwa 3m. Block za msingi kwa moja ni 150pcs na kuinua 700. Upauaji wa Contemporary
Kwahiyo upauaji wa contemp ni nafuu?
 
Wadau naomben ushaur kwa 17mil naweza kujenga apartment nne zenye room moja ya kulala na sitting room plus choo na jiko?

Msaada tafadhali
Yaani kila apartments igharimu milioni 17 au hiyo milioni milioni 17 ndio apartments zote 4.
 
Inawzekana ila zitakua local sana... Hazina umeme wala maji...
 
Acha ujinga, apartment niliyoitaja ni ya chumba kimoja jiko na bafu bila sebule, nikaongeza kuwa zikiwa na sebule zitatoka 3. Hiyo sebule umeweka wewe. Moja ya nyumba zangu ina nyumba 3. Viwili ni self na sebule yenye 3.5m kwa 5.5m na dinning. Nilitumia 2200 blocks na kuingia ndani unapanda ngazi 4. Tena kuna upande una kozi 11 kwa 10 kabla ya kufunga dirisha. Acha uboya. Blocks 1600 unajenga nyumba kamili yenye vyumba 2 vya kulala, sebule, store, choo na bafu. Kwa nondo hizo unazungumzia nyumba yenye mzingo wa mita 48 au 29 kutegemea kama msingi hautaweka au utaweka nondo respectively. Hiyo nyumba yako ni ya 14m by 10m au 8m by 6.5m. Hizo ni nyumba kubwa.
PIGA HESABU. ACHA UMBUMBUMBU AU HUJUI GHARAMA ZA UJENZI ZILIVYOPANDA KWA SASA. CHUMBA KIMOJA BILA SEBULE UNAKIITA NI APARTMENT.....AKILI YAKO IKOJE WEWE?
 
Zinaitwa studio/efficiency nchini US
Kenya wanaziita bed seaters.
Studio haiqualify kuwa aprtment. Hata hiyo studio kaa chini uipigie hesabu kisha kuanzia kiwanja. Usikurupuke. Utaishia kuikimbia site. Ni rahisi kujenga kwenye fikra na kwenye makaratasi. Ukianza ndipo unakumbana na uhalisia mgumu
 
studio haiqualify kuwa aprtment.
Zinaitwa studio apartments..,
Yaani unampigia real estate agent unamwambia nahitaji studio apartment.
Umeambiwa kiwanja anacho
Screenshot_20210523-084530~2.png
 
Chief nahitaji mahesabu ya kujemga chini tu hapa, itanigharimu kiasi gani, nataka nijenge chini, nivute pumzi nitamalizia juu kipindi kijacho.

Nimejaribu kupandisha ramani yake hapa inagoma..

Idea yake iko hivi chini najenga fremu 5 na geti.. Kisha juu nitajenga fremu 6, ya sita ni juu ya eneo la hilo geti..
Vipimo
Upana wa fremu ni mita 3
Urefu utakuwa ni mita 4.5.
Fremu au apartment UNATAKA NINI...?
 
Kujenga maana yake anacho kiwanja. Apartment maana yake nyumba 4 za kupangisha bila kujali idadi ya vyumba. Hadhi ya apartment ni atleast 4m kwa moja. Kiasi ambacho kinatosha sana kwa chumba choo na jiko lake × 4.
Nyie wenzetu hizi nyumba mnajengea wapi?
 
Back
Top Bottom