Wadau kwa Milioni 17 naweza kujenga apartment 4?

Nyie wenzetu hizi nyumba mnajengea wapi?
Dar es Salaam, watu wengi wana nyumba. Ukifuatilia vipato vyao ndiyo utajua kuwa nyumba ni rahisi tatizo uwanja. Na wengi ujenzi wao si smart hakuna Square. Lakini mwisho wa siku wanatumia material yale yale. Fundi yule yule akijenga na mchina kazi nzuri. Ukimuacha site yako kazi ovyo.
 

Mkuu wasamehe, wengi humu hawajawahi hata kujenga, hawajui hata gharama za ujenzi na materials zipoje , wengine hata milioni 2 hawajahi kushika kwahiyo wakitajiwa mil 17 wanaona kama ni Bilioni.

Ujenzi ni gharama sana,kuna msanii mmoja wa bongo movie alilala na viatu ,alipata dili nono akakamata fedha ya maana ,akamtafuta fundi akampigia mahesabu kuanzia msingi hadi anahamia akampa full quotation ,msanii kweli alikuwa na mzigo wote fresh ,akamwambia fundi aanze ujenzi ,mwisho wa siku alilala na viatu mzigo umekata wote aliishia kupaua na kuweka grill na plasta tu.

Kwenye ujenzi fundi akikwambia gharama ya kitu flani kujenga basi inabidi uwe na balance nyingine ya ziada kwa vitu vidogo vidogo vitkavyotokea ,mara nyingi mafundi wanaweka gharama ndogo ili uanze maana wanajua ukishayavulia nguo maji lazima uyaoge ,akikutajia gharama kubwa utashindwa kuanza,anakutajia ndogo ili uanze ,kwahiyo kama haujui mahesabu ni bora uwe na balance ya ziada.
 
Ni kweli atusamehe, maana sisi kwetu tukilipa buku block mpaka site. Sasa yeye anakokujua akilipa block usafiri juu yake na anataka kote iwe hivyo.
 
Sawa
 
Ujenzi siyo maneno tu, ni mahesabu. Ndiyo maana watu wengi ambao hawajajenga huwa na vimaneno vya dharau.
Nyumba zipo za aina nyingi sana siyo lazima uige. Siyo lazima iwe na tiles, gypsum, aluminum windows, grills ....
Siyo lazima na nyumba inakuwa nzuri tu.
 

Ni kweli mkuu.
 
Nyie mafundi wezi sana. Yaani chumba, sebule na jiko unataka at least block 1600?
 
Nyie mafundi wezi sana. Yaani chumba, sebule na jiko unataka at least block 1600?
Kama kuna fundi amekwambia unaweza ukatumia matofali mia mbili amekudanganya. Labda kama unataka kujenga bafu la uchochoroni. Siku ukianza ujenzi, utaujua ukweli na utarudi humu kutafuta huu uzi unishukuru.

Na kama kuna fundi amekwambia 17mil inatosha apartment nne na umemuamini nakupa pole, huwajui mafundi ujenzi walivyo. Ukimtangazia kazi hata ukimwambia una 10mil unataka kujenga ghorofa atakwambia tuanze inawezekana maana yeye anajua atalipwa kutokana na kazi anayoifanya.....msala wa kumaliza au kutomaliza ujenzi ni juu yako.

Wengi mnaodhani 17mil inatosha si ajabu hamjui hata bei ya roofing materials zote, bei ya cement, kokoto, rangi na materials zingine zote zinazohitajika wakati wa finishing na ujenzi mzima pamoja na logistics zake.

Endeleeni kudanganyana, maana millenials mkishavuta bangi mnaona 17mil ni 17bil
 
Aisee nimeshangaa labda hajui block 1600 ni zipi.
Nimewahi simamia ujenzi hata sasa nafuatilia block kwa ajili ya fensi.
Hazifiki tofali 1600 kwa chemba,sebule na jiko

Mkuu inategemea na size ya chumba, sebule, jiko na choo ila kwa standard ya ujenzi yaani chumba kiwe na atleast 4m kwa 4m, sebule 4m kwa 5m,jiko 3m kwa 4m na choo 3m kwa 5m,corridor 2.5m, msingi uinuke juu na baada ya linta unapiga kozi 3, hizo tofali 1600 zinaweza kupelea na zisitoshe.....

Kama ujenzi wa ramani kidole chumba vya futi 8 au 10 na vyoo vya kuingia upande upande na korido watu wawili hamuwezi kupishana unaweza ukatumia tofali unazosema wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…