Wadau na wajasiriamali, naomba kujuzwa kuhusu Mr. Kuku Farms na uhalisia wa aina ile ya biashara

Wadau na wajasiriamali, naomba kujuzwa kuhusu Mr. Kuku Farms na uhalisia wa aina ile ya biashara

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
70,785
Reaction score
186,690
Juzi kuna jamaa yangu kanipigia simu akawa ananieleza vitu sivielewi elewi.

Ni kitu kinaitwa Mr. Kuku Farms akidai ni mradi mkubwa wa ufugaji kuku una physical presence na ni kampuni iliosajiliwa ndio inaendesha huo mradi.

Yeye ameshawishika kuwekeza huko kwamba kuna faida nzuri compared na kuweka hela benki tu ikiwa baada ya miezi 3 unaweza draw 70% ya ulichowekeza na baada ya miezi sita una uwezo wa kuchota 100% ya pesa yako.

Kama tujuavyo kwamba mtu alieng'atwa na nyoka huwa haishi maseke hata anapotambaliwa na jani, basi lazma atarusha miguu tu.

Naomba kwa heshima na taadhima niambiwe na wadau wenzangu wajasiriamali kwa wafanyabiashara. Je, huu mradi ni halisi?

Ni business model gani wanatumia? Na je, kuna hiyo leverage ya kupelekea kutoa gawio kwa rates hizo kwa muda wanaodai wanaweza?

Kama kuna ambaye amepiga hela kupitia hao jamaa aje amwage terms zao na ushuhuda kuwa kapiga dough kweli.
 
Mama yangu aliniambia nimtumie hela anataka kufanya mradi wa kuku bila kufuga.nilishangaa nikamdodosa kwa kina naye anajiuma uma tu. Refer kipeperushi hiko labda nitapata mwangaza maana kaomba dola 500 za Canada.

Naomba mwangaza.

IMG-20200313-WA0005.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu bana, yaani jambo linaonekana tu kwa macho ya kawaida kua hii ni Ponzi Scheme au Pyramid Scheme mtu bado unajiuliza maswali mara mbili mbili?

Hao wenye hiyo kuku farm kwa nini wasiuze kila walichonacho na wawashawishi ndugu zao wauze kila walichonacho wawekeze kwenye hiyo project wapige hela wawe familia tajiri zaidi? Au unadhani hao jamaa wa kuku farm wanawapenda sana kuliko wanavyowapenda ndugu zao? Kwamba waone fursa wasiwaambie ndugu zao waje kuwambia nyie? Uliwahi kuona wapi?

Kila siku humu tunatahadharisha kua ukiona unaitwa kwenye deal ujue wewe ndie deal, ukiona unaitwa kwenye fursa ujue wewe ndie fursa. Wazungu husema when the deal is too good think twice. Hakuna hela inapatikana kwa haraka hivyo.

Ilikuja D9, Deci, Qnet, One coin, sijui vitu gani watu wanapigwa kila siku lakini hawajifunzi.

Hao wa kuku farm wape muda mfupi utaona mada zao humu, ni jambo la muda tu.
 
Serikali imelala ktk hili. Mtu anakusanyaje PESA kwa watu? Anafuata utaratibu upi wa Kisheria? Kwanini asipeleke soko la hisa na mitaji? Kuna mchezo kama wakati wa DESI hapo kwa kivuli cha ufugaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
Umehoji kitaalamu kabisa ila kwa lugha nyepesi ambayo hata mtu aliyeishia darasa la pili anaweza kuelewa. Safi sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama yangu aliniambia nimtumie hela anataka kufanya mradi wa kuku bila kufuga.nilishangaa nikamdodosa kwa kina naye anajiuma uma tu. Refer kipeperushi hiko labda nitapata mwangaza maana kaomba dola 500 za Canada.

Naomba mwangaza.

View attachment 1388373

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii chema sijawahi kuisikia, af mbona kama upepo wa hela umehamia huku! Mmh nimepata mashaka zaidi.
 
Serikali imelala ktk hili. Mtu anakusanyaje PESA kwa watu? Anafuata utaratibu upi wa Kisheria? Kwanini asipeleke soko la hisa na mitaji? Kuna mchezo kama wakati wa DESI hapo kwa kivuli cha ufugaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwani anakusanya pesa kwa fix(maneno matupu) na si kwa kuuza mazao yatokanayo na ufugaji wake huo anaoutangaza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom