Wadau, naombeni mawazo yenu! Maana nahisi kuvurugwa...

Ndugu wa kibongo ni kwa ajili ya kukuzika tu ili mzoga wako usinuke, uwachie mali zako wafuje, wawanyanyase wanao na familia yako.

Ni ndugu wachache sana wanaothamini hatua zako kimaisha. Undugu wetu ni kama wa mdudu kaa.
 
Kosa lako ni kutokujua yapi ya kumshirikisha na yapi si ya kumshirikisha, mambo mengine yalipaswa kujulikana kwa mke wako na watoto wako tu. Sasa hapo chukua uamuzi wa kutengana naye kwa uzuri kama ilivyokuwa kwa Ibrahimu na Lutu.

Mfano mzuri sana. Kumbe haya mambo sio sisi tu wabongo ni human nature
 
Achana na anachoweza au asichokiweza wewe mtoe katika maisha yako ubakize undugu tu.
 
Hapo ndipo KIJICHO CHA HUSDA (Evil eye) kinapoingia . Anayekuhusudu huwa hatoki mbali.

Ulipokosea ni kumwambia afanye kazi bila ya makubaliano ya kulipana. Ungemuajiri na kumwambia kwa kazi atakayofanya kwako utamlipa kiasi kadhaa...hapo usingekuwa na dhima juu yake...ulichokosea ni kufanya nae kazi kishkaji
 
Ushauri wangu

Kama utaweza wewe endelea kuwekeza kwenye real estate & biashara ambazo unajua hazita muhitaji yeye .

Nayeye mgawie sehemu ya miradi yako ajitegemee kivyake na familia yake .
 
Kosa sio lake ila la kwako mwenyewe, ulimpa kazi na misaada bila mipaka.
Ukaishi nae bila mipaka na sasa anataka umuwezeshe bila mipaka.

Issue ni moja, mtu baki ukimuajiri na ukamfanyia yote hayo, pengine angekuchukulia kama mkombozi na mtu bora katika maisha ila kwa ndugu yako. Kwanza anaona wewe kumpa push ni kitu anachostahili

Hapimi msaada wako kwa kile ambacho hana ama umempigisha hatua kiasi gani ila anaupima msaada wako kwa kile unachokiingiza na uwezo wako kiujumla vs kile anachokipata . Na kwa kuwa hukumpa mipaka wala kumfanya awe provider kwa familia yake kiasi cha kubeba majukumu ya familia Yake, anaona ni jukumu lako kumvusha hapo alipo na si atumie kipato anachokipata kupiga hatua

Unaonekana unampenda sana na unatamani umfurahishe (people pleaser). Kama unaweza kuendelea kujiumiza ili afurahi, endelea. Kama umechoka, fanya unachotakiwa kufanya ila uwe tayari kwa vita, haiepukiki🙏🏽
 
Ndugu msaidie akiwa mbali,usichanganye kazi/biashara na undugu au urafiki. Hayataenda.
 
Ndugu wa kibongo ni kwa ajili ya kukuzika tu ili mzoga wako usinuke, uwachie mali zako wafuje, wawanyanyase wanao na familia yako.

Ni ndugu wachache sana wanaothamini hatua zako kimaisha. Undugu wetu ni kama wa mdudu kaa.
Umesema vyema mkuu, hayo mambo ya kuweka ndugu kwenye biashara tuwaachie wahindi na waarabu,sisi hatujafika huko. Familia chache sana wameweza.
 
Kosa lako ni kutokujua yapi ya kumshirikisha na yapi si ya kumshirikisha, mambo mengine yalipaswa kujulikana kwa mke wako na watoto wako tu. Sasa hapo chukua uamuzi wa kutengana naye kwa uzuri kama ilivyokuwa kwa Ibrahimu na Lutu.
Mke tena?,si bora mara 100 kaka yake.Kitu chochote cha kumshirikisha mke kwa 100% ni hatari katika maisha ya mwanaume.
 
Inaonesha hujui kumanage biashara! Biashara ina boss na mfanyakazi. Mfanyakazi analipwa mshahara, hapewi zawadi kama lawalawa. Ni marufuku kugeuza ndugu kuwa mfanyakazi. Nina maana undugu upo nyumbani na kazini hata akiwa ni mama yako, wewe ni boss na yeye ni mfanyakazi anakutii kama mwajiri. Familia ikiugua anatibiwa na bima. Mtoto wake akitaka kwenda shule anakopa kama mfanyakazi. Sema unaweza kumwongeza mshahara tu. Mkiwa nyumbani ni marufuku kuzungumzia biashara maana yeye sasa ni kaka na wewe ni dogo. ETC. Mimi nimemuajiri mtoto wangu wa kumzaa, lakini akiomba pesa namuuliza huna mshahara? Akikopa anakatwa katika mshahara. Kazini anapoingia kazini hawezi kuniaddress Dad!
 
Ishu ndogo hio, tumia mbinu ya kimagharibi, muulize ni biashara Gani anaimudu na kuamini ina mafanikio, akiitaja hata kama inahitaji mtaji mkubwa ifungue then mkabidhi mwambie hio yakwake na umpe miezi SITA aanze kujitegemea Kwa kila kitu, hakikisha ukoo wenu wote unajua Hilo, ili akifanya uzembe usilaumiwe na mtu, watu wengine ukimsaidia wanadhani wewe ndo una shida nao wanaanza kudeka
 
Umezungumzia kiukubwa sana mkuu biashara yangu haijafika level hiyo ..nimelipokea
Mkuu Mungu akubariki the way umeongea ni kama tunaishi wote
 
Umezungumzia kiukubwa sana mkuu biashara yangu haijafika level hiyo ..nimelipokea

Mkuu Mungu akubariki the way umeongea ni kama tunaishi wote
Pamoja kaka, Mungu akupe hekima ya kuvuka mkuu 🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…