Wadau tupunguze bajeti ya pombe, tusaidie ndugu na majirani wasio na uwezo. Hali mtaani ni ngumu sana

Wadau tupunguze bajeti ya pombe, tusaidie ndugu na majirani wasio na uwezo. Hali mtaani ni ngumu sana

Ila ni kweli. Watanzania tubadilike. Matajiri wa kati wa kibongo wengi wao hawapendi kusaidia ndugu zao. Hujilimbikizia mali ili kutafuta sifa ndani ya familia, ukoo na jamii kwa ujumla.

Kinachokera katika ukoo! Ikitokea labda msiba au magonjwa, matajiri wa ukoo huweka viwango flat vya mchango wakati vipato vinatofautiana kwa wanaukoo!

Matajiri wa kibongo wanafki sana. Mtu ana biashara ya kumuingizia faida laki tano kwa siku, ila ukikutana nae analia njaa, eti hali ngumu. Yaani anafanya defensive mechanism. Anahisi utamuomba hela.

Dawa ni kupambana tu!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna watoa misaada kama walevi kama haujui Hilo ndio ujue Sasa ..... Nyie mnajuaga kuvaaa na kununua migari tu kuonyesha ufahari mlevi Hana ratiba hizo .... Mi nimeshuhudia kabisa hivi amekunja kanisani baada ya Misa msoma matangazo akasoma kuna mama anashida yupo hapo nje mwenye chochote wapite wamsaidie.

Padre mmoja mjinga sana (samahani nashukuru na parokiani kaondolewa karudishwa India) akazuia waumini kumpa pesa Wala msaaada pale itakusanywa ipelekwe kanisani ndio apelekwe hospital mtu yupo na Mtoto na Hali ni mbaya ...pembeni tu ya parokia Kuna bar Tatu .... Alipitapita humo na sie wengine hatukupeleka kwanza Baraka nyumbani tulikuwa sehemu Moja wapo tunakemea kemea uzee akapita .... Na mule baa akachangiwa fastaaa 50 na akaitwa mtendaji na Mtu wa afya(bima akakatiwa Chf iliyoboreshwa akaendelea na taratibu za matibabu ya mtoto.

Huu upumbavu ndio ulinifanya had leo nizalau waumin wengi. Yan padri anakwambia usimchangie mtu mwenye shida na ninyi mnakaa kimya tu!? Kisa kiongozi wa kanisa kasema!? Huo ni utumwa wa hali ya juu
 
Ila hali ni tete,kuna watu wanakosa hata jero la kuchekia mpira banda umiza
 
Binadamu ni kati ya viumbe vya hovyo kabisa kuwahi kuishi hapa duniani. Wakati mwingine hua napata mashaka sana kama binadamu kweli ni viumbe wa Mungu!

Unaambiwa hapa duniani, kuna utajiri wa kutosha kabisa kuwafanya binadamu wote waishi maisha "decent" na wapate huduma zote muhimu, lakini ni 1% ya wanadamu ndio wanashikilia 99% ya utajiri! Haya jiulize huo utajiri wanaufanyia nini? Ni starehe.., wanawake.., show off, ulevi, umalaya, kamari, nk.. Wakiona wamechoka wanaanza kuua wenzao huku wao wamekaa pembeni wanaangalia kama kule Ukraine.
Hakuna starehe kubwa Kama kutest mitambo uliyoigundua kwaakili yako kiongozi yuopo sahihi hataingekua Mimi eti niigundue sukhoi55 alafu nisianzishe Vita weee nanikasema
 
Kwa hiyo serikali ya fisiemu inaomba msaada kwa wanyonge wa danganyika......huko arabuni kapu limeshindikana kujaa. Watu wakiambiwa wakae pembeni wanaona wanaonewa.........twende tu mdogo mdogo tutafika.
 
Kama ulikua huna uwezo wa kuhudumia familia yako (mke na watoto wako) kwanini ulioa? Au kwanini ulizaa watoto wengi kuliko uwezo wako? Kuna familia duni nazifahamu, kila mwaka wanafyetua watoto. Wamepangana watano na wanapishana kama mwaka hadi mwaka na nusu. Mimi nina mtoto mmoja, niliona bora niwe na mtoto ninayeweza kumhudumia na kunywa pombe. Leo uniambie nisinywe pombe nikasaidie kutunza familia kama hiyo?
 
kuna mtu nilimuona analipia wine bar tsh 180,000. Toka siku iyo nikaacha kabisa kwenda bar... ni uwendawazimu
Wengine wananunua nyapu inayofanana na ya mkewake nyumbani kwa mamilioni ya pesa kisa tuu ni mpya kwake ilihali ni used wa wengine
 
Mimi napingana na wewe...hao unaowaita wenye hali ngumu ndio wachawi wetu huku mitaa ya uswaz..ukivaa vizuri ukapendeza roho zinawauma sana..nasema hivi hakuna kuwasaidia wacha wafe by Robert heliel..
 
Hali imekuwa ngumu sana maana maisha yamekuwa tight.

Utakuta jirani yako au ndugu yako hana chakula, mavazi hata watoto wake hawana mahitaji ya shule.

Lakini unakwenda baa unazungusha round za kibabe. Mbaya zaidi inakuwa kila siku.

Kwa hiyo kama kwa wiki unatumia laki kwenye pombe basi punguza utumie sitini elfu, halafu elfu arobaini saidia ndugu na jamaa zako. Nunulia hata watoto wa majirani wasio na uwezo madaftari.
Kwaresma njema mkuu,asante kutukumbusha
 
Hakuna watoa misaada kama walevi kama haujui Hilo ndio ujue Sasa ..... Nyie mnajuaga kuvaaa na kununua migari tu kuonyesha ufahari mlevi Hana ratiba hizo .... Mi nimeshuhudia kabisa hivi amekunja kanisani baada ya Misa msoma matangazo akasoma kuna mama anashida yupo hapo nje mwenye chochote wapite wamsaidie.

Padre mmoja mjinga sana (samahani nashukuru na parokiani kaondolewa karudishwa India) akazuia waumini kumpa pesa Wala msaaada pale itakusanywa ipelekwe kanisani ndio apelekwe hospital mtu yupo na Mtoto na Hali ni mbaya ...pembeni tu ya parokia Kuna bar Tatu .... Alipitapita humo na sie wengine hatukupeleka kwanza Baraka nyumbani tulikuwa sehemu Moja wapo tunakemea kemea uzee akapita .... Na mule baa akachangiwa fastaaa 50 na akaitwa mtendaji na Mtu wa afya(bima akakatiwa Chf iliyoboreshwa akaendelea na taratibu za matibabu ya mtoto.
wanywaji na walevi tuna roho nzuri sana....Tujipongeze kwa hilo
 
Back
Top Bottom