Tony254
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 16,017
- 16,431
Wadau huwa tunapigana vita sana huku lakini ukweli usemwe kwamba nchi hizi mbili zikiweka vita kando tunaweza kufanya biashara nzuri sana. Baada ya miezi 11, biashara kati ya Kenya na Tanzania imefikia 905 million dollars na hapo ikumbukwe kuna mwezi moja bado haujahesabiwa. Rais wenu yule aliyechukia Kenya sana na kuzuia mahindi yenu yasiuzwe Kenya, na kufunga mipaka na kadhalika alifanya uhusiano huu udhoofike sana. Sasa baada ya mama kuingia, biashara imenoga na hata Wakulima wenu wanafaidika.
Njia hii ya urafiki ndio njia nzuri maana kila mtu anapata pesa. Hakuna haja ya vita kila wakati. Huyo mwamba wenu alikuwa mzuri sana kwenye kuwajengea miundombinu lakini alikuwa mbaya sana kwenye kujenga uhusiano na nchi jirani.

Tanzania, Kenya trade approaches $1 billion mark | The Citizen
www.thecitizen.co.tz